TRA, TAKUKURU wamtaja anayeiba mil7-8 kila dakika, huyu hapa..

Hivi Takukuru waliokuwapo katika utawala uliopita na TRA kwanini W asipangwe mstari wakanyongwa hadharani hicho kizazi kikapita? je JPM atafanya @ Jambo peke yake ataweza? police iruhusu tuandamane kuunga mkono Raisi watu hawa wanyongwe ni majambazi no 2.
Kweli
 
Kaka Magufuri alipata 58% hii ina maana wataomwelewa Magufuri ni 58% na 42% hawatamwelewa na ndio hawa vichwa mkuki na Magufuri amesema wale ambao hawataendana na kasi yake wataisoma namba ndio hao 42% na hii ina maana 42% wameshindwa kwenda na na kasi ya JPM ndio hao wanaolalamika
Kama ni 42% mbona hata mimi kila mtu humu anajua nilimuunga mkono Lowassa? na wasichoelewa hawa wanaomtukana Magufuli dikteta ni kwamba hata Lowassa tulimpendea hizo elements za kidikteta maana tulipokuwa tumefikia tulihitaji mtu wa aina ile, kama wanamaanisha Lowassa hana tena hizo elements basi wasisimamishe hata mgombea 2020 wajue watz tunahitaji mtu wa aina hii na tumelidhika kabisa mambo yanaenda.
 
Niliwahi kwenda ifisini kwake nihitaji kuonana naye. Pale mapokezi waliniambia ni mtu mwenye dharau sana hibyo hata sitoweza kuongea naye. Nikaishia kuondoka.

Nawewe ukakubali bila ya kuthibitisha Kama kweli Huyo mtu anadharau?.Duh Hii Ni hatari
 
Kwa namna hii uchumi wa nchi lazima ukue kwa double digit by next year.. Lazima tuvunje record kwa ukuaji wa uchumi.
Hakuna cha uchumi au ukuni kukua Tanzani,yote hayo ni maigizo tu,watu wameisha chukua pesa na hawarudishi hata senti,hiyo ni changa la macho,watahonga katika pesa hizo hizo tu na wataendelea kupeta,huo ni mtandao mrefu sana unahusisha na MA MUHESHIMIWA,kama unabisha subiri muda tu hii issue hutaisikia tena na itatupwa kando halafu tunasonga mbele na wimbo wa KUTUMBU MAJIPU kwa kukurupuka baaaaaaaasi.Watakao endelea kufilisiwa na kufikishwa mahakamani ni wafanya biashara wa Mbagala na tandale kwa mfuga nguruwe na wengine kama hao baaasi
 
Mohamed Murtaza Yusuph Alli ni mtu aliye katika tuhuma nzito kabisa za ufisadi kuwahi kutokea nchini.
KWA UFUPI
Mtandao wa huyu jamaa ulijumuisha wafanyakazi wa mamlaka ya mapato,wakala wa usajili wa biashara na leseni(BRELA)
ALIZALISHA RISITI
Kamishina mkuu TRA alisema kwa kutumia mashine za EFDs zilizo nje ya mfumo wa TRA Alli alizalisha risiti za mauzo na kuziuza kwa kampuni 300 bila zenyewe kufanya biashara.
Alikuwa akiuza risiti za EFD kwa bei ya 5% ya kodi,baada ya kuzinunua kwa bei ndogo kampuni hizo zilienda kudai marejesho ya 18% kamili TRA hivyo kuuibia serikali.
Kwa mchezo huo kampuni hizo zilishirikiana na Alli kukwepa kodi kwa kupewa risiti feki zinazojumuisha VAT na kodi ya mapato.
Mkurugenzi mkuu wa Takukuru alisema kampuni hizo zimepewa hadi julai 7 ziwe zimekamilisha kulipa malipo hayo.
MATRILIONI
Akizungumza katika hafla ya kuwaapisha wakuu wa wilaya JPM alisema mamlaka inamshikila kinara wa aliyekuwa akichakachua mashine hizo na hivyo kuisababishia serikali hasara ya matrilioni ya shilingi "tumepoteza matrilioni ya shilingi na alikuwa anashirikiana na TRA na Brela.Bahati nzuri yuko kwenye mikono salama.Hiyo ndo Tanzania"alisema JPM.
Chanzo: NIPASHE

