KERO Traffic lights za Kijitonyama Mataa Tatizo

KERO Traffic lights za Kijitonyama Mataa Tatizo

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Sitaki kuamini kwamba mataa ya kuongozea waenda kwa mguu na magari pale Kijitonyama siku hizi hayafanyi kazi!

Yaani ni kero kubwa sana kwa sababu unakuta zile taa za waenda kwa mguu unakuta ile picha nyekundu ya mtu akiwa amesimama siku hizi haibadiliki. Hivyo muda wote ni magari tu na pikipiki, lakini waenda kwa mguu muda wote unakuta wamesimama au walazimishe kupita wakati ambao magari yanapita.

Watu wanaohusika tunaomba waweze kuchukulia hili suala la uzito, ni hatari sana kukatiza barabara sehemu kama hiyo bila kuongozwa na taa maalumu.

Kwani wanaohusika na taa za barabarani ni akina nani hadi taa zisirekebishwe ikiwa kuna tatizo? Hawaoni kuwa watu wanaweza kugongwa sana na magari?
 
Back
Top Bottom