Katika kutafuta maisha mimi nimeshafanya biashara na mpaka sasa nafanya japo si kwa kiwango cha zamani. Labda niseme tatizo lipo kwenye UKUBWA WA KODI ambayo mfanyabiashara anatakiwa kulipa. Hili ni tatizo la muda mrefu lakini wafanyabiasha hawajawahi kulalamika kwa sababu miaka nenda miaka rudi wamekuwa wanakwepa kulipa kodi halisi. wafanyabiashara wengi kwenye maduka kama Kariakoo wanakuwa na vitabu viwili vya risiti, kimoja halali na kingine haramu. Sasa hizi mashine zimeziba huo mwanya, kwa hiyo watu sasa wanaanza ku-feel ile ''nguvu'' ya ukubwa wa kodi. Kusema ukweli sababu zinazotolewa na wafanya biashara zote ni za UONGO ila sababu kubwa ni kuwa UKILIPA KODI KADIRI INAVYOPASA faida itakuwa ndogo sana au hakuna kabisa. Naona wangeeleza tu ukweli na sio kuzunguka zunguka mbuyu