Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) imegawa Mashine za kukusanyia mapato za Kieletroniki za EFD zipatazo tano kwa kila katibu Mkuu wa Wizara kwa ajili ya kuzitumia kukusanya maduhuli ya serikali.
Hatua hiyo imetokana na agizo la Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ya kutaka Wizara zinazotoa huduma ziwe na mashine za EFD ili kuweza kujiletea maendeleo na kukuza uchumi wa taifa. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata amesema kuwa ugawaji wa mashine hizo kwa taasisi za serikali zitasaidia kutunza kumbukumbu katika kupanga maduhuli.
Aidha amesema mashine hizo ni mashine za kwanza katika mashine zote kutokana na kuwa za kisasa katika kutunza kumbukumbu za huduma ambazo wanazitoa. Kamishna wa Mapato ya Ndani wa TRA, Ellijah Mwandumbya amesema kuwa watawafundisha wakuu wa idara hizo jinsi ya kuzitumia.