TRA yaikadiria ACACIA deni la Tsh. Trilioni 425.4 kama Malimbikizo ya Kodi

kama kweli wamekaa chini na kutumia akili zao vizuri na kulete udanganyifu huu kwa uma hakika huko serikalini hakuna viongozi, kama sio mwenyezi mungu yupo upande wetu hata hapa tusingekuwepo. ifike mahali basi tukue tuache utoto jamani si aibu hii!
 
Kwa hiyo ACACIA Wasipotoa hata mia ndo furaha yako, siyo? huduma za jamii zikiwa mbovu unakuwa wa kwanza kutoa povu
TRA ilikuwa wapi siku zote? Mm sifurah ila hyo hela hawezi kuitoa.. Unacheza na trilion nn babu, au unafikiri ni buku jero hiyo trilion
 
TRA ni financial institution, kamati iloundwa ni temporary, wao hawatakiwi kufuata kamati inasemaje, wao wanatakiwa wafanye audit kwa kufuata taratibu na kutumia documents husika, sio matokeo ya kundi la watu wengine ambao hawajulikani tena. Ukitaka kufanya audit, lazima upeleke notice kwa mhusika, ueleze nia yako, na kitu gani upatiwe (kama documents zipi?), then unapewa mda wa kujitaarisha. Kisha ndio waje wakusanye izo document wakafanye mambo zao. Sasa wao TRA wamefanya hivo?
Mkuu jiongeze basi sasa hivi kila mtu wa serikali anafanya kazi kwa kumuungalia mkulu anataka nini na sio utaalamu unataka kazi aifanye vipi. We unafikiri TRA hawajui hayo unayoyasema wanajua sana tu ila nao wanapenda kazi zao. Kuna vitu mkulu anavitafuta na atavipata muda si mrefu ni suala la muda tu na hata hao wataalamu yatakapotokea hayo nao watakuwa wanachekelea chooni!
 
TRA ilikuwa wapi siku zote? Mm sifurah ila hyo hela hawezi kuitoa.. Unacheza na trilion nn babu, au unafikiri ni buku jero hiyo trilion
Unaelewa nini inaposemwa 'ukwepaji' au kufanya 'udanganyifu' !?
 
Sijui mambo ya madeni pamoja na mikataba ila TUKILIPWA HIZO PESA NITATEMBEA KUTOKA MAGU HADI DAR KWA MIGUU KUJA KUZIONA BENKI.

Usinisahau kwenye Baraza Jipya.
 
Nimeishia kucheka tu

Kampuni haijasajiliwa ila inapokea assessment ya kodi. Kampuni hewa ila TRA wana data zake!!!!!!!!

Kinachoniuma hapa ni kuwa watz tunapumbazwa na propaganda za makinikia wakati kitu pure kinapaa na ndege. Kama kuibiwa ni kweli tumeibiwa na tunaendelea kuibiwa kwa hisani ya usanii wa CCM.

$204billion ni kama 420trilion Tsh. Hii ni budget ya TZ miaka 15. Kama walikuwa wanalipa kodi isiyozidi 15% inamaana hawa jamaa walikuwa wametengeneza zaidi ya $900 billion from Tanzania ndani ya miaka 17. Na hapa acacia ni branch tu ya Barrick. Hii pesa tungekuwa tunalipwa, hivyo basi kodi ya Acacia ingetosheleza kufinance budget yetu ya miaka 17 iliyopita. Yani Watanzania tungekuwa hatulipi kodi wala kuomba mkopo. Yan ni kupokea kodi tu toka acacia na sisi tungekula tu bata.
8db4829c43c06d8b06ad4fe19c6f3bf2.jpg


Kumbuka pia acacia ni moja tu ya Gold mine company in Tanzania. Kuna mgodi mikubwa unaomilikiwa na AngloGold& Ashant kama bonge la openi pit lile la "Geita Gold Mine(GGM)' lililoanza operation toka mwaka 2000. Kwa pesa tunayowadai acacia, kama Geita Gold mine nao wangekuwa wanalipa kodi iyo, bac Tanzania ingekuwa na uwezo wa kupokea zaidi ya $30billion kutoka katika iyo migodi miwili tu. Hata budget yetu tungekuwa tunaongelea zaidi ya Trillion 100 kwa mwaka.

Ki uhalisia, GGM wao hawalipi kodi ya zaidi ya $300 million kwa mwaka. Ila Acacia ndyo wanatakiwa kulipa mara 50 yake kwa mwaka. Na kama ni kweli acacia wanatuibia na iyo ndyo pesa wanayopaswa kutulipa, basi hata na GGM wanatuibia sana sambamba na migodi mingine.

