Trump amuita Putin "kichaa" baada ya Urusi kurusha makombora 360 kwenda Ukraine siku ya Jumapili

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,439
Reaction score
6,692
Wakuu,

Mnakumbuka Trump alivyoingia madarakani alijinadi akisema kuwa anammudu Putin na kwamba akiingia tu madarakani ataimaliza hiyo vita "ON DAY ONE?"

Yaani it seems kabisa matarajio yake na alichokutana nacho ni tofauti kabisa. Naona sio Putin wala Zelensky wanayemsikiliza. Ni kama he was caught off guard!

=================================================

Rais wa Marekani Donald Trump amesema hafurahishiwi kabisa na Rais wa Urusi, Vladimir Putin, baada ya Urusi kufanya mashambulizi ya anga makubwa kabisa tangu vita hiyo ianze mwaka 2022

Katika mashambulizi hayo takribani watu 12 waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa Ukraine.

Urusi ilituma makombora na drones takriban 360 usiku wa Jumapili, makombora ambayo wachambuzi wamesema ni idadi kubwa zaidi ya makombora kuwahi kutumwa Ukraine katika usiku mmoja tangu vita hiyo ianze mwaka 2022

trump putin.png

Trump kufuatia shambulizi hilo la Urusi kwenda Ukraine amesema:

“Nimekuwa nikimfahamu Putin kwa muda mrefu na tumekuwa tukielewana, lakini sasa anatuma na kushambulia makombora kwenye miji ya Ukraine na na kuua watu. Putin anaonekana kama amepoteza mwelekeo. Anaua watu wengi sana.”

Kupitia ukurasa wake wa Truth Social, Trump alimtaja Putin kuwa “amepotea kabisa” na kuongeza kuwa Putin amekuwa kama kichaa

“Nimesema muda mrefu kuwa Putin anataka Ukraine yote, si kipande tu, na huenda nilikuwa sahihi lakini akiendelea kufanya hivyo, hiyo ndiyo itakuwa sababu ya kuanguka kwa Urusi!”

Trump pia alimkosoa kwa Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky akisema, “Zelensky haisaidii nchi yake kwa jinsi anavyozungumza. Kila anachosema kinazua matatizo. Sipendi kabisa, na inabidi aache mara moja,” aliandika Trump.

Wiki iliyopita, Trump na Putin walizungumza kwa njia ya simu kwa zaidi ya saa mbili kujadili pendekezo la Marekani la kusitisha mapigano. Trump alisema mazungumzo hayo “yalienda vizuri sana” na kwamba Urusi na Ukraine ziko tayari kuanza mazungumzo ya moja kwa moja ya kuelekea kusitisha vita.

Ukraine tayari imekubali kusitisha mapigano kwa siku 30, huku Putin akisema Urusi iko tayari kuandaa “hati ya makubaliano ya amani .” Hata hivyo, Kyiv na washirika wake wa Ulaya wameeleza hatua hiyo kama mbinu ya kuchelewesha mchakato.

=================================

US President Donald Trump has said he is "not happy" with his Russian counterpart Vladimir Putin, following Moscow's largest aerial attack yet on Ukraine.

In a rare rebuke, Trump said: "What the hell happened to him? He's killing a lot of people." He later called Putin "absolutely crazy".

Ukrainian President Volodymyr Zelensky earlier said Washington's "silence" over recent Russian attacks was encouraging Putin, urging "strong pressure" - including tougher sanctions - on Moscow.

At least 12 people were killed and dozens injured in Ukraine overnight Sunday after Russia fired 367 drones and missiles - the highest number in a single night since Putin launched a full-scale invasion in 2022.

Source: BBC, CNN
 
Trump alikuwa anajitoa akili tu, vita ya Russia na Ukraine niya kimkakati haiwezi kumalizwa kipumbavu kwa namna alivyokuwa anaelezea.

Wajinga tu, ndio wangeweza kumuamini Trump kwamba yeye ndio anauwezo wa kumaliza hii vita kwa muda mfupi.

Watu walikuwa wanamuona kama mwehu tu, ndiomaana walikuwa wanamuuliza kwamba unasema utamshauri Putin aache vita maramoja, akikataa utamfanya nini, akawa hana majibu anazugazuga tu.
 
Putin na Netanyau ni vichaa..
 
Hii ni Kama Ile habari ya,,"Kama hakuna mabadiliko hakuna uchaguzi,,😂Hatususii uchaguzi Bali hakutakua na uchaguzi".
Yaani mtu anaongea ugoro,alikua anaongea ugoro,Jambo haliwezekani lakini anaongea tu Ili kupata popularity ya mda mfupi..
 
Rais wa Marekani DJT ananasema kuna jambo limempata Putin na sasa amekuwa kichaa kabisa akifanya mauaji ya kutisha ya raia kiholela bila sababu ya kueleweka.

Macron wa Ufaransa anasema ni kama Trump ndio anazinduka na kushtuka alikuwa anachezeshwa shere na Putin.

20250527_085747.jpg
 
Mbona hashtushwi na mauaji anayofanya nentanyahu? Urusi inatumia zana nyingi na nzito ndani ya Ukraine yenye ukubwa mara mia kadhaa ya eneo la Gaza, huku Ukraine ikiwa na mamilioni ya watu ila wanakufa raia wachache sana tena mara mojamoja.
Israel inalipua raia waliokusanyika kaeneo kadogo kwa kisingizio cha kupambana na panyaroad ambao hawana hata kifaru wala ndege lakini unashangaa anaua mamia ya raia kila wiki.
Maajabu ni kuona Trump anatokwa machozi Urusi ikilipua maeneo ya kijeshi pale Ukraine lakini anachekelea Israel ikiwalenga raia na watoa msaada pale Gaza.

Upumbavu unazidi kuongezeka ulimwenguni
 
wagaza wanakufa kwa ujinga wao kuendelea kung'ang'ania raia wa Israel waliowafanya mateka na ujinga wa Hamas kuvaa kiraia kipindi cha vita na kujificha maeneo ya raia wa gaza
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom