Watawala wa Afrika wameifanya Afrika kuwa "shithole place". Msijisahaulishe kuhusu sisi wenyewe kubaguana kwa rangi na dini zetu. Civil War sisi ndio wataalam, magonjwa, njaa and political malaise, Afrika ndio sehemu yake. Sasa kwanini wasitupe majina ya kukera kwa sababu hizo?
Nchi ambayo "a well pardon rapists and children molesters" wanapata 'a clean mogul consideration', wanapewa msamaha kutoka gerezani, wanapata mwaliko kwenda Ikulu, serikali inawapeleka studio. wanatumbuiza kwenye sherehe za kitaifa. Bado tu hamtaki kuitwa "SHITHOLE countries"
Mbunge/diwani anajiuzuru. Baadae anaomba tena nafasi ya kugombea nafasi ambayo alijiuzuru awali. Wakati kata/jimbo kuna huduma Duni za jamii. Pesa inapelekwa kurejea chaguzi za wajinga hao. Kwanini tusiitwe "SHITHOLES?". Tunastahili kuitwa hivyo. (Tundu la choo cha shimo)
Unamchukia TRUMP kwa kusema ukweli? Ndio, ukweli. Mmekubali kupewa hadi misaada ya KONDOMU kwanini asiwaite "SHITHOLES?", mmekubali kupewa misaada hadi ya VYANDARUA. Trump anatukumbusha wajibu wetu kwa nchi zetu. Viongozi watengeneze nchi zetu. Tuache kuwa WAHAMIAJI haramu.
Choo cha shule kinaanguka. Kilijengwa na wakoloni (ambao ni wazungu). Sisi tunashindwa kutengeneza. Wanakuja wafadhili kutoka Marekani na kutengeneza matundu ya vyoo vya shule. Wanaweka alama "msaada wa watu wa Marekani". Kwanini TRUMP asituite "MATUNDU YA VYOO VYA SHIMO?"
Trump sio tapeli. Anatekeleza alichowapa ahadi Wamarekani. Theme yake ni "MAKE AMERICA GREAT AGAIN" na alisema atawafanya Wamarekani kuwa kipaumbele chake kwanza. Kwanini tumshangae kutumia kauli kali dhidi yetu? Ndio, ni Rais wa USA sio mwafrika yule. Anatekeleza ahadi zake.
Trump yupo sahihi. Africa kuna 'SHITHOLES countries' nyingi. Mfano, nchi ina mbuga za Wanyama, bahari, maziwa, milima, dhahabu, Almasi, Gesi, Rubi. hiyo nchi bado inaomba msaada wa kujenga miradi ya maendeleo na inashindwa kutoa mikopo ya elimu ya juu kwa wanafunzi wake.
Wakati ni huu sasa, Waafrika waache kupeleka taaluma zao ulaya na Marekani. Wazitumie kujenga nchi zao. Wazitumie tasks zao ipasavyo Afrika. Ili Afrika iweze kusimama na kuwa na hadhi ya USA siku moja. Kwanini kuishi kwenye nchi ambayo hamtakiwi na mnang'ang'ania?