466349f6eb07d7cc7646bff5abb4c811.jpg


Tanzania ni nchi ya 4 duniani kwa kuzalisha Gold. Tanzania imekuwa ikizalisha Gold yenye value isiyozidi $1.5billion kwa mwaka. Ila kwa kodi tu tunayoidai acacia ni kuwa mgodi mmoja uliweza kutoa gold yenye thamani zaidi ya $70billion kwa mwaka.

South Africa NI nchi inayoongoza katika uzalishaji wa Gold. Lakini haijawai zalisha gold yenye value inayofikia $4billion kwa mwaka. Kwa maana hiyo, kwa data wanazotumia TRA, Tanzania inabidi ndyo iwe nchi inayoongoza uzalishaji wa gold na ipewe Guiness Award kwa kuvunja record ya kuzalisha Gold nyingi kiasi kuwa hata dunia nzima haikuwai zalisha.

Inabidi ifikie atua watu wazima waache kufanya maigizo ya kitoto aseeee. Watanzania sio wajinga to that extent.


Siku acacia wakilipa hata 10% ya ilo deni, mimi nitatembea uchi toka kibiti hadi kariakoo. I swear.

Sent using Jamii Forums mobile app
Aliyepewa notice ni Acacia au Bulyahulu n.a. Buzwagi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo letu watanzania wa sasa, hatuangalii tena facts na uzalendo.Misimamo yetu imeegemea kwenye Ukabila,Ukanda na Uchama.Tunaamini katika bora tukose wote kuliko fulani apate.Nyerere bado hakuumaliza Ujinga Nchi yetu unarudi haraka sana.eti wanasubiri Noah zao.Utani kwenye mambo mazito.
 
Kitu ambacho sipendi kitokee ni kubeba hela kwenye toroli halafu unaenda kununua nyanya sokoni.....
Badala ya kuanza kuandaa hayo matoroli wewe unasema hupendi itokee, hiyo lazima itokee, mnataka itokee Zimbabwe tu kwenu hapana wakati mliyataka wenyewe.
 
Ndyo maana watanzania mnapotoshwa na mnapotoka ki kweli kweli maana mnashadadia mambo hata hamuyaelewi.

Kwa kukusaidia ni kuwa acacia ndio wamiliki wa iyo migodi miwili.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanini unataka tuamini wewe unachosema ndio ukweli na sio mwingine yoyote? Inawezekana wote wawili ni waongo vilevile. Nilitegemea ungejibu swali kwanza kabla ya kutuhumu kitu usichokijua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwa UJUHA Huu walioleta TRA ndio wanataka tuamini vitakwimu vyao wanavyotoa vya makusanyo! Ni MAJUHA tu watakubali huu UJUHA!
 
Hechinodemata watu wengi hawaelewi biashara za kimataifa, hasa linapokuja suala la "MNCs doing business in countries with inadequate institutions". Sasa wengi tunawashangaa mnaposema eti sisi ni wajinga tuache ili tuendelee kuibiwa.

Kwa ufupi ni kuwa, nchi nyingi ambazo MNCs zilienda kupiga hela na mikataba hiyo hiyo kama ya yule mjingaa mjingaa aliyesema MIGA, MNCs waliishia kupigwa faini na nchi zao, ila MNCs husika haziwezi kuja kama Tz zikasema zilishapigwa faini hivyo zinaogopa kufanya dili mbaya.

In short, wazungu, wahindi wanatumia sana udhaifu wetu waafrica ktk kufanikisha dili zao, na mara nyingi CEOs hupenda hizo loophole ili wapate bonus kibao na kuongeza CVs zao ili waje wapate pia mishahara mikubwa (wagombaniwe na makampuni mwengine). Mfano, CEO wa ACCACIA hawezi kukubali hili suala na ndiyo maana mpaka kamhonga lisu ili ajiokoe kwani ACCACIA ikilipa hiyo hela basi ujue kibarua chake kitaota nyasi na hatopata tena dili ya kazi kwani ataonekana ni CEO asiyekuwa makini).

In short kuna mambo mengi sana nyuma ya pazia, sisi werevu tunawashangaa sana ninyi msiotumia akili zenu, watu ambao hamuna hata exposure kushabikia mzungu. Na kwa ufupi mzungu anashangaa sana waafrica kwanini hatuendelei.
Huyo CEO atakuwa chizi kumhonga Lissu wakati he is no where near the decision making table of the country. Kwa taarifa yako huwa wanahonga decision makers kama wale wawili waliopita ambao makaburi yao hatuyafukui ng'o!!
 
Back
Top Bottom