TRC - Sijawaelewa msemapo Tanga, Moshi hadi Kilimanjaro

Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
31,876
33,308
Nawaomba waungwana msikilize na kutazama video hii na kunisaidia kuelewa wanaposema Tanga, Moshi na Kilimanjaro, je Moshi si ipo Kilimanjaro? Au walitaka kusema Arusha?
 
Attachments

  • VID-20190715-WA0008.mp4
    9.6 MB
Kiswahili ni kigum sana mzee. Ukifika Mwanga unakuwa umefika Kilimanjaro lakini haujafika bado Moshi.

Mkuu katika hili tangazo kiswahili kigumu kwa anayesikiliza na kutazama au kwa aliyetengeneza tangazo
 
Hivi umeshawahi kujiuliza serikali yetu kupitia wizara na mamlaka yake wanapotaka kufanya jambo lolote huwa wanakuwa serious kwa kiwango gani?!
 
nadhani walitakiwa waseme tanga ,moshi na kilimanjaro kwa ujumla

Ile reli inapita Same, Mwanga, Moshi na kuendelea mpaka Arusha, nilidhani ili kuweka tangazo vema wangetaja vituo vyote badala ya kutaja mji mmoja na jina la Mkoa kama sehemu tofauti
 
Nawaomba waungwana msikilize na kutazama video hii na kunisaidia kuelewa wanaposema Tanga, Moshi na Kilimanjaro, je Moshi si ipo Kilimanjaro? Au walitaka kusema Arusha?
Ukweli ni kwamba Kilimanjaro siyo sehemu ya Tanzania ndiyo maana hata TRC hawajui tofauti ya Moshi na Kikimanjaro!
 
Mkuu naona kama hapo ulimi umesingiziwa, labda team nzima kuanzia mwenye tangazo, na mtengenezaji yawezekana hawana ufahamu kabisa wa walichoiandalia hadhira
Ufahamu umeelemea kwenye sifa, sio ujumbe.
 
Nawaomba waungwana msikilize na kutazama video hii na kunisaidia kuelewa wanaposema Tanga, Moshi na Kilimanjaro, je Moshi si ipo Kilimanjaro? Au walitaka kusema Arusha?
Acha maswali ya kipuuzi kwani Rukwa na Sumbawanga kwenu tofauti ipo wapi
 
Siku hizi wanakosea sana sijui nn tatizo. Mara elfu 45 na laki nane, mara mwaka 2083 na hii tena 😏😏😏😏
 
Back
Top Bottom