Mkuu mimi nikiwa mdau mkubwa wa masuala ya teknolojia ya mawasiliano mara zote ufatilia habari zinazo husu nyaja za mawasiliano Duniani kwa ukaribu sana. Kitu cha kwanza Trump anashinikizwa na Wabunge wanao tumwa na makampuni ya uudaji vifaa vya mawasiliano huko Amerika kuwasingizia Wachina kwa shtuma za kutunga tu hasa wakiona biashara au ushindani unakuwa mkubwa - kitu cha kwanza ni kikimbilia kulahumu kampuni za nje zinazo Wapa changamoto wanakwenda mbali zaidi kwa kudai eti Wachina wana waibia teknolojia as if Vyuo Vikuu vya Uchina na Mataifa mengine hawafundishi masuala ya Solid State Physics na jinsi ya ku-design na ku-manufacture Very Large Scale Integrated Circuits - ajabu kweli kweli!! Wamejaa Dharau na propaganda za kitoto mwanzo mwisho.
Nani ambaye hajui kwamba kampuni ya ZTE wako very innovative wanaunda vyombo vya mawasiliano na Systems bora zaidi kuliko za huko Marekani, kwa nini Trump hajiulizi ilikuwaje Wizara ya ulinzi ili-prefer kununua simu za mkononi na vyombo vingine vya mawasiliano kutoka Uchina (ZTE) wakavisambaza karibu kwenye idira zote, sasa swali: kwa nini MoD haikununua vinavyo undwa huko Merikani? Baadae kumpuni ya kichina ikajengewa mizengwe kwa kudai eti simu na system za ZTE zimewekewa an embeded programs zikufanya ujasusi na kutuma taarifa Uchina, simu na vifaa vyote vya ZTE vikaondolewa kwenye Wizara ya Ulinzi, Trump Govt walikusudia waende mbali zaidi kwa kupiga marufuku vifaa hivyo visiuzwe nchini Merakani -sijui mwisho wa siku walishitukia nini wakasema simu zinaweza kuuzwa kwa Raia wa kawaida na sio kwa watu wanao husika na idara za ulizi na upelelezi.
Nimesema haya yote kuonyesha jinsi gani wenzetu wasivyo penda ushindani wa kibiashara, watasema lolote kutaka kuwaondoa wenzao kwenye soko - hawana simile hata; hivyo kauli ya leo ya Trump ni ya kinafiki kuna kitu ameshitukia kwamba Wachina na wao wana njia zao ya kulipiza kisasi kwa kampuni za Marekani zinazo fanya biashara na Uchina - Chinese are very crafty they know to hit you where it hurts the most - si watu wa kuchukulia kimzaa mzaa hata kidogo.
Kwa leo naishia hapa siku nyigine ntazungumzia kuhusu kampuni nyingine maarufu ya Uchina(Huawei) inayo uunda vifaa vya mawasiliano/systems ntazungumzia kuhusu adha wanayo kumbana nayo nchini Marekani. In a nutshell - regardless ya kauli ya leo ya Trump tukae tukijua kwamba Amerika hata siku moja haiwezi kuonea huruma washindani wao wa biashara - lini Taifa la man eat man likajali binadamu wenzake - lini?