TRA yajipanga kudai mabilioni CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TRA yajipanga kudai mabilioni CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MAFILILI, Jun 8, 2011.

 1. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,915
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 160
  CHAMA cha CHADEMA, ambacho kinadaiwa kukwepa kulipa kodi halali za serikali, kimeshindwa kutoa taarifa za mapato kwa kile kilichodaiwa kumbukumbu zimepotea. Badala yake, CHADEMA imetoa taarifa ya hesabu za mikoa mitatu ya Kilimanjaro, Arusha na Dar es Salaam, za kuanzia mwaka 2007 hadi 2010, huku ikidaiwa kutolipa kodi tangu kuanzishwa kwake.

  Kutokana na hilo, CHADEMA iko katika hatari ya kudaiwa mamilioni ya shilingi na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ambayo imeanza kufanya uchunguzi wa madai hayo. Habari za kuaminika ndani ya TRA zimesema taarifa ya hesabu za chama hicho kwa mikoa hiyo zina utata na zinaonyesha ukwepaji kodi.

  Katika utetezi wake kwa maofisa wa TRA, CHADEMA imedai haiwezi kukatwa kodi kwa kuwa inawalipa watendaji wake posho na si mishahara.

  Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari, maofisa wa TRA katika uchunguzi wamebaini fedha wanazolipwa watendaji wa chama hicho ni nyingi kuliko kima cha chini cha mshahara. Sheria ya Kodi inaagiza posho yoyote inayozidi kima cha chini cha mshahara kukatwa kodi. "Taarifa zao zinaonyesha kodi hawalipi na viongozi wao wanasema hawalipani mishahara bali ni posho, lakini kisheria posho inayozidi sh. milioni moja inakatwa kodi,'' kilisema chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya TRA.

  Uchunguzi wa kina uliofanywa na gazeti hili umebaini CHADEMA iliwasilisha taarifa ya fedha ambayo ina dosari.

  Watendaji ambao hawalipiwi kodi ni pamoja na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, anayelipwa mshahara wa zaidi ya sh. milioni 7.4, fedha ambazo ni nyingi kuliko mshahara wa mbunge.

  Dk. Slaa alishawahi kuhadaa Watanzania kwa kupaza sauti akidai mshahara wa mbunge ni mkubwa hivyo upunguzwe. Kuibuliwa ufisadi huo ndani ya CHADEMA kulimfanya Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa chama hicho, Anthony Komu na Mjumbe wa Kamati Kuu, Mabere Marando kukanusha kupitia vyombo vya habari wakidai ni uongo.

  Komu alidai Dk. Slaa analipwa mshahara wa sh. 1,725,000 na lita 1,000 za mafuta kila mwezi, wakati waraka ambao Uhuru inao unaonyesha mamilioni ya fedha yanayochotwa na mtendaji huyo. Viwango hivyo ni mwendelezo wa mapendekezo ya posho ya Dk. Slaa kama Azimio la Kamati Kuu iliyokutana Januari 29 na 30, mwaka huu, mjini Dar es Salaam na kuonyesha kuna tofauti kubwa na maelezo waliyotoa Komu na Marando.

  Kwa mujibu wa waraka huo ambao hauonyeshi kiwango kinachokatwa kodi, posho ya Dk. Slaa imegawanywa katika sehemu sita ambazo ni posho ya mwezi, fedha za mafuta, majukumu, viburudisho, nyumba na utendaji kazi. Wakati Komu katika ufafanuzi wake alisema Dk. Slaa analipwa mshahara (basic) wa sh. 1,725,000 waraka unaonyesha analipwa sh. 2,300,000. Mbunge analipwa sh. 2,305,000 kabla ya kukatwa kodi.

