Treni ya SGR kuanza kazi imeishia wapi?

Treni ya SGR kuanza kazi imeishia wapi?

Treni imesha anza kazi, ila inafanya kazi Gambishi, maana tukiileta Dar MK254 na @Wakenya wenzake watairoga ikatike vipande vipande

Lakini tukiweka utani pembeni, hivi nini kimekwamisha huo mradi maana mlianza kutupigia makelele kwamba ikifika 2019 hapo Dar-Moro mtakua mnateleza kwa SGR ya umeme. Leo tunaelekea 2024.....
 
Itaanzaje kazi wakati train hazijafika?

SGR hadi leo hawajamaliza kipande cha Moro Dar
 
Masanja Kadogosa akitokea majibu ni wamefika asilimia 90 kipande cha Dar Moro[emoji16]
 
Lakini tukiweka utani pembeni, hivi nini kimekwamisha huo mradi maana mlianza kutupigia makelele kwamba ikifika 2019 hapo Dar-Moro mtakua mnateleza kwa SGR ya umeme. Leo tunaelekea 2024.....
Sio 2024 tu ni mpaka mwisho wa kalenda hakuna kitu pale
 
Za ndaniii zinasema yule jamaa anaetakiwa kuleta vichwa mbali na kukosa winch la kinyanyua vichwa ila aliangukiwa na bomu lililorushwa toka ukrain kwahiyo kiufupi hakuna vichwa vitakavyokuja labda mtumie yale madude yaliokuja na manailoni kama vitumbua😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom