Yaani hii nchi sijui tulete malaika kutoka mbinguni aje aongoze, yaani kila idara ya serikali utendaji kazi ni wa hovyo hovyo tu. Road license yangu ilikuwa inaisha tar nane mwezi huu. Nimekwenda TRA kulipia tangu tar 8, wakachukua hela yangu wakanambia hawana sticker. Nikaambiwa niifuate tar 12 (jana), ilipofika tar tisa nikapaki gari (bahati nzuri ilikuwa weekend), tar 12 (yaani jana nimekwenda kuulizia sticker naambiwa hazipo, leo tena nimeenda kuulizia wananambia hazipo labda hadi keshokutwa. Nawauliza sasa nifanyeje na gari, wananijibu kwa kiburi kabisa eti nipaki. Na kwa bahati mbaya njiani wakati narudi kwenda home polisi wamenikamata na wamening'ang'ania hadi nimelipa faini. Hapa nilipo nina hasira mbaya. Laiti ningemwona mkurugenzi wa TRA karibu yangu ningeweza hata kumrushia jiwe. Inakera inakera inakera kupita kawaida.
Najuta kuwa Mtanzania mie.