  Kwa upande wa posho, Dk. Slaa analipwa fedha za mafuta sh. 1,387,500 kwa wastani wa lita 750 kwa mwezi, huku fedha za majukumu zikiwa sh. 575,000, mawasiliano sh. 460,000 na nyumba sh. milioni moja. Posho nyingine ni kwa ajili ya viburudisho sh. 462,500 na utendaji kazi sh. 989,000. Mshahara huo umefanywa maalumu kwa Dk. Slaa pekee na iwapo chama hicho kitapata katibu mkuu mwingine hawezi kulipwa hivyo. Dk. Slaa anadaiwa kupata posho ya nyumba mara mbili, kwani ilipendekezwa alipwe sh. milioni 40 ili kukamilisha ujenzi wa nyumba yake eneo la Mbweni, nje kidogo ya mji wa Dar es Salaam, ambako anaishi kwa sasa.

  Hata hivyo, licha ya kulipwa fedha hizo Dk. Slaa ameendelea kupewa posho ya nyumba ya sh. milioni moja kila mwezi.


  Source: Gazeti la Uhuru, Juni 8,2011


  KAZI KWELI KWELI CDM
   
 2. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Luoga in action....wakubwa wetu bwana usiwakosoe hata kidogo...kama vile hawakosei
   
 3. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #3
  Jun 8, 2011
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Gazeti la UhUrU
   
 4. Mumwi

  Mumwi JF-Expert Member

  #4
  Jun 8, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 592
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Bado mnasomaga tu uhuru?
   
 5. Zegreaty

  Zegreaty JF-Expert Member

  #5
  Jun 8, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 638
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  gazeti lenyewe hivi linakuwaga na wateja kweli hilo?au ukiwa una kadi ya magamba tu ukionesha unapata nakala yako papo hapo?:becky::becky::becky:
   
 6. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #6
  Jun 8, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,915
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 160
  Wewe mawazo yako mgando, hauwezi kuamini habari sharti itolewe na TZ Daima pekee!
   
 7. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #7
  Jun 8, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Wakamdai kikwete, mbona mshahara wake haukatwi kodi? Au nao ni posho? Vilevile hizo ni mbinu chafu na umeagizwa na nepi, tra wakague mahesabu kwani chadema imekua kampuni?

  ni lini ccm ilikaguliwa? acheni use nge? Mkaguzi wa mahesabu ya vyama vya siasa ni msajiri wa vyama vya siasa na c tra.
  wakakague yale magari ya ccm yaliingia kwa msamaha wa kodi hatukuongea, mabango ya kampeni za kikwete hamna lililo lipiwa kodi hata moja, na vile vibanda vyao vya biashara ni lini walilipa kodi ya mapato tra?

  ccm inamiliki nyumba nyingi sana na imepangishia watu mbalimbali nikiwemo mimi na ile ni biashara lakini hawajawahi lipa kodi tra hata siku moja?
  na vile viwanja vya mipila vya ccm huwa kuna % wanapewa je walisha wahi lipia ushuru?
  ccm mpaka leo haijawatangazia wananchi ilitumia kiasi gani kwenye uchaguzi ulio pita na hata wa 2005.

  mplekee nepi hii samary fupi ke nge wewe.
   
 8. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #8
  Jun 8, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  TRA fanyeni haraka kuwadai ili kazi ya CDM iwe rahisi zaidi.
   
 9. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #9
  Jun 8, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  wewe unaye soma hilo gazeti waulize wafanye ulinganifu na chama kingine ambacho kinafanya vizuri ili kiwe reference na hasa CCM, aidha waambie TRA waijibu tuhuma za kumuuingizia umasikini TANGO. wafanye kazi waache siasa na umbea.
   
 10. MWEEN

  MWEEN JF-Expert Member

  #10
  Jun 8, 2011
  Joined: Feb 6, 2010
  Messages: 472
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Walikuwa wapi toka CDM ianzishwe. Maofisa wao wanapotajwa kuwa ni mafisadi wanalipa kisasi. Wanatumia uti wa mgongo kufikiria badala ya ubongo! Mwaka huu wataipata kwani wahisani hawatatoa pesa zao mpaka wajisafishe na kuacha kutumiwa kisiasa. Wanajisahau kuwa wananchi wanajua wanachofanya hivyo HAWADANGANYIKI TENA.

