Wafanyakazi wa TRA wako wengi,kuna walioingia kwa migongo ya vigogo(although ni ngum kudhibitisha) na walioingia haki bin haki.
Kwahiyo walio wengi pale wachagga na pia weshapenyezwa. Hahaaa..Duh hata wanaume wanapenyezana ? Basi hata hiyo kazi sitaki..
Huenda hii ya kuingizwa mingongoni na mwa vigogo ikawa ina ukweli ndani yake, Masanilo anasema( wanapenyezwa), kwani si dhani wale vijana wa Longroom wana tumia Elimu zao.
Najua si neno sahihi (wale jamaa ni wajinga) reasoning yao duuuuu
Sasa mkuu kimemo tu bila chochote kitu utakipewa na nani ?
Tafuta urafiki na akina Lowassa ama mzee wa standard and speed.....hapo lazima upate kazi!
Mkuu mimi hao watu huwa nawaona tu kwa mbali wakipita kwenye motokaa, Hata uwezo wa kusalimiana nao sina. Ila vyeti vyenye kukidhi qualifications za longroom natumaini ninavyo.
Inategemea wewe ni nani katika nji hii! Ajira za TRA lazima upelekwe na mtu na ukweli ndio huo!
Pia lazima hata ukipelekwa na mtu utaanzia Mtwara
then utaamishiwa Kigoma utapelekwa Musoma
halafu ndio utarudi Dar hapo chumba-kirefu!
Ina ogopesha.. TRA hakuna sheria za mapato ambazo zinafanya kazi. Jitu likiamkia kwenye supu ya utumbo likifika pale linaweka bei yoyote ya ushuru. Halafu hawa watu wana kiburi fulani.
hili suala kwa kweli linatakiwa kuangaliwa kwa makini,ukitaka balaa import kitu ambacho hawajawahi kukiona wala kukisikia,kwanza hawajui hata wapi wakatafute detail sasa utaletewa bei yao ya ajabu ambayo inaweza kukupa nafuu ya ajabu au hasara ya ajabu.kwa kweli kama alivyosema MASANILO reasoning yao duuhh.
Najua si neno sahihi (wale jamaa ni wajinga) reasoning yao duuuuu
Hivi tuna kwenda wapi na hali ya jinsi hii ? Huku ni kudumaza uchumi wa nchi, Kwasababu sasa kwanza watu wataogopa hata kuingiza bidhaa nchini na matokeo yake bei za vitu zitakuwa juu sana. Sitegemei kuona mtu kalipia ushuru wa milioni 7 au 9 kwenye Toyota Mark II aje kukuuzia gari hiyo kwa milioni 10.
Kama TRA wataendeleza hali hii ya ajabu ajabu ya kubuni bei za vitu ambavyo tayari vimesha lipiwa na document original zikaonyesha malipo halali, Itatokea kuwaumiza wananchi walio maskini.
Hawa jamaa wa TRA wameanzisha tabia moja mbaya sana, Ambayo kama itaendelea hivyo itakuja kutuletea madhara makubwa japo kwa sasa tulio wengi hatujaweza kulitambua hilo.
Ina shangaza sana kuona Mtanzania mwenzio anakuja kukupangia bei ya kitu ambacho ulishalipia nje ya nchi na kukithamanisha kwa bei anayo taka yeye . Huu ni utaratibu gani ? Let say mtu ananunua Plasma TV yake nje ya nchi kwa ml 2 na risiti au invoice aliyofanyia malipo anayo, wewe unakuja kupanga bei kwenye TV hiyo mfano Ml 3 au hata laki 3.
Huu utaratibu wanaofanya hawa jamaa sio mzuri, Huku ni kuwakomoa watanzania walio wengi. Hata kama ni kukusanya kodi, watu hawakusanyi kodi kwa utaratibu wa namna hii. Ni heri basi ikawekwa bayana kwamba unapo nunua kitu nje ya nchi na kukiingiza Tanzania mnakipa bei ingine tofauti na ile mtu anayo nunulia.