True story: Ushuhuda wa ndoa yangu


AHIMIDIWE MUNGU MUUMBA WA MBINGU NA NCHI, KWAKE HAKUNA LINALOSHINDIKANA
 
Ubarikiwe sana hakika Mungu yupo,kwa ushuhuda huu hakika Mungu ataendelea kukubariki zaidi ya sasa
 
Asanteni sana kwa kushiriki nami kumshukuru na Kumtukuza Mungu. Ee Mungu wangu, bila wewe mimi ningekuwa mgeni wa nani?wanadamu hawaaminiki, mashetani nayo ni roho za machukizo, ni wewe tu Bwana Unastahili sifa na Kuabudiwa, ni wewe tu una nguvu, ni wewe tu unaponya, ni wewe tu unafungua vifungo, ni wewe tu Uliumba Mbingu na nchi na vyote vilivyomo, upendo wako ni mkuu sana, uwezo wako ni mkuu sana, nguvu zako hazipimiki, wewe ni Alfa na Omega, Mwanzo na mwisho, aliyekuwepo aliyepo na atakayekuwepo milele. Nakuabudu Mungu wangu, nakupa sifa Mungu wangu, nakutukuza Mungu wangu, naliinua Jina lako eee Mungu wangu, bila wewe mimi ningekuwa wapi, bila wewe wanadamu wangenionea, bila wewe mashetani wangenionea, bila wewe nani angeniponya, wewe uliumba mbingu na nchi, vyote vimefanyika kwa mkono wako ee Mungu, ni nani aliyejuu yako? ni nani atashindana na wewe, wewe ukisema ndiyo hakuna wa kusema hapana, wewe ukisema hapana hakuna wa kusema ndiyo, wewe ukiokoa hakuna wa kuua, wewe huhuisha nafsi roho na mwili wake yeye uliyeamua kumuokoa.

...Umeahidi kila alitajaye Jina lako ataokoka, umesema yeyote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe....Naja Kwako Eee Mungu wangu kama nilivyo, mimi ni mwanadamu mwenye madhaifu mengi, umenitendea makuu mno, nisaidie nisikusahau wewe, nisaidie kuushinda ulimwengu huu, nisaidia kuishinda dhambi, nisaidie niwepo nyumbani mwako ee Mungu....Unastahili sifa Mungu wangu, hakuna Mungu aliye kama wewe, hajawahi kuwepo na hatakuja kuwepo aliye kama wewe. Unastahili sifa milele na milele, kwani wewe watawala milele yooote.

Unatenda mambo makubwa na ya ajabu ee Mungu, wewe unaponya magonjwa yetu, wewe unafufua wafu, wewe unaokoa, nilifungwa minyororo ya dhambi na minyororo ya adui, Mkono wako umeikata minyororo yote na kuniweka huru, wewe ni yeye yule jana leo na hata milele,

ulifanyika mwili ukakaa kwetu nasi tunauona utukufu wako, Damu ya Yesu msalabani imenisafisha na kufuta laana na mikosi yote, akafanyika laana ili mimi nisilaaniwe, akafanyika aibu ili mimi iondolewe aibu, hakika ameyachukua madhaifu yetu yote, amejitwika huzuni zetu zote, alijeruhiwa kwa makosa yetu, alichubuliwa kwa maovu yetu, adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake na kwa kupigwa kwake sisi tumepona....hakika kwa kupigwa kwake mimi na mke wangu tumepona utasa, na kwa Jina la Yesu, yeyote anayesoma kurasa hii akiamini kwa Jina hili kama hajapata mtoto ATAPATA HAKIKA. Asante Mungu wangu, ASante.
 
Ashante ndugu kwa ushuhuda
 
Ahsante ndugu kwa ushuhuda wa kututia moyo
 
Mungu ni mwaminifu siku zote.
Ubarikiwe sana kwa ku-share nasi
 
Mungu ni muaminifu sana nilichelewa pia kupata mtoto ingawa sikufunga ndoa ila sikuitaman kabisa ilo janga lisikie kwa mwingne.jmn namshkuru Mung mwaka Jana umekuwa mwaka wa baraka kwang mungu kanijalia mtot wa kiume
Mwache Mungu aitwe Mungu
 
Mwenyezi Mungu ana huruma sana...

Mi kulikuwa na vitu namuomba hadi nikawa nishajikatia tamaa, siku ameniinua hata sikuamini!

Namuabudu Mungu wangu hata mwisho wa pumzi yangu! Ee Mwenyezi Mungu nisaidie
 
Duh ebwanae hii Kali, Hongera sana. Hakika imani yako imekuponya
ni neema tu ndugu, wakati mwingine hata unapitia maumivu hadi unakuwa sugu na imani inakuwa sio sababu tena bali ni neema tu, wala siwezi kujisifu kwamba nilikuwa na imani sana, ni kwamba nilikuwa frustrated kama panya aliyenaswa kwenye mtego na na haoni mbele wala nyuma ila maumivu tu....mara ikatokea msamaria akafungua mtego na kumtoa akaondoka zake salama. Ndivyo Mungu alivyofanya kwangu, sikustahili, ndio maana mwingine alisema ...."Bwana naamini lakini nisaidie kutokuamini kwangu...." akiwa na maana kwamba hata kama una imani lakini wakati mwingine unaweza kuwa na mapungufu ya imani, ukawa na wasiwasi na Mungu kwa neema yake akakuponya hivyohivyo bure kabisa. siwezi kujiita gwiji la imani, siko miongoni mwa hao, mimi ni mdhaifu tu ninayehitaji kukamilishwa na Mungu siku baada ya siku.
 
Kati ya vitu vyote ulivyoongea hapa umeongea jambo la maana sana!

Imani mda mwingine inapotea kabisa!

Mda mwingine unaeza hisi Mwenyezi Mungu hasikilizi unachomuomba!

Usiombe uwe desperate hakuna rangi unaacha ona!

Hii hali ishanikuta sana lakini nilivyochopolewa mpaka sasa hivi siamini kabisa

Mkuu ubarikiwe kwa kushare..
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…