TRA na mfumo mpya wa kufanya valuation of Used Vehicles

Wakuu katika hangaika hangaika za kimaisha imetokea mzee wangu alipata ajali akiwa safarini kutokea Arusha kwenda Dar na hivyo kupata structural disorder kwenye mgongo. Shughuli zote za kiuchumi za mzee zimesimama kwa zaidi ya miaka 4 sasa. Baada ya kuhangaika sana na matibabu kushindikana nikaamua niingie benki na kukopa Tsh. 8 milion ili nimuagizie gari la kumpeleka hospitali kwenye mazoezi na kumrudisha nyumbani kwa sababu gharama za teksi nilikuwa naelekea kushindwa kuzimudu.

Baada ya kufanya research kwa ndugu na jamaa waliokwisha kuagiza magari, nikaambiwa ukinunua gari CIF atmost USD 2500 pamoja na kodi haitozidi shilingi mil 7.5 (yaani USD 2500*1500 plus 70% covering taxes & clearing charges). So nikajua nikichukua loan ya sh. 8 milioni ingetosha gharama zote mpaka angalau third party insurance.

Nikapata gari kwa CIF USD 2380 (cresta ya mwaka 2000).

Cha ajabu leo hii nimepata gharama halisi ya kulipa kama kodi ni USD 4700 (kodi tu) sawa na shilingi milioni 7.2. Jamani huu si ni uuaji.

gari nimelipia |CIF 3,700,000 lakini kodi nalipa milioni 7.2?

Naombeni ushauri wakuu, nafikiria kulisusa gari hilo kwa sababu sina hela ya kulipia hayo mamilioni.
 
Brooklyn huu mpango wengi wanalalamika lakini wako watu wanalipa utaratibu mpya wa ukadiriaji wa kodi kwa magari yaliyotumika ni mzigo kwa mtanzania wa kawaida. Bila kuungana tutaendelea kulipa zaidi.
 
... (cresta ya mwaka 2000).....
Nadhani hapo ndio tatizo lako lilipoanzia! Magari yenye zaidi ya miaka kumi tnagia kutengenezwa yanalipiwa kodi zaidi kama 'adhabu' kwa kuingiza nnchini gari chakavu!
 
Mzee mzima pole na matatizo. Hili suala limeshaongelewa hapa jamvini sana tu watu tumetukana mpaka matusi yameisha, tumefura ghadhabu mpaka tumeshidwa kunywa maji.
 
hii ni sawa na ina maana kuwa katika kusubmitt documents haina haja ya msururu wa nyaraka bali Bill of Lading pekee kuonyesha kuwa unaingiza mzigo nchini, bei haihusiani tena na seller bali TRA! (this is only in TZ!!!)
Cha msingi hapa tangazo hili liendane na tangazo lingine la Tanzania kujitoa uanachama wa World Trade Organization (WTO) ili ijulikane sisi ni watu wa "ki JK JK" na "Kimkullo mkullo"

Mkuu upo sahihi kabisa maana invoice haina maana tena bei wanazo
 
Hili swala kila mtu analipigia kelele, ni kweli watu walishalijadili na mpaka kufikia kutukana... TRA Imeamua kuumiza raisa wasio na uwezo.
 
Exactly!! Sasa kinachotisha ni kwamba je tuna viongozi na wataalamu ambao ni critical na great thinkers??? mhhhhh!! wajua hata England pamoja na kuwa ktk EEC nayo pia imetofautiana na members ktk baadhi ya vitu mfano hiyo currency Euro vs Pound sababu waliona haina manufaa kwao kubadilisha. Sasa linchi ambalo limeoza kama TZ we are lacking those thinkers to challenge and be critical! watu wameweka sana politics mbele! hakuna researches na wanajifanyia tu kuholela.

Mkuu nimesoma mahali wanasema kitengo cha research kipo..ila kuna mwingine amesema hii taxation system inaweza kuwa imekubaliwa kwa nchi zote za EAC, huku kufuata mkumbo ni hatari sana.

New and used cars are inexpensive; car ownership fees and fuel levies are used to promote energy efficiency. However, at just 50 percent of all distance traveled, car usage is the lowest of all G8 countries.

Hii sentensi nimeitoa kutoka wikipedia kuhusu Japan, (bahti mbaya link yake imeshindwa kufunguka) hawa ndio mabwana magari wa kuaminika ktk sayari hii. Pamoja na kuwa na barabara za kutosha na matreni bora kabisa bado wanauza magari kwa bei ya chini hata yale yaliyotumika ambapo hata akina sisi ndio tunapoponea..Usafiri bora wa umma umewawezesha hata watu wasitumie magari yao kwa asilimia 50%. Sasa sisi ambao hatuna viwanda vya magari, hatuna usafiiri wa maana wa umma, hatuna matreni, hatuna lolote la maana, bado tunajitia kiherehere cha kuongeza gharama za upatikanaji magari. This insane.
 
Ninanvyojua Masuala ya hizi kodi yapo kwenye Income Tax Act ya mwaka 2004, na inazungumza kama ilivyokua mwanzo, je waziri au kamsihna ana uwezo gani wa kubadilisha sheria bila kupitia bungeni ilikoanzia?
 
Hivi hatuna vyombo nchini vya kudhibiti huu utungaji na ubadilishaji sheria kiholela? Najijibu mwenyewe, si ni walewale tu!
Na mfumo huu mpya wa ushuru ukija kurekebishwa, wale watakaokuwa tayari wamelipa si itakuwa tayari imekula kwao?
Kuna siku naona aibu kuwa mtanzania, kama leo.
 
