Nadhani sheria inatakiwa kuwa reviewed, mbona wandishi wa habari wanapigwa hadi kuuawa wakiwa kazini na hatuoni hatua zikichukuliwa dhidi ya wahusika, the same law has to apply kwa hawa wala rushwa
Ama kweli huu ni mwaka na mwezi kwa TRAfiki hapa Tanzania kwani kila uchao ni mwendo wa series za matukio ya trafiki. Il nao wamezidi kwa majanga inabidi wajitathmini na kwenda kutubu ili kupunguza munkari wa upanga wa moto unao wanyemelea. Kwani akumbuke zimwi likujualo halikuli ukakwisha...
Hao jamaa wakikukamata katika 18 zao hawana msalie mtume tena kwa nyodo sana wanakwambia ulipe 30000 ambazo hata haziingii kwenye mfuko wa serikali na bado wanakunyanyasa utafikiri ni kosa kuwa na chombo cha usafiri, mbaya zaidi wanakupa notifications ambazo zimepitwa na wakati,FAKE, ukigoma unapewa choice au uache chombo chako cha usafiri mpaka utakapo pata hiyo chenji. hata ukiipata bado kuna usumbufu kukitoa chombo kilichozuiwa!! haki yao kipigo! naonga mkono kwa sana tu.
Kama namsikia huyo mwenye mwanya maneno yake hapo "mmezidi sana, mnajiona mko juu ya sheria, haya maisha na kila kitu, mnachojua nyie rushwa tu. Mbona mnamtetea huyo mwacheni tuendelee kumpa disipilini"