Si unaona hapo, nna uhakika huyo Mzee Karama , hapo Saudia alikuwa si kwao, nae alikuwa ni muhamiaji haramu.
Msaudi hususan mwenye asli ya Jiddah, hawezi kabisa kuhangaika, wao wana "system" ya "Umdah" ambae huyo mzee angekuwa ana asili ya hapo, lazima angemjuwa Umda wake na huyo Umdah asingekubali kabisa apate taabu.
Kati ya Watanzania nnao wajua wenye asili ya Jiddah ni kina Jidawi (wa Zanzibari), hawa ni ukoo maarufu sana Zanzibar na hakuna asiyewajua, ingawa wamechanganya damu "nadhani na wangazija" na watoto wengine wameolewa na kuoa makabila tofauti, lakini asili yao ni watu wa Jiddah na ndio maana wanaitwa "Jidawi". Hawa hata waende leo Ubalozini wakaoneshe roots za na family tree, basi watafanyiwa kila kitu chao kiwe sahali na watapokelewa kwa mikono miwili.
Nna uhakika Mzee Karama alikuwa ni illegal immigrant hapo Jeddah, Saudi Arabia.
Kama bado wapo Saudia na wanahitaji msaada wowote hapo, tafadhali ni PM ntakujulisha wafanye nini na waonane na nani.