True Story

Mlachake

JF-Expert Member
Oct 13, 2009
4,412
4,559
Kila Jumatatu saa tatu Usiku Redio Maria Inarusha Kipindi Kiitwacho Wanamaridhiano.
Kipindi cha jana kilikua ni marudio ya Jumatatu iliyopita.

Now comes the story.
Kuna dada mmoja ambaye ni Mhasibu katika shirika moja hapa Tanzania.
Alufunga ndoa na bwana mmoja pale Chuo kikuu cha Dar es salaam miaka minne iliyopita. Katika kanisa la KKT.(huwa pale dini zote za kikristu hutumia Jengo moja)

Kuna kipindi huyu dada alimwambia mme wake kuwa amepata contract job Arusha. Kwa upendo mume wake huyu alichukua gari na kumsindikiza mwenzi wake Arusha mpaka hotel aliyofikia.

Kwasababu mume wake hakuhitaji kwenda iliko ofisi mpya ya mkewe ilimbidi Kesho yake
arudi Dar es salaam kuendelea na majukumu yake. Huyu mwanamama alikua anaka mpaka miezi sita na zaidi bila kuonana na huyu mumuwe.

Kila mume wake alipotaka kwenda kumtembelea Arusha huyu mama alitoa vijisababu.
Oh! ''Huwa nabanwa sana na kazi so natoka usiku sana haina haja wewe uje, wacha
nitafute muda wa kujiiba nije mimi Dar''

Storry zikawa ndio hivyo.
Wiki mbili zilizopita, Huyu dada amefariki dunia akiwa katika harakati za kujifungua. Huyu mume wake alipo pata taarifa aliamua kufunga safari mpaka Arusha.
Cha ajabu alikuta huyu mwanamama an mume mwingine wa ndoa, na yule mwnao wa kwanza
jina la baba na la huyu mume wa pili.
Tafrani ilitokea kwa nani ni mume halali wa kuuzika mwili!!
hadi sasa bado huu mwili haujazikwa.

my dear ladies, please be careful jamani
 
He!

Halafu mnasema tusiwanyemelee kwa nyuma............................abiria chunga mzigo wako!:becky:
 
Ila huyu jamaa naye alikuwa bushoke... Yani mkewe ana mimba hadi anajifungua hujui?
 
Ila huyu jamaa naye alikuwa bushoke... Yani mkewe ana mimba hadi anajifungua hujui?


Tema mate chini mkuu...........................unaweza usijue ..............why not! Hujasikia mambo ya matambara nini weye!?:eyeroll2:
 
Paukwa pakawa.

It may be.
Lakini ningeomba upate kamuda kidogo uwe unasikiliza hii programme on mondays.
Labda the way mimi nimeipresent ndio inaonekana paukwa pakawa. but this is a true story my friend
 
hadithi. hadithi? Hadithi njoo...! Umempeleka mkeo kwa gari hadi Arusha. Unajua hotel aliyofikia halafu unakubali Miezi SITA mizima akukatalie kwenda kumsalimia eti kwa vile ana kazi nyingi na anarudi usiku!!! SO WHAAT! Rudi Usiku na utanikuta nimeishakuja kutoka Dar na ninakusubiri Reception ya Hoteli...Unless na wewe Huku Dar ulikuwa na yako na unafurahi anapokuambia usimfuate Arusha!:eyeroll2:
 
Inasikitisha sana tena inauma sana. kwanza tuwape pole wenzetu walio fiwa na mpenwa wao. maoni yangu nawashauri wakubaliane na wasaidiane kumzika mwenzao.


Baada ya hayo..!! haya matukio ni mengi hasa kwa wanaume. wana watoto na wake kila wanako kwenda.

ila huyo aliye kufa,,,sijuih,,,. atajua yeye na Mungu! labda hiyo ndiyo safari ya kuelekea hukumu yake.

Nanyi ndugu zangu jihadharini na kuwa mbali na wapendwa wenu.

mwenzio akinyolewa wewe suka rasta! au twende kilioni.!!!!!
 
story inaweza kuwa ya kweli ila huyo mume orijino nae ni Bushoke iweje mkeo akae sehemu kuanzia mimba mpka anajifungua wewe hujaonana nae kuna umbali gani hapo Arusha tu.... na kingine ina maana hamna hata mtu mmoja unayemjua hapo Arusha ukamtuma amtafute ili akupe taarifa mmm kizunguzungu tupu ngoja niishie hapo
 
story inaweza kuwa ya kweli ila huyo mume orijino nae ni Bushoke iweje mkeo akae sehemu kuanzia mimba mpka anajifungua wewe hujaonana nae kuna umbali gani hapo Arusha tu.... na kingine ina maana hamna hata mtu mmoja unayemjua hapo Arusha ukamtuma amtafute ili akupe taarifa mmm kizunguzungu tupu ngoja niishie hapo

Yawezekana huyo mume naye aliona ndo chance yakujirusha akaona bora aendelee na kazi huko AR asimsumbue na ndivyo ilikuwa!!
 
Chini ya jua kila kitu kinawezekana ila huyu mwanamama alikuwa mafia wa ukweli:confused2:
 
Yawezekana huyo mume naye aliona ndo chance yakujirusha akaona bora aendelee na kazi huko AR asimsumbue na ndivyo ilikuwa!!
matokeo yake imekula kwake. Halafu mwisho wa siku wanagombea kumzika marehemu ningekuwa mm ningempotezea tu ningeshiriki mazishi kama mtu baki
 
Aisee, ila huyu mwenzetu alizidi, yaani anaomba ruhusa kumtembelea mkewe? Si ukimkumbuka unapamba basi unafikia na kulala anakolala!! Si ndio ubavu wangu? Popote pamoja.
 
Haya ndo ya dunia. lakini mwanamume alitakiwa ajue wapi mkewe anakaa, hata kama huyu mke alikuwa akibanwa ofisini sana. hata kupitisha wikendi kidogo. kweli alikuwa Bushoke. lakini haya wnaume pia huyafanya huwa na ndoa mbili bila wakeze kujua.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom