chinchilla coat
JF-Expert Member
- May 16, 2016
- 5,107
- 10,969
Mamlaka ya mapato Tanzania imevuka lengo la ukusanyaji wa mapato kwa mwaka 2015/2016 kwa kukusanya kodi ya shilingi trilioni 13.371 sawa na asilimia 100.04% ya lengo lilipoangiwa na serikali kwa Tanzania bara na Zanzibar
Kamishna wa mapato Tanzania amesema mapato hayo ni ongezeko la asilimia 23.70 ukilinganisha na mapato ya mwaka wa fedha 2014/2015
Akizungumzia suala la bandari amesema pamoja na mizigo kupunga bado wanakusanya kodi kubwa ya zaidi ya bilioni 400 hadi 500 kwa mwezi ukilinganisha na wastani wa bilioni 200 hadi 300 kwa mwezi waliokuwa wanakusanya kabla na sasa bandari haitumiki kama uchochoro wa kupitishia bidhaa kama ilivyokuwa mwanzo
Pia wamezungumzia suala la kodi ya VAT na kusema kodi hiyo itakatwa kwa watoa huduma na sio wananchi