Trump aitaka Marekani kuboresha silaha za nuklia

Sexer

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2014
Posts
8,521
Reaction score
8,286
Donald Trump ameitaka Marekani kuboresha zaidi uwezo wake wa zana za nuklia.

Rais huyo mteule ambaye ataingia ofisini mwezi ujao amesema kuwa Marakani ni lazima ichukue hatua kama hizo, hadi wakati ulimwengu utatathmini suala la nuklia.

Trump aliyazungumza hayo saa kaadha baada ya rais wa Urusi Vladimir Putin kusema kuwa Urusi inahitaji kuboresha uwezo wake silaha za nuklia
Marekania ina silaha 7,100 za nuklia huku Urusi ikiwa inamiliki silaha 7,300 kulingana na shirika la kudhibithi silaha la marekani.

Trump aliyaandika hayo kwenye akaunti yake ya mtando wa twitter
Wakati wa kampeni, Trump alisema kuwa silaha la nuklia ndilo tatizo kubwa zaidi linaloikumba dunia.

Mgombea wa chama cha Democratic Hillary Clinton mara kwa mara alimtaja Trump kuwa mtu asiye na uvumilivu wa kuweza kuzuia vita vya kinuklia.
 
Huwa najiuliza sana...ni kwanini Marekani inaona sawa kuwa na silaha za nyuklia na tena kuboresha

LAKINI haitaki kusikia Iran inamiliki silaha hizo?

Sio bure yule chalii wa Korea kaskazini na V. Putin wanakuwa wababe sana na wapo tayari kwa lolote.
 
Nahsi urafiki wa putin na trump utaishia hapo mana vita ya nchi hizi mbili ni umiliki wa silaha za nyuklia
.
.
.
Kyenekyaka mkighanile une
 
trump na putin ni marafiki?!
 
wakati mwingine ni bora tatizo ukaliacha kama lilivyo kwasababu unapo sema ulitatue lile ndio unazidi kuongeza mengine.

kama ni swala la kuto kumiliki nyukilia kwa marekani hawezi kuacha kumiliki.
ila cha msingi ni kwamba hayo hayo madini ya nyuklia wayaboleshe ili wawe na makombola machache kutoka 7100 hata wakija kuwa na makombola 1000. yanatosha sana.

unajua kuna vitu vingine zinakuwa kama sifa na hawana uhakika na wanacho fanya. makombola ya nyuklia 7100 yote yanini mbona ni mengi sana.
na wakati huo sheria za umoja wa mataifa mnapo kuwa vitani haitakiwi kutumia makombola za nyukilia.
 
Hapo ndiyo utajua Usa ni mnafiki yeye anaboresha zake halafu hataki wenzake wawe na hizo silaha kwanini?
 
Huwa najiuliza sana...ni kwanini Marekani inaona sawa kuwa na silaha za nyuklia na tena kuboresha

LAKINI haitaki kusikia Iran inamiliki silaha hizo?

Sio bure yule chalii wa Korea kaskazini na V. Putin wanakuwa wababe sana na wapo tayari kwa lolote.

Hivi majuzi Putin amekutana na makamanda wake wakajadili mikakati ya kuongezea nchi uwezo wa kijeshi, hivyo wewe baki hapo ukishangaa, wenzetu wanendelea kujihami.
 
hujawahi kujiuliza kwanii china na russia na wao walipiga kura kwe UNSC ya kuiwekea vikwazo iran kwa sababu ya shughuli zake za kinunklia?
 
Kuna mahali nimepinga suala la Russia kujihami?
 
hujawahi kujiuliza kwanii china na russia na wao walipiga kura kwe UNSC ya kuiwekea vikwazo iran kwa sababu ya shughuli zake za kinunklia?
Sijawahi kujiuliza, hebu niambie sababu ni ipi mkuu
 
wakati mwingine ni bora tatizo ukaliacha kama lilivyo kwasababu unapo sema ulitatue lile ndio unazidi kuongeza mengine.

kama ni swala la kuto kumiliki nyukilia kwa marekani hawezi kuacha kumiliki.
ila cha msingi ni kwamba hayo hayo madini ya nyuklia wayaboleshe ili wawe na makombola machache kutoka 7100 hata wakija kuwa na makombola 1000. yanatosha sana.

ukilia.
kuna preemptive attack kaka asa kama una warheads chache watu wanaanza kuziangamiza hizo kwanza kabla ya mambo mengine
 
Sijawahi kujiuliza, hebu niambie sababu ni ipi mkuu
aah sa hujui kwann unasemamarekan anazuia wenzake wakati hayo makatazo huwa yanatolewa na UNSC ambayo ina member wa 5 bro naukiyakiuka UNSC inakuwekea mavikwazo
 
Mataifa Makubwa kama USA, Russia, Ulaya Magharibi( Germany, UK, Spain, France, etc), China, Japan, India, Canada, Brazil, Argentina, Australia, haya yanaaminika kuwa hata yakiwa na Nyuklia, dunia itabaki Salama maana, 1. Yamestarabika, 2. Hayaendeshwi kwa visasi, 3. Kuwa na nyuklia kwao kuna balance power ya ulimwengu kuepusha vita vingine vya ovyo. Lakini mataifa yale ya kizazi cha Ishmael hayaluhusiwi, kwa kuwa wao wapo duniani kwa ajiri ya visasi na kuchinja!.
 
Mkuu ustaarabu unapimwaje?
 
Back
Top Bottom