True story: Ushuhuda wa ndoa yangu

Hakika Mungu anaweza!
Mungu nifanyie wepesi kwa haya ninayopitia.......
 
mhhh, nitakujibu maswali yote ndugu. Kipindi hicho tumeoana, wote tulikuwa tumemaliza shule ila mimi nilikuwa nimetangulia kwake mda mrefu, sikutafuta kazi niliingia kwenye deals zangu binafsi na nilipata hela nyingi ktk umri mdogo, mimi ndiye nilikuwa na pesa, mke wangu alikuwa jobless, siku majanga yametupata, mimi niliyekuwa tegemeo nikafilisika, nuksi au jaribu hili lilitupata wote, kuna mengi sijaandika juu ya Mke wangu, hapangetosha hapa. hivyo, sote ni kama milango ilifungwa, hakuna chochote utakachofanya kikafanikiwa, na mwanamke alivyokuwa frustrated, mda wote hasira na kulia machozi, ndio hata kwenye interview wakawa wanamkimbiza tu. ndugu nyota yako au mlango wako ukifungwa au ukinajisiwa, pasipo kusafishwa na Mungu utazunguka dunia yote hadi nnzi watakukimbia...usiombe yakukute.

2. sitataja fani aliyosoma. ila profession aliyoisoma, ilihitaji cheti cha professionalism ili awe consultant. milango ilipofunguka, kila kitu tunachokifanya kinafanikiwa, hata mke wangu kwasasa, aliamua asiajiriwe kabisa, kuna biashara zetu anaziendesha na yeye kama consultant na professiona......, na suala kwamba tumekula mihogo ya 200, ni kutu halisi, hauwezi kuamini kama kilitokea hadi kikukute, au kama kuna mtu yalishamkuta maisha kama hayo. siwezi kubisha, nilipokuwa na hela nilikuwa na kiburi, hata mke wangu pia, wakati mwingine huwa naamini Mungu aliamua kukishusha kiburi chetu kwa kufunga milango yote ili tumtafute, wakati mwingine kuna dalili na watu walishawahi kuconfess kwamba walituchezea, yote namwachia Mungu,ninachojua mimi ni kwamba nimepota na ninamshukuru Mungu kwa hilo.

3. mke wangu naye hakuwa anafanya kazi mkuu. nafikiri hilo nimeshajibu. ni ile mtu unaoa mtu anayemaliza shule hajapata kazi, anakutegemea wewe, akiwa kwako atatafuta kazi atapata, halafu tegemeo anadondoshwa hadi chini, na anayetegemea naye ndio anadondoka naye, milango imefungwa yote kwa wote wawili, na stress na frustration ikiwakuta kabla hamjatengeneza maisha, au hamjapata kazi,...ni hatari sana.

the whole of this story imejikita kwenye kipengele kimoja tu. no matter umetajirika namna gani, haijalishi una elimu ya namna gani, kama hakuna kibali cha kutoka, kama milango yako imefungwa either na Mungu au na shetani, isipofunguka utazunguka dunia yote na hautafanikiwa. ukikipata chanzo cha tatizo, kikatatuliwa, either spiritually au kwa kawaida tu, everything kinabadilika. nawahakikishia maisha haya nimeyaishi. wengi hapa mnaweza kusema kwasababu tulikuwa na elimu pengine tulizembea, ndugu yangu, usitegemee hiyo elimu, bila kibali cha Mungu utajitaabisha bure. vilevile, amini usiamini kuna nuksi hapa duniani ambayo mtu akikumwagia bila msaada wa Mungu haufunguki. hata mimi nilitegemea elimu hivyohivyo, nilitegemea ndugu, nilikuwa na viwanja nikauza nikasema ngoja nifanye hiki ngoja nifanje kile, mlango ukifungwa ndugu chochote utakachofanya kitaishia hewa wala hautaelewa. haya mambo ni spiritual, whether kwa Mungu au kwa shetani.
 
Mungu anaweza zaidi ya haya ulioandika hapa mkuu ila punguza drama na simulizi zako.
hahaha, drama...inawezekana sijui kuandika mkuu. ni kweli anaweza zaidi ya haya niliyoandika. kuna watu hapa wanaamini napiga promo kanisa langu, labda mimi ni mchungaji....kwa kifupi mimi ni mwanasheria. uliza lolote la kisheria unidadiso vyovyte vile ndio utajua kama mi ni raia wa kawaida tu na haya yamenitokea maishani mwangu. sifa na utukufu kwa Mungu, mwenye kunielewa atakua amenielewa. Mbarikiwe sana.
 
Pole sana kwa mitihani uliyopitia. Matatizo ya hapa duniani yanaweza kukujenga au kukumaliza. Wewe ulichagua fungu jema. Na Mungu akafanya yake kwa wakati wake. Ila nikupongeze tu kwa ujasiri na mapenzi makubwa kwa shemeji yetu. Njia mliopitia si ndoa nyingi zinaweza ku survive. Utukufu una wewe Bwana.
 
A
Ameen atatenda tuu mpendwa
 
NimekuPM naomba usomapo ujumbe wangu usiache kunijibu
 
Mh watu wana roho mbaya, yan cku hiz mtu ukipata hela nyingi, ndugu wanakua karib zaid na ww kinafki wakijifanya eti wanakupenda sana. AZUSA STREET
 
'Awesome narration;
 
Read Responsibly!!!! mm ilikuwa kidogo tu niingie mkenge nilipokuja kushituka kumbe huwa wanaandaa hata waumin washuhudie uongo kuwahadaa waumin....ila nasema huyu wanayemzushiia atawahukumu kadiri wanavyostahiri
 
Kama kuna changamoto kwa mwanamke aliyeolewa ni kukosa mtoto....

Utadharauliwa hata na vitoto....
 
Nakuelewa sana AZUSA, na waliokufanyia hayo mabaya ni watu wako wa karibu mno. Watu wabaya jamani, hivi ukimfungia mwenzio riziki yake wewe ndo unapata? Nimepitia kama haya ila Mungu huwa anawaacha vinywa wazi maadui zangu. Wakifunga Mungu hufungua.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…