Trafiki apigwa faini badala ya dereva

leiya

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
654
1,558
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Awadh Haji amemwajibisha askari wake kulipa faini ya Sh30,000 baada ya kutaka kumbambikizia kesi dereva. Askari huyo aliyejulikana kwa jina moja la Beatrice alikumbana na mkasa huo baada ya kudaiwa kutaka kumbambikizia kosa, dereva wa gazeti la Jamhuri, Leonce Mujumuzi.

Akizungumza na gazeti kwa simu, Kamanda Haji amesema tukio hilo lilitokea juzi katika mataa ya makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi Kariakoo. Alisema dereva huyo alikuwa akitokea Mnazi Mmoja kwenda Ilala na alipofika katika mataa hayo alisimama baada ya kukuta taa nyekundu ikiwaka na ilipozima na kuwaka ya kijani aliendelea na safari yake.

“Baada ya kuvuka taa za kijani, askari huyo alikutana na dereva katikati nakumweleza kuwa hakufuata ishara yake wakati yeye ndiye alikuwa anaongoza magari. “Hata hivyo dereva alimweleza askari kuwa hakumuona na bali alifuata maelekezo ya taa zinavyoongoza,” alisema Kamanda Haji.

Alisema kuliibuka mvutano wa muda mrefu kidogo kati yake na dereva huyo na mwisho wa siku alimwandikia faini ya Sh30,000 kwa kosa kutofuata ishara yake.
Hata hivyo, Kamanda Haji alisema dereva huyo hakupewa muda mwafaka wa kujitetea baada ya kutokea sintofahamu hiyo hali iliyosababisha Leonce kutokubaliana uamuzi wa Beatrice.


Chanzo: Mwanachi
 
Watupe hii mbinu, ili tuwe tunawarudishia mzigo wenyewe,maana ishakuwa kero.
 
Leo nimefarijika sana baada ya Kamanda wa Usalama Barabarani Kanda Maalum ya Dar es Salaam (ZTO), ACP Awadhi Haji kusimamia Sheria na kumwamuru askari wa Usalama Barabarani WP Beatrice alipe faini ilipobainika kuwa alitaka kumbikia kosa la kupita kwenye taa nyekundu Dereva wa Gazeti la JAMHURI.

WP Beatrice alilazimisha kuwa Dereva Leonce Mujuruzi amepita taa nyekundu wakati alipita taa ya kijani baadaye akabadili kauli na kusema yeye alikuwa anaongoza magari hivyo Dereva Leonce hakupaswa kufuata ishara ya taa bali maelekezo yake WP Beatrice.

Katika kikao tulichofanya Ofisi ya ZTO Awadhi leo Aprili 28, 2017 Dar es Salaam, Afande Awadhi amesema amebaini ukweli kuwa WP Beatrice hakufuata utaratibu anaopaswa kufuata askari anaponkamata Dereva kwa kosa analomtuhumu nalo Barabarani.

Nitaandika kwa kina sakata hili kwenye safu yangu ya SITANII Jumanne ijayo katika Gazeti la JAMHURI, ila kwa ufupi amesema askari akimkamata Dereva anapaswa kufanya yafuatayo:-

1. Askari akimkamata Dereva anaangalia aina ya kosa. Adhabu ya kwanza ni ONYO.

2. Adhabu ya pili imegawanyika sehemu mbili. Dereva akikiri kosa, anapigwa faini. Akikataa anapelekwa Mahakamani pande mbili zisikilizwe na haki itendeke.

Katika shauri lililokuwa mbele yetu, imethibitika WP Beatrice hakumpa fursa Dereva wetu Leonce ya ama onyo au kuchagua kati ya faini au kupelekwa Mahakamani.

In charge wa Traffick Police Msimbazi Inspekta Bihemo, alikuwa ameelekeza Dereva Leonce awekwe ndani na kufunguliwa mashtaka kutokana na Leonce kulalamika kuwa WP Beatrice amemwonea.

ACP Awadhi amesema hayupo kutetea Polisi au Raia. Mwenye makosa anawajibika kwa makosa yake. Amebaini WP Beatrice amekiuka wajibu wake hivyo akamwagiza alipe faini aliyokuwa amemwandikia Leonce.

Nitaandika kwa kina kwenye safu yangu ila nampongeza ACP Awadhi. Sisi kama JAMHURI tumekuwa tukipokea malalamiko juu ya uonevu wa askari.

Si kwamba hatukuwa na Sh 30,000 za kulipa faini, ila tumejiuliza kama askari ana uwezo wa kutubambikia kesi sisi, inakuwaje kwa wasio na kuwasemea?

Ilitubidi tusimame kutetea haki. Tunamshukuru ACP Awadhi kwa kutetea na kusimamia haki bila uonevu.

Tunaamini WP Beatrice na Inspekta Bihemo kuanzia sasa watafanya kazi kwa weledi na kitenda haki kwa kila mmoja.

Asante ACP Awadhi na Mungu akubariki uendelee kusimamia haki, leo, kesho na baadaye.

C&P
 
Uchunguzi gani ulitumika kumbaini huyo askari kwa kitendo hicho?
siku hizi wamewekea malengo basi hata ukiendesha huku unacheka unalimwa faini
Kama sehemu kuna taa na zinafanya kazi kwa ufasaha,hata kama hukumuona askari mradi umezifuata taa upo sahihi tu.
Kama askari kweli alikuwepo sehemu sahihi ambako ni katikati ya barabara lazima angeonekana tu,
 
siku hizi wamewekea malengo basi hata ukiendesha huku unacheka unalimwa faini
Kama sehemu kuna taa na zinafanya kazi kwa ufasaha,hata kama hukumuona askari mradi umezifuata taa upo sahihi tu.
Kama askari kweli alikuwepo sehemu sahihi ambako ni katikati ya barabara lazima angeonekana tu,
Siyo wameweka malengo, wakikuandikia elfu thelathini trafick hapo ana elfu saba yake
 
Mimi ushauri wangu siku au mahali wakiamua kukaa askari wenyewe basi zile taa wawe wanazizima ili zisiwachanganye watu
 
Back
Top Bottom