Mandla Jr.
JF-Expert Member
- Dec 15, 2013
- 3,098
- 631
Moshi. Ofisa wa polisi mwenye cheo cha Koplo, Wilson Mwakipesile wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani Kilimanjaro amefariki dunia ghafla akiwa ndani ya daladala alilokuwa amelikamata.
Hata hivyo, haikujulikana mara moja iwapo trafiki huyo alifariki dunia akiwa njiani kulipeleka gari hilo kituo cha polisi, alifariki muda mfupi baada ya kufika kituoni au wakati anapelekwa hospitali.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz alisema polisi huyo alikufa ghafla akiwa kazini lakini alikataa kuingia kwa undani wa tukio hilo lilitokea Ijumaa kati ya saa 5:00 asubuhi na saa 6:00 mchana, baada ya trafiki huyo kukamata daladala linalofanya kazi zake kati ya Kiborloni na katikati ya mji.
Mmoja wa mashuhuda alisema "Baada ya kuikamata hiyo Hiace (Toyota) pale Kiborloni aliingia kwenye hiyo gari na kukaa kiti cha mbele pembeni ya dereva na kumwamuru kulipeleka kituoni.
"Wakati wakiwa njiani kuelekea kituoni ghafla yule trafiki akawa haongei na akawa anamwegemea dereva… hiyo hali iliendelea hadi walipofika kituoni ndipo dereva akawaeleza trafiki wenzake." Mwili wa polisi huyo ulisafirishwa juzi kwenda Mbeya kwa mazishi.
Chanzo:MWananchi
Kumbe uchagani nako si kwa mchezo???
Yuko mzee mmoja wa kipare anaitwa "Kilenga" ni maarufu sana mkoani kilimanjaro, huyo mzee ana magari (Kilenga Luxury) yanayopiga ruti za Arusha, Moshi, Tanga. Ikitokea trafiki akakamata gari yake basi huo ndo mwisho wa uhai wa huyo trafiki.
Yuko mzee mmoja wa kipare anaitwa "Kilenga" ni maarufu sana mkoani kilimanjaro, huyo mzee ana magari (Kilenga Luxury) yanayopiga ruti za Arusha, Moshi, Tanga. Ikitokea trafiki akakamata gari yake basi huo ndo mwisho wa uhai wa huyo trafiki.
TusihukumuOfisa wa polisi mwenye cheo cha Koplo, Wilson Mwakipesile wa Kikosi cha Usalama Barabarani
mkoani Kilimanjaro amefariki dunia ghafla akiwa ndani ya daladala alilokuwa amelikamata.
Hata hivyo, haikujulikana mara moja iwapo trafiki huyo alifariki dunia akiwa njiani kulipeleka gari hilo
kituo cha polisi, alifariki muda mfupi baada ya kufika kituoni au wakati anapelekwa hospitali.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz alisema polisi huyo alikufa ghafla akiwa kazini lakini
alikataa kuingia kwa undani wa tukio hilo lilitokea Ijumaa kati ya saa 5:00 asubuhi na saa 6:00 mchana,
baada ya trafiki huyo kukamata daladala linalofanya kazi zake kati ya Kiborloni na katikati ya mji.
------------------------------------------------------------------
Kumbe uchagani nako si kwa mchezo???
Tusihukumu
Acha kuwajambisha askari kwa ushirikina. Wengine wanalindwa kwa damu ya Yesu
Huo ni ukatili na ushetani kwa binadamu mwenzako anayetafuta maisha, mshauri kama yeye ni mlozi sana afanye hivi: Magari yake yote yawe hayawezi kuonekana kwene macho ya trafiki, as simple as that.Yuko mzee mmoja wa kipare anaitwa "Kilenga" ni maarufu sana mkoani kilimanjaro, huyo mzee ana magari (Kilenga Luxury) yanayopiga ruti za Arusha, Moshi, Tanga. Ikitokea trafiki akakamata gari yake basi huo ndo mwisho wa uhai wa huyo trafiki.
Yuko mzee mmoja wa kipare anaitwa "Kilenga" ni maarufu sana mkoani kilimanjaro, huyo mzee ana magari (Kilenga Luxury) yanayopiga ruti za Arusha, Moshi, Tanga. Ikitokea trafiki akakamata gari yake basi huo ndo mwisho wa uhai wa huyo trafiki.
Ndio zetu hizo mkuu, watu wanaamini uchawi kuliko vyote ila mbele za watu utasikia "mie mambo ya ushirikina sipendi"lakini akiwa chocho au na hizi ID zetu anautukuza huyosio kila kitu ni uchawi aisee... acha mawazo vimini