TRA ni SHIDA: Wavamia Ofisi hapa Viwandani

Mwingereza

JF-Expert Member
Jan 21, 2014
944
1,000
Ninaambiwa kila siku TRA ni majambazi sijawahi kuamini. Leo wamevamia Kampuni moja hapa ITV, nimeshtushwa. Wameingia kama Majambazi na kufunga geti, wametoka na nyaraka pamoja na computer mpakato 4. Lengo sijui ni nini, ila hii inaogopesha sana.

Hatuji tunaelekea wapi. TRA ni hida. Mama inabidi ushugulikie hii taasisi, wanajiona miungu watu. Something must be done. Makapuni yanakamuliwa ipasavyo
 

mtanzania1989

JF-Expert Member
May 20, 2010
3,725
2,000
Wafanyabiashara Tanzania hawataki kulipa kodi halali, na matamshi yakukurupuka ya SSH yamewapa kibri cha kukataa kulipa kodi halali kwa uwazi kabisa, TRA wafanye nini kwa mtu anayekataa kulipa kodi kwa uwazi kabisa? SSH is naive na anaenda kuleta mgogoro mkubwa wa TRA kwa sababu akili finyu.
 

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,532
2,000
mtanzania1989

Wewe unaona walichokuwa wanafanya TRA ndiyo sahihi, wakati Wa utawala wa mwendazake?

Mimi naunga mkono kauli ya Rais wetu, mama Samia Suluhu Hassan, aliyowaambia hao TRA kuwa wadai kodi kwa ustaatabu na siyo kwa kutumia mabavu.

Hivi unaona njia za kufunga account za wafanyibiashara ndiyo sahihi?

Sasa ukishafunga account ya mfanyibiadhara huyo, hivi hiyo kodi utaendekea kuipata?

Inabidi hao TRA watumie akili kidogo na siyo kutumia mabavu, ambayo ndiyo ilikuwa msingi wa ufanyaji kazi chini ya utawala wa mwendazake!
 

Mafuluto

JF-Expert Member
Aug 25, 2009
1,867
2,000
Ingawa mm pia ni muumini wa ustaarab, hii taarifa haijakaa sawa. Toa details zaidi maana wabongo tunajuana.

Hakuna mtu mwehu au mjinga avamie tu, na kuondoka na laptops.

Sera ya Mama haimaanishi husilipe kodi, au wao TRA wakae tu ili ukijisikia ndo ukalipe.

Kama unadaiwa, na sasa wanatoa sana demand notice basi nenda kawasikilize!
 

TASK FORCE

JF-Expert Member
Apr 7, 2017
2,423
2,000
Wafanyabiashara Tz hawataki kulipa kodi halali, na matamshi yakukurupuka ya SSH yamewapa kibri cha kukataa kulipa kodi halali kwa uwazi kabisa, TRA wafanye nini kwa mtu anayekataa kulipa kodi kwa uwazi kabisa? SSH is naive na anaenda kuleta mgogoro mkubwa wa TRA kwa sababu akili finyu.
yaani we kenge unamuita Rais akili finyu? Moderator
 

Champagnee

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
5,771
2,000
Kama wameacha document inayoonyesha wamechukua hizo computa bhs ni halali kama hawaacha documents wameiba. TRA wanaruhusiwa kifanya inspection kama watahisi kuna kodi inakwepwa.

Ila tuwe wa kweli wa Tz hatuna moyo wa kulipa kodi, last week nimeenda kununua nguo kariakoo za thamani ya 420,000 kwa dada mmoja hv. Nimeomba risiti akawa mgum kutoa ile kukomaaa akanipa ya laki1 akasema ya njiani, nikamwuliza kwanini unafanya hivo si nmekupa cash taslimu kwanini usinipe risit yangu niende?

Akawa hana point bhs tu yan anaona kutotoa risit ni kama ujanja hivi, baada ya kukomaa sana nikamwambia napiga simu TRA waje ndo akatoa risit ya amount ilobaki.

Kweli nikaamini wafanya biashara ndo wanashida na sio TRA. Imagine mtu anagoma kukupa risit na umelipa cash akipewa adhabu analalamika.
 

TASK FORCE

JF-Expert Member
Apr 7, 2017
2,423
2,000
Ninaambiwa kila siku TRA ni majambazi sijawahi kuamini. Leo wamevamia Kampuni moja hapa ITV, nimeshtushwa. Wameingia kama Majambazi na kufunga geti, wametoka na nyaraka pamoja na computer mpakato 4. Lengo sijui ni nini, ila hii inaogopesha sana.

