Hii ndio Tanzania, zaidi ya uijuavyo, yaani haishi vituko. Mosi, gazeti la Uhuru ndio limekuwa Afisa Habari wa TRA? Pili, TRA walikuwa wapi mpaka Chadema ikakwepa kodi kwa miaka 19? Tatu, rekodi ya ulipaji kodi ya CCM iko wapi? Nne, TRA wameshindwa kukusanya kodi kwenye sekta nyeti ya madini, mafuta na biashara leo wanataka tuamini kuwa Chadema ndio wakwepaji wakubwa wa kodi? Tano, kwa Tanzania kodi hulipwa kutokana vipato vya uwekezaji, ajira na biashara. Kimantiki chadema haiwezi kukwepa kodi kwa sababu haifanyi biashara, haina uwekezaji na haijaariwa. Tunaposema wamekwepa kodi tuna maana gani? Ushuru wa forodha, kodi ya mapato, ushuru wa stemp, kodi ya ongezeko la thamani, kodi ya majengo, Skill and Development Levy, withholding tax? Kuhusu kodi ya mapato ya waajiriwa PAYE, mwajiriwa ndiye anayelipa kodi ambapo mwajiri ana jukumu la kukata kodi hiyo kwa mujibu wa sheria kutoka ktk mshahara na mapato mengine ya mwajiriwa na kuwasilisha TRA. Taarifa zilizopo zinaonyesha mpaka mwaka jana mwishoni chadema ilikuwa ikipata ruzuku ya sh mil. 20 hivi na baada ya uchaguzi kiasi kimeongezeka mpaka zaidi ya mil 200. Taratibu za kisheria zipo za kupambana na ukwepaji wa kodi (anti-avoidance/evasion) inashangaza kwanini hazitumiwi. TRA fanyeni ukaguzi mtoe kadirio la kodi wanayodaiwa chadema walipe kwa mujibu wa sheria. Tuache kulialia. Hitimisho, ukanjanja na ushabiki wa kisiasa unadharirisha taaluma ya habari. Kuandika chadema wamekwepa kodi bila kusema aina ya kodi na kiasi cha kodi husika ni ishara kuwa waandishi wetu wana fikiri kwa kutumia matumbo yao. Tanzania ya leo sio ya jana wala juzi, wallaah iko siku bubu atasema halafu watawala watakosa pa kushika. Mungu ibariki Tanzania.