Traffic police fuatilieni tatizo hili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Traffic police fuatilieni tatizo hili

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Magobe T, May 26, 2009.

 1. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #1
  May 26, 2009
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180
  Baadhi ya makondakta wa daladala wanatoa tiketi ambazo haziendani na namba za magari yenyewe. Zamani nilipokuwa nikipewa tiketi, nilikuwa naitunza na baadaye kuitupa bila kusoma imeandikwa nini.

  Baadaye, niliamua nikipewa tiketi niwe naisoma na kuona kama inaendana na namba za gari yenyewe na route ya gari. Tangu nianze kufanya hivyo, nimegundua kwamba tiketi haziendani na namba za magari lenyewe. Sijui ni kwa nini makondakta wanafanya hivyo.

  Lakini kama litatokea tatizo fulani, mfano, ajari au abiria kupoteza mzigo au mtoto au mgeni itakuwa vigumu kwa abiria huyo kubaini gari alimojipakia na pia kama ni kitu cha dharura itashindikana kutoa ushirikiano kwa mamlaka husika kwa ufuatiliaji vile tiketi siyo za gari lenyewe.

  Kwa hili, naomba traffic police walifuatilie kwa karibu na makondakta wanaopatikana wakifanya ulaghai kama huo wapewe adhabu zitakazowafunza kuwa wawajibikaji katika kazi zao.

  Inafaa pia abiria wapewe maelekezo ili kama watabaini vitu vya namna hiyo, waweze kupeleka matatizo yao kwenye mamlaka husika na ikiwezekana wapewe namba za simu za mkononi ili wawasiliane na mamlaka hizo.
   
Loading...