TRA na promosheni za kampuni za simu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TRA na promosheni za kampuni za simu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by commonmwananchi, Mar 26, 2011.

 1. commonmwananchi

  commonmwananchi JF-Expert Member

  #1
  Mar 26, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 2,145
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 180
  Kumekuwa na promo nyingi toka kampuni za simu na nyingine ni kuwauzia wateja ringtones za miito.

  Hii ni tofauti na mauzo yaliyo wazi kama mauzo ya airtime, na hata simu za makampuni husika ambapo walau TRA wanaweza kuweka angalizo, kwa wastani biashara hii ni kubwa mno hasa hapa kwetu ambapo kiwango cha umiliki simu za viganjani ni mkubwa.

  JE? Kodi ya mauzo ya Ringtones na promotion mbalimbali tunazotangaziwa kila ukicha mbona TRA hawatutangazii ni kiasi gani serikali inapata au ni ufisadi mwingine huu?
   
 2. C

  CHESEA INGINE Senior Member

  #2
  Mar 26, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 180
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hawana misamaha ya kodi hawa? Maan kwa huruma tanzania ndiyo yenyewe!
   
 3. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #3
  Mar 26, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,948
  Likes Received: 1,274
  Trophy Points: 280
  Kweli we Great Thinker
   
 4. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #4
  Mar 26, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,483
  Likes Received: 5,570
  Trophy Points: 280
  Mkuu ni swali zuri, pamekuwa na tatizo kwa muda mrefu kwa tra ku establish tax base pamoja na mbinu za wawekezaji hasa kitechnologia sambamba na tra ambao walikuwa nyuma sana kimbinu.mfano wa makampuni tata wa mfumo wa kulipa kodi kwa shughuli zao hasa wakitumia mwavuli wa technologia ni Dstv nafikiri kodi katika sophificated technology ya ulimwengu wa sasa inaitaji iundwe kitengo maalum kitachoweza kudeal na this situation hasa wenye ufahamu wa kutosha wa kodi na technologia.
   
 5. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #5
  Mar 26, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,483
  Likes Received: 5,570
  Trophy Points: 280
  tra wamebuni njia mpya za kukusanya mapato kwa mabadiliko ya income tax upande wa withholding tax na ujio wa machine zinazotoa receipt kwa kila mauzo lakini utaona pia upande wa wakwepa kodi kitechnology ni wengi mno.wanaotengeneza sera pale tra ni watu wanaofahamu vizuri mambo ya kodi lakini bado nahofu na jinsi ukwepaji wa kodi kwa technologia umepatiwa mwarobaini.
   
 6. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #6
  Mar 26, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,483
  Likes Received: 5,570
  Trophy Points: 280
  mfumo wa kodi unachangamoto sana, VAT na withholding tax kwa sasa vitazidisha hali kuwa mbaya sababu ya matumizi ya serikali yasiyo na priorities.
   
Loading...