Hatuji tunaelekea wapi. TRA ni hida. Mama inabidi ushugulikie hii taasisi, wanajiona miungu watu. Something must be done. Makapuni yanakamuliwa ipasavyo
Kwaiyo Kama wamekwepa Kodi ulitaka TRA wasiende kufanya ukaguzi
 

Detective J

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
13,716
2,000
Wafanyabiashara Tz hawataki kulipa kodi halali, na matamshi yakukurupuka ya SSH yamewapa kibri cha kukataa kulipa kodi halali kwa uwazi kabisa, TRA wafanye nini kwa mtu anayekataa kulipa kodi kwa uwazi kabisa? SSH is naive na anaenda kuleta mgogoro mkubwa wa TRA kwa sababu akili finyu.
Acha upotoshaji. eti matamko yamefanya mfanya biashara asilipe kodi. toka lini?

Kodi iko kisheria sio tamko la rais?

Wala rais hakusema watu wasilipe kodi.
 

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
117,307
2,000
TRA kumejaa wahuni na majambazi kama polisiccm, takukuru na mahakama.
Ninaambiwa kila siku TRA ni majambazi sijawahi kuamini. Leo wamevamia Kampuni moja hapa ITV, nimeshtushwa. Wameingia kama Majambazi na kufunga geti, wametoka na nyaraka pamoja na computer mpakato 4. Lengo sijui ni nini, ila hii inaogopesha sana.


Hatuji tunaelekea wapi. TRA ni hida. Mama inabidi ushugulikie hii taasisi, wanajiona miungu watu. Something must be done. Makapuni yanakamuliwa ipasavyo
 

KikulachoChako

JF-Expert Member
Jul 21, 2013
16,280
2,000
Ingawa TRA approach yao ni ya kibabe lakini sisi waTanzania tunajulikana hatuna utaratibu wa kufanya mambo kwa hiyari, kama uliwahi hata mkusanya ushuru wa soko utaelewa hili. Ku deal na waTanzania ni kipawa sana.

Alafu mtu ambaye anajijua ni mkwepaji mkubwa wa kodi unakuta analalamikia huduma duni na miundominu mibovu.
 

DidYouKnow

JF-Expert Member
Jul 28, 2019
680
1,000
Ninaambiwa kila siku TRA ni majambazi sijawahi kuamini. Leo wamevamia Kampuni moja hapa ITV, nimeshtushwa. Wameingia kama Majambazi na kufunga geti, wametoka na nyaraka pamoja na computer mpakato 4. Lengo sijui ni nini, ila hii inaogopesha sana...
Sasa hawa TRA tunawaonea. Wakiwa wapole tunasema Mama SSH hawa jamaa wanakuangusha, wakija kininja tunawaita majambazi.
 

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
11,576
2,000
mtanzania1989
Wewe unaona walichokuwa wanafanya TRA ndiyo sahihi, wakati Wa utawala wa mwendazake?...
Kodi huwa haidaiwi kwa kumwomba mlipa kodi alipe kadri anavyotaka, inadaiwa kwa kufuata sheria za kodi zilizopo. Maafisa wa kodi wanaotumia madaraka yao vibaya wasiwe kisingizio cha kuacha kutumia sheria zilizomo vitabuni; hao maafisa watafutwe na washughulikiwe kwa mujibu wa sheria lakini sheria ya kodi ibaki pale pale.

Waliokaa nchi za wenzetu walioendelea nadhani watagundua kuwa kwa kwenye ulipaji kodi serikali huwa haibembelezi kabisa. Pamoja na kukufunga, wanaweza kukamata account zako za benki na vile vile wanaweza kusimamisha mshahara wako uwe unaingia serikalini moja kwa moja kulipia deni ulilokwepa.

Mwulizeni mwenzenu Wesley Snipes au Lauryn Hill au Chuck Berry waliopelekwa kunakohusika kwa mapumziko marefu kwa sababu ya kukwepa kodi.

By nature, serikali ni chombo cha mabavu; serikali inayofanya kazi kwa kubembeleza siyo serikali, bali ni chama cha siasa.
 

fasiliteta

JF-Expert Member
Jul 2, 2014
1,726
2,000
Kama wameacha document inayoonyesha wamechukua hizo computa bhs ni halali kama hawaacha documents wameiba. TRA wanaruhusiwa kifanya inspection kama watahisi kuna kodi inakwepwa...
Nimenunua simu juzi nikadai reset,jamaa wa pembeni akammaindi mwenzie eti awaulize wateja kwanza kama ni jumla au rejareja,kwa madai nimeuziwa jumla kwa simu moja hivyo no reset,tena kwa kuvimba kabisaaa na kakasirika hatari mpaka nimeogopa.

Sa hivi wanaeza hata kukudunda kudai reset, Nafikiri mama awe Makini hii sekta ya kukusanya kodi kwa nchi changa kama TZ isiyo na mifumo madhubuti ya ukusanyaji kodi inataka ujitoe akili kidogo ndo upate kodi,akicheza na nyani atavuna mabua.Yeye nia yake nzuri ila wafanya biashara hawajawahi kua na nia nzuri zaidi ya kujineemesha wao tu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom