TRA Yakusanya Sh Trilioni 8.42 Kwa Miezi Sita

McCain

JF-Expert Member
Dec 2, 2016
1,169
517
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imekusanya Sh trilioni 8.41 kuanzia Julai mwaka jana hadi Januari mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo, inaonesha makusanyo ya Januari mwaka huu ni Sh trilioni 1.14.

Kayombo alisema pamoja na juhudi za kukusanya kodi mbalimbali, hivi sasa wameelekeza nguvu katika kukusanya kodi ya majengo kwa kutoa ankara kwa wamiliki wa majengo katika mikoa mbalimbali.

“Wamiliki wa majengo wanakumbushwa kwamba kodi ya majengo inakusanywa na TRA kuanzia Julai mwaka jana, hivyo tunawaomba watoe ushirikiano kwa kulipia ankara zao kwa wakati,” alisema Kayombo.

Kuhusu zoezi la uhakiki wa Namba ya Mlipakodi (TIN), alisema kuna mafanikio makubwa na kwamba wananchi wa mikoa ya Arusha, Mwanza, Kilimanjaro, Dodoma, Mbeya, Morogoro, Tanga na Pwani waitikie wito huo mapema kuepuka usumbufu.

Chanzo: Mtanzania
 
Zinaenda wapi sasa mbona hatujafanya kitu cha maana.

KATI YA HIZO MISHAHARA NI 50%=TILLION 4.2 KWA HIYO BAKI NI TILLION 4.2 AMBAYO INAGHARIMIA MAFUTA,MADENI YA NCHI, NA KUWEKEZA. KWA KWELI MAGUFURI ANAKAZI. KAMA TUNGEKUWA HATUDAIWI NADHANI INGEKUWA POA
 
Kingekuwa kipindi cha yule bwana zote zingekaa mifukoni mwa riziki no ² tungeambiwa 1 trillion
 
Siyo zote zinatokana na makusanyo ya TRA, kuna nyingine zitatoka kwa Donors wa nje. So ukijumlisha zote ndo unapata Tr. 29.
Hapo hakuna donors acha uchochezi kama yule bwana mwenye majina feki ya watuhumiwa wa unga
 
Stand by,Action!!! wakiona mwezi fulani hata watumie calculator na vikokotozi vyote hesabu inakataa,sasa wanakuja na hesabu ya jumla jumla na visentence kibao ndani yake kumvuruga Mtanzania.baadae watakuja na hesabu ya mwaka mzima,Tusubiri.
 
Back
Top Bottom