  Wanatakiwa wafikiri namna ya kuongeza walipa kodi na kuondoa misamaha ya kodi sio kulipa visasi.TRA sio mali ya watu wachache ni ya Tanzania.
   
 11. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #11
  Jun 8, 2011
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Loo nimepodeza muda wangu. kumbe source ni gazeti la uhuru!
   
 12. C

  CHESEA INGINE Senior Member

  #12
  Jun 8, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 180
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kama kweli TRA wako makini kiasi hicho wangeenda kwa wakwepa kodi wakubwa wanaofahamika kwa wengi na si kwenye taasisi kama hizi. Wangewarekebisha kama kuna dosari za hapa na pale si kulivumisha kiasi hiki. Na hili si kwa Chadema tu ni kwa vyama vyote. Kuvuana nguo huku hakutaishia pazuri. Leo umenvua Chadema kesho CCM keshokutwa CUF mtondo goo NCCR hii kwa TRA itawaweka mahala pabaya na jamii. TRA wakipelekewa tuhuma wasiwaambie vyombo vya habari wazifanye kimya kimya mambo ya wateja wao wasiyapeke kwenye vyombo vya habari! Haswa kwa hivi vyama vyetu vya siasa. Wakaguzi wafanye kazi zao kwa makini wao kama wanataka kuwaumbua kwenye vyombo vya habari sawa! lakini isiwe TRA!
   
 13. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #13
  Jun 8, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hata mimi, Mod tusaidie kuondoa hii crap!
   
 14. The Emils

  The Emils JF-Expert Member

  #14
  Jun 8, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  gazeti la uhuru magamba? Nasikitika kupoteza mda kusoma riwaya ya ****
   
 15. k

  kizazi kipya JF-Expert Member

  #15
  Jun 8, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  sio lazima itoke tanzania daima,but ikiandikwa na uhuru ni upuuzi na propaganda za kijinga,afadhali hata zingeandikwa na sani au ijumaa kuliko ile toilet paper
   
 16. m

  mbagasa Member

  #16
  Jun 8, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi tra ni wanasiasa au watumwa wa siasa,je wao wanalipa kodi ya mishahara wanayojilimbikizia?Kwa kazi aliyoifanya Dk. slaa ni kubwa anapaswa kulipwa zaidi ya hapo.
   
 17. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #17
  Jun 8, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  CCM Kirumba wameshalipa wao?:confused2:
   
 18. M

  MAJANI YA KUNDE JF-Expert Member

  #18
  Jun 8, 2011
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 213
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Gazeti la Uhuru, Habari leo ,TBC1 Radio Uhuru,TBC
  zinatia kinyaa kuziona ,kusikia,kuyasoma Ole wenu nyie Vibaraka wa Chama cha Mafisadi sijui mtakimbilia wapi kesho.
   
 19. m

  mozze Senior Member

  #19
  Jun 8, 2011
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 185
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mamilioni ni kiasi gani?
  Dr. Slaa kaanza lini kulipwa hicho kiasi mnachosema?
  Je gharama za kufanya huo uchunguzi na Watakachopata TRA ni halali?

  Huu ni upuuzi, na matokeo yake ni kuwa Wananchi watapoteza imani na hao TRA mana hawata come up na anything kusaidia masikini wa tanzania...... je kipato cha CDM na cha CCM kipi kikubwa? CDM vs Makampuni ya Madini/ mafuta etc?????
  Hili Gazeti ni waliochakaa fikira!
   
 20. F

  FJM JF-Expert Member

  #20
  Jun 8, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Ili tuamini kwelie UHURU hawajatumwa, basi wangetuandikia record ya ulipaji kodi wa CCM. hilo tu Uhuru tulinganishe wawili hawa.
   
Loading...