TRA, tuwatumie Machinga kwa faida

TRA, tuwatumie Machinga kwa faida

getrusa

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2013
Posts
2,150
Reaction score
1,824
tunahitaji watu wanaowajibika kulijenga Taifa lao kwa namna yoyote, kwa muda mrefu sana tumekuwa tukiwaapuzia machinga kwa kuona kuwa ni watu wa haki ya chini.
Lakini ni ukweli usiopingika kuwa machinga wanaingiza pesa nyingi kuliko hata muuza duka aliyeko pale manzese Dar es salaam, watu hawa wanapanga bidhaa zao eneo ambalo ni "hot" linapitiwa na wateja muda wote,
Ninapendekeza TRA wawe na mfumo mzuri na rafiki wa kukusanya mapato toka kwa wafanyabiashara hawa.

Mfano kila mfanyabiashara (machinga) wale waliotandika chini akitoa tsh 2000 kila siku kwa kutumia EFD. Kwa eneo la kariakoo tu. Je tutapata tsh ngapi kwa siku..?
Kiwango cha kodi kinaweza kuwa kikubwa ama kidogo kutegemeana na mahali ambapo machinga huyu ameweka bidhaa yake. Mfano ili kukatisha tamaa uwekaji wa bidhaa pembezoni mwa barabara ni kuweka kiwango kikubwa cha kodi..
Ukiamua kupanga bidhaa barabarani kodi yako iwe kubwa kuliko ukiwa na duka.na ukiwa pembezoni mwa soko bei yako iwe kidogo,

Lakini pia TRA wanaweza kuchukua kodi ya chini sana hata tsh 500 tu kwa siku bado itakuwa ni pesa nyingi sana, nimepata hili wazo baada ya kumsikia yule mbunge aliyesema alihamasisha watu kujenga zahanati kwa tsh 1000.

Mimi binafsi naamini watu hawa wakitumika vema kwa njia rafiki wanaweza kuwa na mchango mkubwa sana kwa Taifa letu.
Nawasilisha..
20180919_125013.jpg
20180919_124002.jpg
 
Wazo zuri ilaulitakiwa ulilete kama mchumi ambaye abaifahamu sera ya kodi na namna mwananchi mmoja mmoja anavyoweza kuchangia uchumi.
Mm nasema hivi,serikali kupitia pato la taifa inawajibu kusaidia wananchi wake kuboresha maisha kwa kuweka mazingira rafiki ya kujenga maisha yao katika sekta mbalimbali za kiuchumi.
Mathalani wakulima ,serikaliimebakia kuwa na majina ya kimkakayi na sera mfu bila kuwasaidia wakuima hata kuwasaidia kupata masoko nalo tatizo.
Hili machinga nadhani ww mgeni Dar ,kulikuwa na mradi wa kujenhea machinga mazingiravmazuri yakuyanya biashara zenye tija.Je huu mradi umetekelezwa na kuleta mrejesho gani ulio na tija?
Si hoja ya kukimbilia kutoza kodi bali kwanza biresha biashara ziwe endelevu na zenye tija ndo utoze kodi.
Haiingii akilini unaanza kumkamua ng'ombe bila kumpa majani na vyakula vingine,hatatoa maziwa atayoa damu.
Na tujiulizechanzocha umachinga nini nn?na jeni biashara endelevu?jezinaweza kutoa ajira pana kwa waliowengi na ni kivipi?
Ukijibu maswali hayo ndo uje kutoza kodi. Tafakari na chukua hatua
 
Ndugu hoja yangu hapa ni ushiriki wa kila Mwananchi kutoa mchango wake katika ujenzi wa Taifa, tukianza kutoa sabbu katu haziwezi kuisha..
 
Huna elimu ya kodi; kwani mtu akitoa risiti ya EFD ya TZS 2000 kila siku serikali itapata nini?

Jibu ni kuwa serikali itapata sifuri. TZS 2,000 X 30 = 60,000 ambayo kiwango hiki hakilipiwi kodi hata hakistahili kuandikishwa kwenye VAT.

Muhimu kule anakonunua bidhaa zake adai risiti hapo serikali itapata mapato ya VAT na faida kwenye mauzo
 
Ndio maana nikasema kama kuna utaratibu unaoweza kufanyika ili hawa pia wachangie haiwezi kuwa vibaya.
 
Ndugu hoja yangu hapa ni ushiriki wa kila Mwananchi kutoa mchango wake katika ujenzi wa Taifa, tukianza kutoa sabbu katu haziwezi kuisha..
Mkuu unayo biashara yoyote ile ? Rasmi? Rasmi namaanisha imesajiliwa na kupitia taasisi zote ime Brela, TRA na Halmashauri, Au wewe ni mkaa ofisini huku ukiwa umevaa tai? Kwanza kabisa mashine za EFD zina category yake unapaswa uwe unazidi turn over ya 20 millioni ( kama wamebadilisha anaefahamu atakuja kurekebisha) pili huwezi anza kumtoza mtu kodi tu ili mradi sijui kuchangia uchumi wa nchi, tatizo linalofanya Tanzania isiendelee ni hili anaetunga sera hafanyi biashara hivyo hawezo elewa mazingira magumu ya kodi na ushuru kwa hapa Tanzania yalivyo
 
Back
Top Bottom