TRA yampiga faini ya 3,500,000 dereva kisa kapakia tenga 27 za nyanya

gimmy's

JF-Expert Member
Sep 22, 2011
3,283
3,274
Siku chache zilizopita niliandika kueleza ugandamizwaji unaofanywa na TRA uliomuhusu dereva mmoja wa semi ambae alipigwa faini ya 3,000,000/= kisa kapakia tenga 20 za parachichi na alipoulizwa risiti ya transport hakuwa nayo kwani mzigo ule haukuhusu ofisi,ilikuwa ile kawaida ya madereva kujiongezea kipato kwa vimizigo vya njiani ambacho kilimponza akapoteza ajira.

Sasa huyu ni muendelezo wa vitimbi vingine kwani dereva mwingine amepigwa faini ya 3,500,000/= kisa kapakia tenga 27 za nyanya na alipoulizwa risiti ya transport hakuwa nayo. Dereva huyu analazimika kukatwa hii pesa na ofisi kwenye mshara mpaka deni litakapoisha.

Kwakweli kama hizi ndio sheria zilizotungwa kwa ajili ya kutetea wanyonge basi hiki ni kituko.

Hivi mshahara wa Rais ni sh ngapi, mawaziri pesa ngapi, wabunge je? Hawa hawatusikii kwakuwa wao wanalipwa pesa ndefu, hivi dereva mwenye mshahara wa laki tatu kwa mwezi atakatwa hilo deni mpaka lini?

Ushauri wa bure ni kwamba;hii miradi mikubwa ilioanzishwa nchini inasababisha mateso kwa raia,ni bora tukarudi kwenye mgao wa umeme kuliko haya maisha ya karaha tunayoishi sasa.

Kwakweli nachuma dhambi ila kama Mungu anasikia vilio vyetu basi.
 
Sio muumini wa hii serikali ila ukweli Lazima usemwe. Kwa hilo swala lako Dereva ana makosa kwasababu alitakiwa amkatie risiti ya EFD huyo mteja wake ya huo mzigo.

Kwa hiyo Kosa hapa liko kwa dereva. Kwanini hakumkatia risiti ya EFD mashine huyo mteja wake?
Wacha limkute
 
tukarudi kwenye mgao wa umeme
Ushindwe na ulegee sana hadi mawazo haya mabaya yakutoke kichwani, kisha ujazwe mawazo mema kwa manufaa ya watanzania wote.
====
Nampa pole huyo dereva. Hata hivyo, TRA wawe wanafanya kazi kwa kutoa elimu ya kutosha juu ya sheria zote zinazoboreshwa juu ya kodi na makato mengine. Si busara wala hekima kuficha elimu ya sheria kwa wahusika ili uwavizie kuwatoza faini! Kuna na "mfuko mwingine wa masuala ya wafanyakazi wa viwandani", nao ulikiwa na mtindo wa namna hii lakini nadhani umeishajirekebisha.
 
Kipo kilio kwa wafanyabiashara wenye deni la kodi kufungiwa kutoa pesa " Agency notice" waraka wa TRA maelekezo bank husika ya mteja. Waziri wa fedha, biashara nk washauri vinginevyo watu wengi wawezao wataepuka mfumo wa bank hivyo kuharibu mfumo mzima wa uchumi!
 
Kipo kilio kwa wafanyabiashara wenye deni la kodi kufungiwa kutoa pesa " Agency notice" waraka wa TRA maelekezo bank husika ya mteja. Waziri wa fedha,biashara nk washauri vinginevyo watu wengi wawezao wataepuka mfumo wa bank hivyo kuharibu mfumo mzima wa uchumi!!!
Side effects ya hili jambo wafanyabiashara kutokuweka pesa benki, hatimaye benki kuyumba kiuchumi!

Ndio maana wahindi na Wachina hawaweki pesa benki, pindi akipata pesa ananunua dola anaficha ndani.
 
Ushindwe na ulegee sana hadi mawazo haya mabaya yakutoke kichwani, kisha ujazwe mawazo mema kwa manufaa ya watanzania wote.
====
Na mpa pole huyo dereva. Hata hivyo, TRA wawe wanafanya kazi kwa kutoa elimu ya kutosha juu ya sheria zote zinazoboreshwa juu ya kodi na makato mengine. Si busara wwla hekima kuficha elimu ya sheria kwa wahusika ili uwavizie kuwatoza faini! Kuna na "mfuko mwingine wa masuala ya wafanyakazi wa viwandani", nao ulikiwa na mtindo wa namna hii lakini nadhani umeishajirekebisha.
Kuna sheria nyingine ni zao la watunzi matajiri ambao wakati wanazitunga hawakufikiria watu masikini, utawala wa awamu hii unatesa wananchi kuliko mkoloni.

Siku moja nilishamsikia mfanyakazi wa TRA akisema kwenye utawala huu hatafanya biashara yoyote inayoingiliana na kodi za serikali.
 
Kipo kilio kwa wafanyabiashara wenye deni la kodi kufungiwa kutoa pesa " Agency notice" waraka wa TRA maelekezo bank husika ya mteja. Waziri wa fedha,biashara nk washauri vinginevyo watu wengi wawezao wataepuka mfumo wa bank hivyo kuharibu mfumo mzima wa uchumi!!!
Kuna mfanyabiashara namjua alifunga acc number zake zote kwa sababu ya TRA.

Kama anapeleka pesa benk basi ni kwenye acc binafsi
 
Tenga 27 kwa bei ya juu kabisa ya mwezi uliopita ni 675,000 Tsh.

Faini inapigwa 3,500,000. Mfano angelipa kodi ilitakiwa iwe shilingi ngapi?

Kuna miongozo ya faini? Mfano thamani ya kipi inaangaliwa mpaka kuamua mzigo wa 675,000 faini iwe 3,500,000?
 
Back
Top Bottom