Magufuli alipokuwa anawaambia waandishi wa habari kuwa wamambaini mtu huyo na kumuweka mikono salama
 
1467443808822.jpg
Mohamed Murtaza Yusuph Alli ni mtu aliye katika tuhuma nzito kabisa za ufisadi kuwahi kutokea nchini.
KWA UFUPI
Mtandao wa huyu jamaa ulijumuisha wafanyakazi wa mamlaka ya mapato,wakala wa usajili wa biashara na leseni(BRELA)
ALIZALISHA RISITI
Kamishina mkuu TRA alisema kwa kutumia mashine za EFDs zilizo nje ya mfumo wa TRA Alli alizalisha risiti za mauzo na kuziuza kwa kampuni 300 bila zenyewe kufanya biashara.
Alikuwa akiuza risiti za EFD kwa bei ya 5% ya kodi,baada ya kuzinunua kwa bei ndogo kampuni hizo zilienda kudai marejesho ya 18% kamili TRA hivyo kuuibia serikali.
Kwa mchezo huo kampuni hizo zilishirikiana na Alli kukwepa kodi kwa kupewa risiti feki zinazojumuisha VAT na kodi ya mapato.
Mkurugenzi mkuu wa Takukuru alisema kampuni hizo zimepewa hadi julai 7 ziwe zimekamilisha kulipa malipo hayo.
MATRILIONI
Akizungumza katika hafla ya kuwaapisha wakuu wa wilaya JPM alisema mamlaka inamshikila kinara wa aliyekuwa akichakachua mashine hizo na hivyo kuisababishia serikali hasara ya matrilioni ya shilingi "tumepoteza matrilioni ya shilingi na alikuwa anashirikiana na TRA na Brela.Bahati nzuri yuko kwenye mikono salama.Hiyo ndo Tanzania"alisema JPM.
Chanzo NIPASHE

Huyo ndo Mohamed murtaza aka Farmplant owner now inajulikana kama tough supplies ipi sukuma road
 
Hizo Trillioni akirudisha mjenge Viwanda, acheni kulipa StarTV na TBC kutumia TV zao wakati wa Kampeni zenu.
 
....huyo Ally sawa alipishwe pesa zetu,lakini hata washirika wake wasiachwe nao wakamatwe!, kuhangaika na huyo Ally peke yake ni sawa na kuhangaika na kipele cha cancer,wakati cancer yenyewe imeshasambaa mwili mzima.

Watumbuliwe wote!
 
Trilioni ngapi nataka takuukuru waje na data kamili halafu tujue na hayo makampuni yaliyokwepa .na nyongeza tunataka hao watu warudishe hayo matrilioni tujengee reli ya standard gage
 
Waongoooooooo
Hahahaaaa mnatafuta kik
Kinguvuuuuuuu tumeshawajua tafuteni story nyingine
 
Nyuma ya alli na farm plant ltd yake na mchezo huu wote kuna watu hawajatajwa bado na ambao walishawekwa kwenye mikono salama, alli ni mbuzi wa kafara!
 
this might be cooked scandal to swallow Tundu Lissu and Ukawa issues perse
 
hakuibia nchi kias hicho milioni 7 kwa dakika magufuli alikuza sana ili kupata attention kubwa zaidi, na alikuwa haibi milioni saba kama hela alikuwa anatengeneza risiti za mauzo zenye thamani hiyo kisha anawauzia watu ambao huonekana wamefanya manunuzi feki hivyo kulipa VAT ndogo au kutolipa kabisa,
kwa hiyo pesa aliyokuwa anaiibia serikali kwa dakika hizo anazodai Magufuli ni 18% x 7,000,000= 1,260,000
ila yeye alikuwa hapati hiyo 1,260,000 alikuwa analipwa 5% ya hiyo amount kutoka kwa wafanya biashara waliokuwa wananunua hizo risiti kwa 5% ya ile 18% waliokuwa walipe

ambayo ni 5% X 1,260,000=630,000
 
Back
Top Bottom