Treni yaanza kwa hujuma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Treni yaanza kwa hujuma

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mgomba101, Oct 30, 2012.

 1. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  UZINDUZI wa safari za treni ya abiria jijini la Dar es Salaam, nusura uingie dosari jana wakati kibaka aliyetambuliwa kwa jina la Vincent Michael alipoamua kuiba vyuma vya breki katika moja ya mabehewa yaliyoegeshwa katika kituo cha Yombo.

  Tukio hilo lilifanyika muda mfupi kabla ya treni iliyombeba Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe haijafika katika kituo hicho.

  Msafara wa Dk. Mwakyembe aliyeambatana na waandishi wa habari pamoja na maofisa wa Sumatra na wale wa Shirika la usafirishaji la Tanzania na Zambia (TAZARA), ulikuwa unarejea stesheni ya Dar es Salaam, ukitokea katika kituo cha Mwakanga nje ya jiji.

  Safari hiyo ilikuwa ni baada ya Waziri Mwakyembe kuzindua usafiri wa aina hiyo kwa treni ya Shirikla la Reli nchini (TRL), uliofanyika eneo la Ubungo Maziwa.

  Mmoja wa maofisa wanaolinda katika eneo hilo la Yombo, aliyeomba jina lake lihifadhiwe kwa kuwa si msemaji, alisema kuwa walimkamata kibaka huyo wakati akitekeleza uhalifu wake pasipo kuhofia athari zitakazojitokeza endapo behewa hilo lingeanza kufanya safari zake.

  Kufuatia tukio hilo kibaka huyo alibebwa katika moja ya mabehewa yaliyombeba Waziri Mwakyembe na kisha kufikishwa katika Kituo cha Polisi Tazara kwa hatua zaidi.
   
 2. 124 Ali

  124 Ali JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2012
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 5,709
  Likes Received: 2,394
  Trophy Points: 280
  OOHOO!vp tena vifisai vidunchu,mara hii?
   
 3. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Hayo ndiyo matunda ya Serikali mbovu inayoongoza watu maskini waliokidhiri.
   
 4. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Watanzania wote tuwe walinzi wa treni yetu najua wapo watu wanamuonea gere mwakyembe kwa uthubutu wake.
  Pia nawaomba EL,RA na AC waje wapande hii treni yetu.
   
 5. sun wu

  sun wu JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 0
  dawa ni kuinvest kwenye CCTV kwenye kila behewa lakini hii pia haitamaliza wizi sababu wezi wakubwa ni wafanyakazi na wataiba wakati mabehewa yamepaki
   
 6. Simple

  Simple JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2012
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 249
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hata yakipaki, CCTV ni masaa 24 yenyewe haipaki.. CCTV ni lazima,,sio swali.
   
 7. R

  Rwey Senior Member

  #7
  Oct 30, 2012
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 103
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Dah huu umaskini wetu matatizo... umaskini wa akili unatufanya tusifikilie maendeleo,, na umaskini wa fedha ndoo kabisaaa unaongeza tatizo.
   
 8. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #8
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Vincent michael kwa nini wewe hujasoma kama wenzako waliomo humu ndani wanaojisifia jamii yao wanaakili kuliko jamii nyingine
   
 9. K

  Kidzude JF-Expert Member

  #9
  Oct 30, 2012
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  for sure CCTV na Simu ni muhimu pia spika for announcement in train.
   
 10. m

  malaka JF-Expert Member

  #10
  Oct 30, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,323
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Watapata hasara mara mbili kaka. Wabongo wataiba hadi hizo kamera aisee.
   
 11. t

  tupel Member

  #11
  Oct 30, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Dah ushafika huko mara hii
   
 12. m

  motherservant Member

  #12
  Oct 30, 2012
  Joined: Jul 19, 2012
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Kwanza kabisa ni vizuri kila mmoja wetu akaelewa tunawajibika kwa utunzaji wa mali zetu. Hizi ni jitihada tu za wachache wasiopenda kuona wenzao wakifanya vizuri lakini pia jamii ieleweshwe kila mara inapopatikana nafasi juu ya umuhimu wa kujiona wamiliki wa mali za umma. Umaskini ni jambo lingine pia uangaliwe uwezekano wa kuwasaidia vijana wetu hasa kwa elimu na kujitambua maana si kweli kwamba vibaka wote hawana uwezo wa kufanya kazi au wale wanaoomb mchana kutwa si kweli kwamba wote wana matatizo ni kutokujitambua na uvivu ambao umeendekezwa na jamii pamoja na serikali yetu. Kila anayepata nafasi ya kutoa elimu popote afanye hivyo. Ukimpa mtu shilingi 500 tuseme haitamsaidia sana kuliko angeelimishwa akajua kujitafutia hata zaidi ya hapo. Tusibaki kulaumu serikali kila wakati nasi tutumie nafasi zetu
   
 13. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #13
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Chadema wakichukuwa nchi itawaongoza matajiri.
   
 14. ram

  ram JF-Expert Member

  #14
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 6,224
  Likes Received: 918
  Trophy Points: 280
  Chezea wabongo weye!!

   
 15. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #15
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. SIERA

  SIERA JF-Expert Member

  #16
  Oct 30, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,232
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Wezi mpaka USA wapo....wizi nitabia mbaya tu alonayo mwanadamu ..wangapi wezi unawajua na wametoka family bora...think before u talk
   
 17. SIERA

  SIERA JF-Expert Member

  #17
  Oct 30, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,232
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Daah itabidi Vincent wamchangie akasome maana hii jamii wote wamesoma..
   
 18. P

  Ponera JF-Expert Member

  #18
  Oct 30, 2012
  Joined: Dec 3, 2011
  Messages: 556
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mkuu nimekugongea bonge la like, chukua jingine "LIKE" angekuwa sio mwenzao ungeona comment zingesomeka kama hivi( alitaka akauze akanunue ubwabwa)
   
 19. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #19
  Oct 30, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,347
  Likes Received: 2,685
  Trophy Points: 280
  Hivi huyo Vincent Michael sio kuwa kuna wasiopenda maendeleo walimpandikiza kweli?...najaribu kufikiria kuwa alijiamni vipi hata akaenda kujaribu kung'oa hicho chuma ulichobainisha mleta mada...
   
 20. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #20
  Oct 30, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  kama huwapi elimu watu ,tegemea uchawi,mazingaombwe, udokozi n.k
   
Loading...