Trump asema Ukraine itahitaji makombora ya Patriot kujilinda

The Zanzibar Echo

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2025
Posts
490
Reaction score
836
Rais wa Marekani Donald Trump alisema Ukraine itahitaji makombora ya Patriot kwa ajili ya ulinzi wake, baada ya kuzungumza na Rais Volodymyr Zelensky siku ya Ijumaa, na kueleza kukatishwa tamaa na Rais wa Urusi Vladimir Putin kushindwa kusitisha mapigano.

Trump aliwaambia waandishi wa habari ndani ya Air Force One kwamba alifanya mazungumzo ya simu na Zelensky, akirudia kwamba "hakufurahishwa" na mazungumzo ya simu na Putin siku moja kabla, kutokana na kile alichokiita kukataa kwa kiongozi huyo wa Urusi kusitisha mapigano.

Alipoulizwa kama Marekani itakubali kusambaza makombora zaidi ya Patriot kwa Ukraine, kama alivyoombwa na Zelensky, Trump alisema: "Watayahitaji kwa ulinzi... Watahitaji kitu kwa sababu wanashambuliwa sana."

Trump alipongeza ufanisi wa makombora ya Patriot, akiita silaha hiyo "ya kipekee mno."

Alipoulizwa kuhusu matarajio ya kusitishwa kwa mapigano, Trump alisema, "Ni hali ngumu sana... Sikufurahishwa sana na mazungumzo yangu na Rais Putin. Anataka kwenda mbali zaidi, aendelee kuua watu tu - sio nzuri."

Zelensky alisema amekubali kuimarisha uwezo wa Kyiv wa "kulinda anga" wakati mashambulizi ya Urusi yanaongezeka, akiongeza katika ujumbe kwenye Telegram kwamba alijadili uzalishaji wa pamoja wa silaha za ulinzi, pamoja na ununuzi wa pamoja na uwekezaji na kiongozi wa Marekani.
 
Hili beberu huwa lina ubinadamu, ni ulimwengu tu na walimwengu ndio wanalichanganya
 
I still repeat

No Man will be buried uncircumcised, as long as I'm still working at the mortuary
Una tatizo la akili wewe, kwahiyo unajiona mjanja kucomment huu upumbavu kwenye kila post!? Utakuwa kocho si bure maana "mtoto wa kiume" kuzungumzia govinda za wanaume wenzio sioni kama imekaa sahihi! Lazima wanakupakua
 
Rais wa Marekani Donald Trump alisema Ukraine itahitaji makombora ya Patriot kwa ajili ya ulinzi wake, baada ya kuzungumza na Rais Volodymyr Zelensky siku ya Ijumaa, na kueleza kukatishwa tamaa na Rais wa Urusi Vladimir Putin kushindwa kusitisha mapigano.

Trump aliwaambia waandishi wa habari ndani ya Air Force One kwamba alifanya mazungumzo ya simu na Zelensky, akirudia kwamba "hakufurahishwa" na mazungumzo ya simu na Putin siku moja kabla, kutokana na kile alichokiita kukataa kwa kiongozi huyo wa Urusi kusitisha mapigano.

Alipoulizwa kama Marekani itakubali kusambaza makombora zaidi ya Patriot kwa Ukraine, kama alivyoombwa na Zelensky, Trump alisema: "Watayahitaji kwa ulinzi... Watahitaji kitu kwa sababu wanashambuliwa sana."

Trump alipongeza ufanisi wa makombora ya Patriot, akiita silaha hiyo "ya kipekee mno."

Alipoulizwa kuhusu matarajio ya kusitishwa kwa mapigano, Trump alisema, "Ni hali ngumu sana... Sikufurahishwa sana na mazungumzo yangu na Rais Putin. Anataka kwenda mbali zaidi, aendelee kuua watu tu - sio nzuri."

Zelensky alisema amekubali kuimarisha uwezo wa Kyiv wa "kulinda anga" wakati mashambulizi ya Urusi yanaongezeka, akiongeza katika ujumbe kwenye Telegram kwamba alijadili uzalishaji wa pamoja wa silaha za ulinzi, pamoja na ununuzi wa pamoja na uwekezaji na kiongozi wa Marekani.
Trump kigehu gehu sana, yaani atabiriki leo kasema hili kesho kasema lile, lakini mimi nilisha mshitukia siku nyingi kwamba hana nia thabiti ya kumaliza mgogoro huu wa Ukraine, anataka mgogoro uendelee ili viwanda vya silaha vya Merikani vifanye biashara, we angalia amekwisha kutana na Zelensky ana kwa ana zaidi ya mara nne tangu achaguliwe tena kirudi White House, lakini kwa makusidi hataki kukutana na Putin ana kwa ana anampigia simu tu na baadae kudai eti "Putin inaelekea hataki kumaliza mgogoro WA Ukraine" Trump anajifanya ku-ignore madai ya Putin ya kumaliza mgogoro, na hii ya Trump kubadirisha maoni kumuhusu Zelensky inatokana na nini kwa kujifanya kuwa karibu nae siku za hivi karibuni,?

