Takriban siku 40 kabla ya msimu mpya wa EPL kuanza timu zote kubwa zimeshaanza kufanya usajili wa nguvu, ...kasoro ARSENAL tu! Alichofanya mzee Wenger hadi sasa ni kumchukua kinda mfaransa Yaya Sanogo (free transfer)
Hii peleka pale juu kwenye thread ni muhimu kwa wadau wa soka wapitie Mkubwa!
Na kuna hili la kiungo matata wa Liverpool FC (Njonjo) kuihama club na kujiunga na Swansea City na ameuzwa moja kwa moja!
Mshambualiaji Arouna Kone (29) amehamia Everton kwa dau linalofikia £6.5m, mkataba wa miaka 3. Kone alikuwa Wigan pamoja na kocha Roberto Martinez msimu uliopita.
Arsenal bado wanamatumaini makubwa ya kukamilisha dili la kumchukua Gonzalo Higuain, pamoja na longolongo zote wanazowekewa na Real Madrid. Mkakati wa Wenger ni kuwapata washambuliaji wawili WAKUBWA kwa msimu ujao.
Timu ya Fulham imeuzwa kwa bilionea wa Kimarekani Shahid Khan (62), baada ya kumilikiwa na Mohamed Al Fayed (84) kwa miaka 16, kwa dili linalokadiriwa kuwa £150 - £200m.
Khan anamiliki kampuni kubwa ya vifaa vya magari Flex-N-Gate.
Arsene Wenger akiongelea fedha za usajili msimu huu: "We have better financial resources than the years before, and it's the resources WE HAVE CREATED OURSELVES. That's massively important to us."