Trump amteua jaji wa mahakama kuu Neil Gorsuch

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
_93899831_gorsuch2.jpg

Rais Donald Trump amemteua Neil Gorsuch kujaza nafasi katika mahakama kuu kwa mwaka mmoja. Bw Gorsuch mwenye umri wa miaka 49 ni jaji katika mahakama ya rufaa mjini Denver.

Jaji huyo hatarajiwi kutoa hukumu juu ya utoaji mimba na ndoa za wapenzi wa jinsi moja. Hata hivyo uteuzi wake unasubiri kuidhinishwa na bunge la Seneti.

Maseneta wa Democratic wametishia kumfungia nje mgombea yeyote atakayeonekana kuwa mhafidhina. Awali maseneta hao walipinga uteuzi wa watu watatu uliofanywa na rais kuchukua wadhifa wa waziri.

_93899834_gorsuch.jpg

Walisusia vikao vya kuwaidhinisha mawaziri wa fedha na afya waliopendekezwa na kuchelewesha upigaji kura wa kumuidhinisha Jeff Sessions aliyeteuliwa kuwa Mwanasheria mkuu.

Chanzo: BBC/Swahili
 
Hivi kwenye utawala wake watu weusi wangapi wameteuliwa kushika uwadhifa wa juu wa uongozi
 
Hivi kwenye utawala wake watu weusi wangapi wameteuliwa kushika uwadhifa wa juu wa uongozi
unaangalia ngozi au uwezo wa kazi
we umewaona weusi tu mbona hujawaulizia
warabu,wahindi na watu wengine kama hao

nyie ndio watu mnaaongozwa na media bila
kushirikisha ubongo wenu

wakati wa obama watu wangapi weusi wameuwawa marekani tena na mapolisi
na husikii blm(black lives matter) wakikoment chochote

nb : acheni nongwa mwacheni mtu aongoze
nchi awape watu maendeleo aliyohaidi
 
unaangalia ngozi au uwezo wa kazi
we umewaona weusi tu mbona hujawaulizia
warabu,wahindi na watu wengine kama hao

nyie ndio watu mnaaongozwa na media bila
kushirikisha ubongo wenu

wakati wa obama watu wangapi weusi wameuwawa marekani tena na mapolisi
na husikii blm(black lives matter) wakikoment chochote

nb : acheni nongwa mwacheni mtu aongoze
nchi awape watu maendeleo aliyohaidi
Sawaa mkuu
 
Trump ni kizazi cha zamani (70+) hivyo haya mambo ya ushoga sijui ndoa za jinsia moja kizazi hicho kinajiuliza ilikuwaje au inawezekanaje tofauti na kizazi cha Obuma ambao "kufirana" (ashakum si matusi) huko mashuleni ilikuwa jambo la kawaida hivyo hawaoni hata aibu kutetea huo upuuzi. Angalia pro-mashoga; wengi wao ni 50-.

Wazee wamezidiwa na vijana hivyo wanajifia na sononeko moyoni. Nakumbuka kauli aliyowahi kutoa The Queen (90+) ilionesha hisia alizokuwa nazo dhidi ya ushoga na hasa nchi yake kutumbukia kwenye hilo janga ila ndio hivyo afanyeje wakati siku zake ndio zimekwisha hivyo.
 
Back
Top Bottom