Jamal Akbar
JF-Expert Member
- Oct 9, 2014
- 413
- 471
Kwa kipindi kirefu sasa, nchi yetu imekuwa ikitumia mabavu ili kuwafanya wananchi walipe kodi hasa wafanyabiashara wakubwa. Wazungu wanasema ili kupata "compliance" linapokuja suala la kukusanya kodi sisi kama nchi tulichagua njia ya mabavu (Coercive means) na ndio maana mambo kama task force yamekuwa yakirindima hasa kipinidi kilichopita cha utawala.
Lakini kwa mujibu wa wataalamu mbalimbali, kuota zawadi (rewarding) ni njia mojawapo ya kupandisha morali ya kufanya kazi ili kupata matokeo chanya.
Katika pitapita zangu nimekutana na tangazo toka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mkoa wa kikodi wa Tegeta ambalo linawahamasisha wananchi kudai risiti baada ya manunuzi ili kupata nafasi ya kujishindia kati ya 250,000 mpaka 1,000,000 katika bahati nasibu itakayofanyika mwisho wa mwezi.
Hili ni jambo kubwa na la kuigwa na linaakisi maono ya Rais Samia ya kukusanya kodi bila mabavu, kwani kwa mwananchi kudai risiti tayari serikali inapata mapato stahiki katika muamala uliofanyika. Kutoka zama za kutegeana njiani Kariakoo kunyang'anya wafanyabiashara mizigo yao kwa kukosa risiti, kutoka kujibanza kwenye vituo vya mafuta kuwavizia wasio na risiti hadi kuweka mfumo wa wananchi kujishindia pesa taslimu kwa kuwa na risiti halali, hakika TRA_Tegeta wameonesha mfano unaopaswa kuigwa na nchi nzima.
Wananzengo ninyi mnaonaje hatua hii ya TRA-Tegeta ambayo pia itaongeza Database ya wateja, tujadili hapa.