Trump ametishia kuiwekea vikwazo Iraq ikiwafukuza wanajeshi wa Marekani

Tripitaka

Senior Member
Nov 30, 2019
166
302
Rais Trump ametishia kufanya mashambulizi kadhaa dhidi ya Iraq baada ya bunge lake kutaka Marekani kuondoa majeshi yake nchini humo.

"Tumewekeza kiasi kikubwa sana cha fedha katika jeshi la anga huko. Kujenga msingi wake imetugharimu mabilioni ya dola. Hatutaondoka labda kama watatulipa gharama tuliyotumia", aliwaambia waandishi wa habarai.

Mvutano bado ni mkubwa baada ya Marekani kuusika kumuua kiongozi wa jeshi wa Marekani jenerali Qasem Soleimani huko Baghdad wiki iliyopita.

Iran iliapa kulipiza kisasi.
Soleimani ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka 62, alikuwa akiongoza operesheni za vita katika nchi za mashariki ya kati na alikuwa anatambuliwa na wamarekani kama gaidi.

Mabaki ya mwili wa jenerali sasa yamerejeshwa katika nchi yake Iran, eneo ambalo waombolezaji wamekusanyika barabarani katika mitaa ya Tehran.

Akizungumza akiwa katika ndege ya rais, Trump alisema kuwa kama Iraq inataka majeshi ya Mareani yaondoke nchini mwake kwa nguvu, "Tutalipiza kwa kufanya mashambulizi ambayo hayajawahi kutokea kabla . Na kufanya vikwazo ambavyo Iran imeviweka kuwa vya kawaida sana."

Wanajeshi wa Marekani wapatao 5,000 wapo Iraq kama sehemu ya makubaliano ya kimataifa ya kupambana na kundi la kigaidi la kiislamu 'Islamic State' (IS).

Siku ya jumapili, azimio lilifikiwa na wabunge wa Iraqi kuwa majeshi yote ya kigeni yaondoke nchini humo.

Source: BBC

Naona huko mashariki ya kati mambo bado ni moto.
 
Iran hamuwezi Marekani na Marekani katu hawezi kuondoa vikosi vyake nchini Iran hata kama hela waliyogharamia watarudishiwa kwani Marekani shida yao siyo pesa bali maslahi yao mapana ya kiusalama na kiuchumi ikizingatiwa Iran imejipambanua sana kivita

Sent from my SM-J700H using Tapatalk
 
Kwani US imeingiza vikosi vyake Iran lini?
Iran hamuwezi Marekani na Marekani katu hawezi kuondoa vikosi vyake nchini Iran hata kama hela waliyogharamia watarudishiwa kwani Marekani shida yao siyo pesa bali maslahi yao mapana ya kiusalama na kiuchumi ikizingatiwa Iran imejipambanua sana kivita

Sent from my SM-J700H using Tapatalk

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimekuta nyumba inayumba, nyufa kibao, vibaka wamejaa ndani, nawafukuza, nakujengea ujasiri wa kukabiliana nao, tunakubalina muda wa kukaa, anakuja jirani kunipiga kwako wakati mimi nimekufundisha ujasiri, namdunda leo unataka nitoke kwako? Basi utalipa ukarabati nilio ufanya pamoja na mkeo naondoka nae kwani muda wote nilikuwa natafuna
 
Hehe
Sasa hamtakiwi na wenye nchi lkn bado mnalazimisha muendelee tu kuwepo hahah,si mrudi kwenu aisee.

Wanajeshi wa Germany wao wamesema anytime Iraq ikitaka waondoke wao watasepa fasta tu na hata sasa wamesimamisha training program waliyokua nayo na jeshi la Iraq.

Sent using Jamii Forums mobile app
Waache 2 kama wanagoma kuondoka na washa ambiwa waache 2 niwazi kuna jambo wanalitafta na soon watalipata........

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni IRAQ MKUU
Iran hamuwezi Marekani na Marekani katu hawezi kuondoa vikosi vyake nchini Iran hata kama hela waliyogharamia watarudishiwa kwani Marekani shida yao siyo pesa bali maslahi yao mapana ya kiusalama na kiuchumi ikizingatiwa Iran imejipambanua sana kivita

Sent from my SM-J700H using Tapatalk
C IRAN

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimekuta nyumba inayumba, nyufa kibao, vibaka wamejaa ndani, nawafukuza, nakujengea ujasiri wa kukabiliana nao, tunakubalina muda wa kukaa, anakuja jirani kunipiga kwako wakati mimi nimekufundisha ujasiri, namdunda leo unataka nitoke kwako? Basi utalipa ukarabati nilio ufanya pamoja na mkeo naondoka nae kwani muda wote nilikuwa natafuna
Umeisummarize vizuri Sana Mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom