mathcom
JF-Expert Member
- Oct 13, 2012
- 1,396
- 518
Hata yakipaki, CCTV ni masaa 24 yenyewe haipaki.. CCTV ni lazima,,sio swali.
Wataiba hiyo CCTV kwanza!!
Hata yakipaki, CCTV ni masaa 24 yenyewe haipaki.. CCTV ni lazima,,sio swali.
Dah ushafika huko mara hii
UZINDUZI wa safari za treni ya abiria jijini la Dar es Salaam, nusura uingie dosari jana wakati kibaka aliyetambuliwa kwa jina la Vincent Michael alipoamua kuiba vyuma vya breki katika moja ya mabehewa yaliyoegeshwa katika kituo cha Yombo.
Tukio hilo lilifanyika muda mfupi kabla ya treni iliyombeba Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe haijafika katika kituo hicho.
Msafara wa Dk. Mwakyembe aliyeambatana na waandishi wa habari pamoja na maofisa wa Sumatra na wale wa Shirika la usafirishaji la Tanzania na Zambia (TAZARA), ulikuwa unarejea stesheni ya Dar es Salaam, ukitokea katika kituo cha Mwakanga nje ya jiji.
Safari hiyo ilikuwa ni baada ya Waziri Mwakyembe kuzindua usafiri wa aina hiyo kwa treni ya Shirikla la Reli nchini (TRL), uliofanyika eneo la Ubungo Maziwa.
Mmoja wa maofisa wanaolinda katika eneo hilo la Yombo, aliyeomba jina lake lihifadhiwe kwa kuwa si msemaji, alisema kuwa walimkamata kibaka huyo wakati akitekeleza uhalifu wake pasipo kuhofia athari zitakazojitokeza endapo behewa hilo lingeanza kufanya safari zake.
Kufuatia tukio hilo kibaka huyo alibebwa katika moja ya mabehewa yaliyombeba Waziri Mwakyembe na kisha kufikishwa katika Kituo cha Polisi Tazara kwa hatua zaidi.
ngoja nim googleVincent Michael

Huyoo atakuwa chadema tu.
vincent michael kwa nini wewe hujasoma kama wenzako waliomo humu ndani wanaojisifia jamii yao wanaakili kuliko jamii nyingine
Maisha yakikosa matumaini watu hupoteza hamu ya kuishi na hili likitokea inakuwa liwalo na liwe (Pinda) jamii ikifikia hapo ambapo watanzania wengi wa kawaida tumefikia hufanya watu kujivunia kufanya mambo mabaya kwa hisia za kuwaharibia wale ambao inaaminika kwamba wao ndio wanaofaidi utulivu wa maisha ya taifa hili.kama huwapi elimu watu ,tegemea uchawi,mazingaombwe, udokozi n.k