Trip to Bagamoyo

Bensoy

JF-Expert Member
Dec 21, 2016
577
618
BAGAMOYO TOURS
TAA TANZANIA ni taasisi isiyo ya kiserekali lilosajiliwa mwaka 2008 kwa no. 15995. Inakutangazia kuwa.

Kutakuwa na trip ya kwenda bagamoyo siku ya jumamosi sikukuu ya 8*8 tarehe 8/8/2020 kutalii maeneo mbali mbali ya makumbusho ya Taifa na kutazama burudani ya ngoma asilia katika chuo cha sanaa bagamoyo KAOLE na maeneo wanayofuga nyoka, mamba na viumbe vingine vingi tu.

Gharama ya kwenda kuzunguka maeneo yote na kurudi pamoja na maji ni Tsh 15,000/-.

Usafiri ni coaster ya kisasa yenye AC, TV, FRIDGE na SEAT adjustable yenye abiria 28 tu.
Kwa wale wakristo na haswa wakatoliki watapata nafasi ya kutembelea eneo la msalabani. Kutakua na utulivu na maombi binafsi. Utapata nafasi ya kuona majengo ya mahekalu ya wamisionary wa kwanza Tanzania mfano Mr Rebman na Dr Livingstone oamoja na wengineo.
Kwa wenzetu wa imani ya kiislam pia watakuwa na nafasi ya kuzuru kwenye majengo ya misikiti inayoaminika kuwa ya mwanzo kabisa eneo hili la mashariki ya africa.
Tutaona kisima kinachoaminiwa kina maajabu ambapo maji yake hayapungui wala kuongezeka tangu enzi.

Fanya booking ya jina lako inbox then malipo yatafanyika siku 3 kabla ya safari kuwezesha wenye shift kujua ratiba zao.

Badilisha mazingira, refresh ubongo wako na UTALII wa nyumbani
Booking 0719794789/0719794789
 
Back
Top Bottom