TRA Tanga, nihurumieni jamani

TRA Tanga, nihurumieni jamani

Madam vivian original

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2018
Posts
503
Reaction score
998
Wakuu habari za weekend,

Aisee nimesota sana kulogin JF sijui kwanini imekuwa tabu sana kuingia imebidi nifungue I'd nyingine ili nipate kuwasiliana na marafiki zangu. Aiseee nimewamiss mno.

Turudi kwenye mada
Wakuu nimeamua kujichanga nimefungua biashara yangu ya salon ya kike, japo salon yenyewe ni ya kawaida sana, nina binti anajua kusuka sana nikaona ngoja nimuekee hata drayer moja, wakija wakuosha awe anawakausha.

Basi bwana nikasema ngoja niende TRA nikapate tin no, ndo kasheshe lilipoanzia wamenikadilia kodi kubwa na inabidi niilipe kabla ya tarehe 30 DEC.

Wakuu nimechanganyikiwa mpaka sasa sijapata hata mteja wa kuosha zaidi ya wale wanaosuka nywele za mkono.

Nawaza sijui nirudishe hiyo TIN no yao nifunge biashara maana watanifunga jamani.

Naomba ushauri nifanyaje jamani
 
Wakuu HV nikienda kuwaambia biashara imenishinda watanielewa kweli au bado watataka niwalipe nimekosa aman, hii nchi yetu jaman inakoendea mbona ....
Zote ni sawa tuu,
Unaweza emda waambia ivyo,
Sema wataanza kukufatilia ili wajue kama kweli ume acha.
 
Wakuu HV nikienda kuwaambia biashara imenishinda watanielewa kweli au bado watataka niwalipe nimekosa aman, hii nchi yetu jaman inakoendea mbona ....

Watakuelewa,ni juzi tu hapa wamewasamehe wafanyabiashara kibao ambao madeni yao yalionekana hayalipiki,So hata wewe ukienda ukawaelezea tatizo ni nini watakuelewa tu,kwani wamekuwa wakilaumiwa sana siku za hivi karibuni ya kuwa wanawabambikizia watu madai makubwa ya kodi na wao wanataka kuwaonyesha watu kuwa wanasikia kilio chao na wanabadilika,na ni bora ukaenda kuwaelezea shida zako kuliko ukikausha inaweza kuwa balaa kwako huko mbeleni.
 
Tutakoma mwaka huu

Sema ujue huez kimbia kodi Ndugu yangu,

Tatzo ni makadilio yanapo kua makubwa,

Kuna uzi mmoja humu unaelezea vzur ayo maswala ya kodi na hatua za kuchukua ukiona umeonewa, sa mimi sijui kudirect mtu ili ausome..

Sena nili uku copy nika usave kwa pdf format, ngoja nikuwekee io pdf
 
Attachments

ungeomba ushauri kabla ujaenda uko Tra saivi ungekuta unachekelea tu na sio kuuzunika
 
Wakuu HV nikienda kuwaambia biashara imenishinda watanielewa kweli au bado watataka niwalipe nimekosa aman, hii nchi yetu jaman inakoendea mbona ....
Nenda kafunge watakuelewa kiroho safi.. usipofanya hivyo hata ukikaa miaka 5 utakuja kukutana na likodi lishakuwa trillion 1.5
 
Kama ndo unaanza,unapewa Tin bure,kisha wanakuacha free miezi 3,
baada ya hapo ndo unaenda wanakukadiria,
usiende umevaa sijui wax la bei mbaya na usafiri wa nguvu,vaa katambuga zako vizuri kama enzi za mwalimu,nguo ziwe za upaukwe na ukifiga body language yako iwe ya kimasikini masikini sana,
watakukadiria hata elfu hamsini kwa robo mwaka,
kama hata hiyo inakushinda basi urudi ulime,
pia pengine ulikosea kujaza fomu panapokuuliza unatarajia kupata kiasi gani kwa mwaka,kama ulijaza above milioni 4,it has eaten to you...(imekula kwako)
 
Mi nimewaandikia barua kuwa nimefunga business ...nimeambiwa nikachukue majibu, full uvivu yaan
 
Kama ndo unaanza,unapewa Tin bure,kisha wanakuacha free miezi 3,
baada ya hapo ndo unaenda wanakukadiria,
usiende umevaa sijui wax la bei mbaya na usafiri wa nguvu,vaa katambuga zako vizuri kama enzi za mwalimu,nguo ziwe za upaukwe na ukifiga body language yako iwe ya kimasikini masikini sana,
watakukadiria hata elfu hamsini kwa robo mwaka,
kama hata hiyo inakushinda basi urudi ulime,
pia pengine ulikosea kujaza fomu panapokuuliza unatarajia kupata kiasi gani kwa mwaka,kama ulijaza above milioni 4,it has eaten to you...(imekula kwako)
Yaani wanenipa tin, alafu wakaniambia nikalipe asilimia 10, ya Kofi yangu ya mwaka mzima. Nikalipa elfu hamsini hapo hata cjafungua, nikamwambia ndugu yangu cjaanza hata biashara yenyewe hii pesa mliyonikadilia ntaitoa wapi?, wakasema Dada hiyo ndo kima cha chini kwa wenye biashara ndogo. Niliondoka TRA huku machozi yananitoka nikakaa home siku3 sijafungua nawaza nifanyaje alafu nilipo nisehemu ambayo haijachangamka kabisaaaa.
 
Watakuelewa,ni juzi tu hapa wamewasamehe wafanyabiashara kibao ambao madeni yao yalionekana hayalipiki,So hata wewe ukienda ukawaelezea tatizo ni nini watakuelewa tu,kwani wamekuwa wakilaumiwa sana siku za hivi karibuni ya kuwa wanawabambikizia watu madai makubwa ya kodi na wao wanataka kuwaonyesha watu kuwa wanasikia kilio chao na wanabadilika,na ni bora ukaenda kuwaelezea shida zako kuliko ukikausha inaweza kuwa balaa kwako huko mbeleni.
Kwani ukifunga biashara ukaanza kuuza vitumbua watakuja kukuuliza...watakupatia wapi...
 
Yangu nilipoona inazingua nikaifunga sikwenda hata kureport. Baada ya miaka mi3 nikajua ntakuwa na deni kubwa nilipo angalia details zangu hakukuwa na deni. Nilishukuru sana kimoyomoyo
 
Back
Top Bottom