TRA yawataka 'mawinga' kulipa kodi

TRA yawataka 'mawinga' kulipa kodi

Tusimlaumu bure huyo dada pichani naona alikuwa tayari ameshabugia Ka flying fish kidogo🤣🤣🤣🤣
 
Wachina wanaondoka, hilo jukumu lazima libebwe na mawinga hahahaha.
 
Mbona hawajui na mbinu namna ya kutumia Kodi kiusahihi Bali zinafujwa hawasemi kuwa huo sio uzalendo
 
Mdomo mdomo mdomo. Kuna kidada kikihojiwa ETI kinasema mawinga wanaingiza HADI milioni moja kwa wiki nikashangaa HIVI HUYU anajua anacho kizungumzia mitandaoni na HASARA zake? Ona SASA.



Kwishaaaa
 
Shida ya CCM na watendaji wao huwa ni mkaranganyiko wa fikra katika kufikiria kwao.

Sasa hebu jiulize.

Wanataka mawinga walipe kodi,je mawinga ni ajira rasmi ambayo serikali imeidhinisha kuwa ni mfumo halali wa kiuchumi?

Mawinga ni watu wanaojitafutia pesa ya maisha nje ya mfumo rasmi ya ajira na uchumi baada ya kukosa ajira au mitaji ya kujiajiri. Hakunaga kitu kinaitwa winga katika uchumi rasmi wapi uwinga ulihalalishwa kwa sheria ipi ya uchumi au kibiashara.

Hizo bei wanazoweka mawinga kuna top price juu ya bei original ambayo serikali imeridhia katika soko,na matokeo yake ni mifumuko ya bei na kuleta inflation, unakwendaje kutax mfumo batili ambao unachochea mfumuko wa bei?

Ingekuwa winga wanapewa kiatu na kuuza kwa bei ile ile ya dukani na wao kulipwa sales commission na mwenye duka ningesema sawa hata serikali iwatambue kama sales personnel wa kimtandaoni. Ila mtu anaenda karikoo anapewa kiatu kwa mali kauli,bei ya dukani ni 15,000/= yeye anakwenda kutangaza mtandaoni anakiuza 60,000/= na anauza kiatu chenyewe unakuta material yake ni cheap na kinaharibika ndani ya mwaka. Hii si ni kuchangia mfumuko wa bei katika uchumi? Why serikali wategemee kodi kwa watu wa namna hii sasa?

Hawa TRA watashindwa kweli kuja kuwekea kodi machangudoa na wadangaji kama ajira rasmi?

Watashindwa kuweka kodi kwenye michango ya harusi na birthday party?

Kuna muda nahisi hili taifa linaongozwa na watu wasio vaa chupi na wakienda msalani hawaflush. Hivi mtu timamu unaweza watax watu wanaodalalia bidhaa ambazo tayari zinabei ya soko ila wao wameweka cha juu na kufanya ulaguzi lwa wateja kupitia account za social networks mitandaoni?🤔

Mambo ya hovyo kabisa.
 
Back
Top Bottom