Trump aitishia Urusi kwa kutoza ushuru mkubwa kama hawatamaliza vita huku akiendelea na mpango wake wa kuwapa silaha wa Ukraine

Trump aitishia Urusi kwa kutoza ushuru mkubwa kama hawatamaliza vita huku akiendelea na mpango wake wa kuwapa silaha wa Ukraine

Ritz

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2011
Posts
54,015
Reaction score
43,157
Wanaukumbi

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kuwa Marekani itatuma "silaha za hali ya juu" kwa Ukraine kupitia nchi za Nato, huku pia akitishia Urusi kwa kutoza ushuru mkubwa ikiwa makubaliano ya kumaliza vita hayatafikiwa ndani ya siku 50.

"Tunataka kuhakikisha Ukraine inaweza kufanya kile inachotaka kufanya," Trump alisema kufuatia mkutano na mkuu wa Nato Mark Rutte mjini Washington.

Rutte alithibitisha kuwa Marekani imeamua "kuipatia Ukraine kwa wingi kile kinachohitajika kupitia Nato" na Ulaya wataidhinisha muswada huo.

Nchi za Ulaya zitaitumia Kyiv mifumo yao ya ulinzi ya anga ya Patriot - ambayo Ukraine inaitegemea kuzuwia mashambulizi mabaya ya anga ya Urusi - na mibadala itatolewa na Marekani, Trump alisema.
================
US President Donald Trump has announced the US will send "top-of-the-line weapons" to Ukraine via Nato countries, while also threatening Russia with severe tariffs if a deal to end the war is not reached within 50 days.
"We want to make sure Ukraine can do what it wants to do," Trump said following a meeting with Nato chief Mark Rutte in Washington.
Rutte confirmed the US had decided to "massively supply Ukraine with what is necessary through Nato" and that the Europeans would foot the bill.
European countries will send Kyiv their own Patriot air defence systems - which Ukraine relies on to repel Russia's deadly air strikes - and replacements will then be issued by the US, Trump said.
SOURCE: 👇🏽

 
Us siku hizi anabweka kipumbavu sana...Dunia ishabadilika yeye kakazana na maubabe yake ya kijinga.hizo ni hasira TU baada ya kushindwa kumshinikiza Putin kufikia makubaliano.
 
Aliacha kupeleka silaha ukraine ila kimemuuma,sana baada ya Urusi kuuteka mgodi mkubwa wa madini barani Ulaya ambao USA ilipewa na Ukraine baada ya kuingia mkataba wa kilaghai na hila.
 
Aliacha kupeleka silaha ukraine ila kimemuuma,sana baada ya Urusi kuuteka mgodi mkubwa wa madini barani Ulaya ambao USA ilipewa na Ukraine baada ya kuingia mkataba wa kilaghai na hila.
Kaguswa maslahi yake Sasa, ngoja tuone Kyiev ikiwa uwanja wa mapambamo
 
Trump siku ya Jumatatu alionyesha kusikitishwa na kukataa kwa Putin kukubaliana kusitisha mapigano na akatangaza wimbi la usambazaji wa silaha kwa Ukraine, ikiwa ni pamoja na mifumo ya makombora ya Patriot ya ardhi hadi angani. Pia alitishia kuiwekea Urusi vikwazo zaidi isipokuwa makubaliano ya amani yatafikiwa ndani ya siku 50.
Vyanzo hivyo vitatu vya Urusi, vinavyofahamu fikra za ngazi ya juu ya Kremlin, vilisema Putin hatasimamisha vita kwa shinikizo kutoka kwa nchi za Magharibi na anaamini Urusi - ambayo imenusurika vikwazo vikali vilivyowekwa na nchi za Magharibi- inaweza kustahimili matatizo zaidi ya kiuchumi, ikiwa ni pamoja na kutishiwa kwa ushuru wa Marekani unaolenga wanunuzi wa mafuta ya Kirusi.
 
Back
Top Bottom