Ukweli ni kwamba iinatokana na Trump kukubaliwa na Zelensky achimbe madini adimu kutoka Ukraine na kuyasafirisha kwenda Merikani, ni hilo tu.

Binafsi naona Putin atangaze vita kamili dhidi ya Ukraine bila ya kujali kama Merikani au NATO watajiingiza kwenye mgogoro huo, bila ya kufanya hivyo Ukraine itaendelea kupigana a proxy war wakisaidiwa na Mataifa ya magharibi akiwemo Trump mwenyewe kwa kificho, Putin akifanya makosa kwa kuchelea kufanya mahamuzi hayo magumu, basi Putin abaki akijua kwamba Zelensky atamsumbua sana kutokana na msaada anao upata kutoka nchi za magharibi!!

Hivi sasa naona Trump anamchezea akili Putin kwa kumpigia pigia simu zisizo kuwa na kichwa wala miguu, lakini Trump hataki kukutana na Putin ana kwa ana, kesha pewa biashara ya Madini adimu na Zelensky ya Ukraine unafikiri Trump kama mfanya biashara ndiye atataka vita hii isitishwe, thubutu - nawapa wiki mbili mtamsikia Trump akimlahumu Putin kwamba anaishambulia sana Ukraine kwa hiyo Ukraine inahitaji silaha za ulinzi wa anga kutoka Merikani, lakini Zelensky alipo shambulia airbase ya Urusi na kuharibu baadhi ya ndege za kijeshi za Urusi sikusikia Trump akisema chochote.

Bottom line is: Trump kama walivyo maafisa wengi WA kijeshi wa Merikani wanataka Urusi iwe destroyed totally na mpango huu nchi za magharibi zilikiwa nao tangu mapema mwishoni mwa WW2 wakishawishiwa na Waziri mkuu WA Uingereza wa wakati huo Bwana Winston Churchill, sasa swali ni:je, hivi Urusi ya hivi sasa inaweza itakubali kweli kushindwa hata kama majeshi yote ya NATO yakata shauri kuivamia - personally I don't think so, else it gonna be the end of the World as we know it, sijui mataifa ya magharibi yana kichaa gani cha kutaka kuona Dunia yote inateketea!! Wakisumwa na chuki zao binafsi kuhusu Urusi sijui kwa nini???
 
Rais wa Marekani Donald Trump alisema Ukraine itahitaji makombora ya Patriot kwa ajili ya ulinzi wake, baada ya kuzungumza na Rais Volodymyr Zelensky siku ya Ijumaa, na kueleza kukatishwa tamaa na Rais wa Urusi Vladimir Putin kushindwa kusitisha mapigano.

Trump aliwaambia waandishi wa habari ndani ya Air Force One kwamba alifanya mazungumzo ya simu na Zelensky, akirudia kwamba "hakufurahishwa" na mazungumzo ya simu na Putin siku moja kabla, kutokana na kile alichokiita kukataa kwa kiongozi huyo wa Urusi kusitisha mapigano.

Alipoulizwa kama Marekani itakubali kusambaza makombora zaidi ya Patriot kwa Ukraine, kama alivyoombwa na Zelensky, Trump alisema: "Watayahitaji kwa ulinzi... Watahitaji kitu kwa sababu wanashambuliwa sana."

Trump alipongeza ufanisi wa makombora ya Patriot, akiita silaha hiyo "ya kipekee mno."

Alipoulizwa kuhusu matarajio ya kusitishwa kwa mapigano, Trump alisema, "Ni hali ngumu sana... Sikufurahishwa sana na mazungumzo yangu na Rais Putin. Anataka kwenda mbali zaidi, aendelee kuua watu tu - sio nzuri."

Zelensky alisema amekubali kuimarisha uwezo wa Kyiv wa "kulinda anga" wakati mashambulizi ya Urusi yanaongezeka, akiongeza katika ujumbe kwenye Telegram kwamba alijadili uzalishaji wa pamoja wa silaha za ulinzi, pamoja na ununuzi wa pamoja na uwekezaji na kiongozi wa Marekani.
mnataka kuipa michuma michuma yenu ukraine yangu,wapuuzi nyie USA
 
Hayo mapatriot hayakuwepo pale Tel Aviv?kumbe hata wazungu nao ni wajinga kiasi hicho?
 
Yani wanahitaji patriot kujilinda lakini siyo silaha za kupigana vita?
 
Wazungu wana sarakasi nyingi sana na mbwembwe nyingi sana,patriot,S-400 ,Thaad na Irone Dome yote ni mavyuma vyuma tu ya kuwapiga watu hela,suluhisho la hapo nchi kutafuta Amani hayo mavyuma yatakosa pa kwenda
 
Back
Top Bottom