True Story: Jestina

True Story: Jestina

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,433
Jestina ni binti wa miaka 28, alisoma na kumaliza masomo yake vizuri.na anakazi ajira ya serikalini. Katika hangaika za maisha alishakuwa na mahusiano na vijana kama wanne katika muda tofauti. Jestina alikutana na Kichuguu, Jestina alijua kuwa Kichuguu alikuwa na mpenzi mwingine kabla yake, lakini Kichuguu alimhakikishia Jestina kabisa kuwa ameachana na aliyekuwa mpenzi wake na alitaka kuanzisha maisha mapya na Jestina.

Kichuguu ni kijana mpenda starehe sana, na wengi waligundua kuwa kuwa na Jestina alikuwa anatafuta mahali kwenye maisha yaliyotulia. Jestina alishaona umri unakwenda, alifikiria kupata mtoto na Kichuguu kungemfanya atulie. Maisha yaliendelea lakini baada ya hapo Kichuguu aliimwacha Jestina na kuhamia mkoa mwingine.

Jestina ni binti aliyetulia sana, baada ya Kichuguu kuondoka aliiendelea na maisha yake, juzi tu Jestina amekutana na mwanaume umri wa miaka 32, mwanaume huyu hajaoa. Walianza mapenzi, Jestina alimwambia yule mwanaume hataki tena mwanaume wa kuchezea mwili wake na kumwacha, kama anampenda amsubiri kwanza wasikimbilie kufanya mapenzi mpaka Jestina atakapokuwa tayari.

Jestina alipata homa kali sana akiwa ofisni, alipelekwa hospitali, vipimo vya malaria vilitoka negative, lakini alikuwa anatapika na mwili ukiwa na joto kali. Alishauriwa kupima HIV na yeye alikubali, majibu yamerudi +ve. Kichuguu alimwambukiza Jestina HIV wakati wapo pamoja. Jestina aliumia sana, alirudi nyumbani na kuanza kutafakari, aliamua kufuata ushauri nasaha. Kumbumbuka mchumba mpya bado anahudumia, lakini Jestina alishidwa kabisa kumweleza yanayomsibu. Baada mwaka, mchumba alimwambia Jestina anataka kuwa na mke na familia akifikisha miaka 35, hivyo anataka kuanza mipango ya engagement. Jestina alimweleza status yake. Mchumba alisikiliza na kumwambia, kwanini ulinificha muda wote huo? Alijibu kuwa hata mwenywe alikuwa anatafakari, mchumba alimwambia usiwe na wasiwasi, kwa Mungu hakuna kisichowezekana. Baada ya hapo hajapiga simu tena na Jestina akipiga haipokelewi.

Majina ni fiction tu ingawa story ni ya kweli.
 
Hahahh nacheka kama mazuri mchumba kaniacha hoi ila jestina pole anza dozi kupata hiv sio mwisho wa maisha
 
et kwa mungu hakuna kisichowezekana kumbe ndio ilikua bye bye.... kichuguu mtu mbaya sana aisee.
 
Ninampongeza Jestina kuwa mkweli, asingekaa kwa amani na siri kubwa hii. Imagine mume anakuja kujua baadae.
 
Ninampongeza Jestina kuwa mkweli, asingekaa kwa amani na siri kubwa hii. Imagine mume anakuja kujua baadae.
inaonekana jestina ana hulka ya upole na tabia njema ndio maana yalipomkuta aliamua kubaki nayo mwenyewe nampongeza kwa hilo.
 
...sawa ila huyo kichuguu mbona mimi hivi
 
Pole sana Jestina
Hakuna kitu kizuri kama kujali afya ya mtu mwingine. Zingatia dozi, kuugua sio kufa
 
Bora huyu kawa muwazi

Kuna huyo dada kabla ya harusi aligundua Ana HIV akaogopa kumwambia kwakuhofia kuachwa

akaolewa hivyo hivyo.alimweleza akiwa ndani ya ndoa

mwanaume ndo akaenda kupima akaakutwa hana hata doctors hawakuamin damu ikapelekwa hadi Dar kurudia vipimo Hana mke anao

hadi Leo wanaishi mke anao na mume Hana na hawatumii kinga

kweli kwa MUNGU hakuna linalo shindikana
 
Back
Top Bottom