ze kokuyo
JF-Expert Member
- Jan 24, 2014
- 7,476
- 9,654
Rais Donald Trump amesema kuwa anatafuta njia ya kuruhusu kampuni ya teknolojia ya China kurudi kufanya biashara haraka” baada ya uamuzi wa kibiashara wa Marekani kudhoofisha vibaya sana kampuni hiyo.
Trump mara nyingi amekuwa akilalamika juu ya China kuiba kazi za Marekani. Lakini alituma ujumbe wa tweet kuwa anashirikiana na Rais wa China Xi Jinping kupunguza makali ya kuanguka kiuchumi kwa kampuni hiyo ya ZTE.
“Kazi nyingi zimetoweka China. Wizara ya Biashara imeamrishwa kurekebisha hilo!” Trump alituma ujumbe wa tweet Jumapili, siku chache baada ya kampuni ya ZTE kutangaza imesimamisha “shughuli za operesheni zake kuu.”
Kampuni hiyo iliwekewa vikwazo (baada ya kuuza bidhaa zake ambazo Zina teknolojia ya Marekani kwenye nchi nyingine zilizowekewa vikwazo vya kibiashara na Marekani ikiwemo Iran na Korea kaskazini) vya kuizuia kutumia teknolojia ya Marekani kwenye vifaa vyake ikiwemo vipuli ambavyo vinahitajika na ZTE kutengeneza vituo vya mawasiliano ya Simu, mitandao ya mkongo na simu za mkononi za kisasa.
Marekani iliitoza faini ya Dola za Marekani bilioni 1.2 kampuni ya ZTE mwaka 2017.
Ila vikwazo vya hivi Sasa vimeiharibu vibaya kampuni na kusababisha maelfu kukosa kazi.
In About-Face on Trade, Trump Vows to Protect ZTE Jobs in China