Kama ni hivyo basi tunakufa kwa kifo cha mende. Hivi wataalamu wetu uchwara wanashindwa kupata mapato halali mbadala bila ya kumwumiza mlalahoi na mikweche yao..mathalani serikali inashindwaje kuanza kutoza kodi kwa mishahara na posho za wabunge ili kudumisha haki na usawa ktk jamii. Iweje akina mama ntilie wanakabiliwa na tozo mbalimbali licha ya kipato chao kuwa cha kuganga njaa tu. Ama iweje watumishi wa serikali wajiwekee mabilioni katika posho ( karibu robo ya bajeti nzima), badala ya fedha hizo kuelekezwa katika sekta nyeti zinazolenga kuwatatulia matatizo ya kijamii wananchi???? Kwa hilo nasema HAPANA inatosha.

Mkuu ni kweli huu utaratibu mpya utafanya watu wenye vipato vya kati kushindwa kumudu kuagiza magari.
Ila hapo kwenye nyekundu napingana na wewe, sidhani kama kuna mlalahoi anaeweza kununua hata Tata Nano!! Huyo atakua mlalahai na si mlalahoi.

Nadhani hapo ndio tatizo lako lilipoanzia! Magari yenye zaidi ya miaka kumi tangia kutengenezwa yanalipiwa kodi zaidi kama 'adhabu' kwa kuingiza nnchini gari chakavu!

Siyo adhabu mkuu...ni mambo ya environmental accountability!!!
 
Siyo adhabu mkuu...ni mambo ya environmental accountability!!!
Environmental accountability ningeielewa zaidi kama ingekuwapo sheria kabisa kwamba hakuna kuingiza gari la zaidi ya miaka kumi (jirani zetu Kenya miaka nane mwisho, source website ya KRA)...
Ningeivumilia pia hiyo environmental accountability hiyo kodi ya uchakavu ingeenda kutumika kwenye project zinazoendana na kuboresha mazingira. Na kwa mfumo wa sasa 75% depreciation kwenye magari ya miaka 10 na zaidi, Tanganyika yetu sasa litakuwa jalala kwa kwenda mbele; pamoja na kodi ya uchakavu bado kwa baadhi ya magari unakuwa na nafuu kuagiza gari nzee kuliku umri wa kati au jipya.
 
Wakuu naombeni msaada wenu kuhusu hili, naamini kuna mwenye idea, gari yangu inaingia july mwanzoni bandarini dar na nimejaribu kuitafuta kwenye ile excel sheet ya TRA yenye kuonyesha CRSP (bei za kununulia ikiwa mpya) haijaorodheshwa hiyo modeli, ni Subaru Forester GF-SF5 4wd modeli ambayo ndio nyingi mtaani, wanaonyesha SG5 na nyinginezo pekee, sasa mwenye wazo kwamba case kama hii wanai-treat namna gani pls anijuze. Jamani kwa kifupi TRA wametunyongelea mbali, mtu umejiandaa kwa gharama za kawaida unakuja kuambiwa mara mbili yake..!!!! duuh, si ndio mwanzo wa kuacha gari liozee huko.. msaada tafadhalini jamani..
 
Wakuu katika hangaika hangaika za kimaisha imetokea mzee wangu alipata ajali akiwa safarini kutokea Arusha kwenda Dar na hivyo kupata structural disorder kwenye mgongo. Shughuli zote za kiuchumi za mzee zimesimama kwa zaidi ya miaka 4 sasa. Baada ya kuhangaika sana na matibabu kushindikana nikaamua niingie benki na kukopa Tsh. 8 milion ili nimuagizie gari la kumpeleka hospitali kwenye mazoezi na kumrudisha nyumbani kwa sababu gharama za teksi nilikuwa naelekea kushindwa kuzimudu.

Baada ya kufanya research kwa ndugu na jamaa waliokwisha kuagiza magari, nikaambiwa ukinunua gari CIF atmost USD 2500 pamoja na kodi haitozidi shilingi mil 7.5 (yaani USD 2500*1500 plus 70% covering taxes & clearing charges). So nikajua nikichukua loan ya sh. 8 milioni ingetosha gharama zote mpaka angalau third party insurance.

Nikapata gari kwa CIF USD 2380 (cresta ya mwaka 2000).

Cha ajabu leo hii nimepata gharama halisi ya kulipa kama kodi ni USD 4700 (kodi tu) sawa na shilingi milioni 7.2. Jamani huu si ni uuaji.

gari nimelipia |CIF 3,700,000 lakini kodi nalipa milioni 7.2?

Naombeni ushauri wakuu, nafikiria kulisusa gari hilo kwa sababu sina hela ya kulipia hayo mamilioni.

wezi tu hao,hawana maana,wanatafuta mahali pa kufia na kulipa kodi za nyumba
 
jamani hawa TRA basi waanzishe kiwanda chao cha magari tuyanunue kwa bei rahisi kuliko hv wanavyotufanyia......unajua TRA ni kama denti anaefanya pepa, huwa wanakimbilia kujibu maswali rahisi ili wafikishe maksi za kufaulu....huku ni kuogopa maswali magumu ya kukusanya kodi ndo mana wanakimbilia kwenye urahisi wa kukusanya kodi kwa kumbana mtanzania wa kawaida while mi-wekezaji inapewa misamaha ya kodi kwa miaka kedekede.jamani gari yako iko melini inafika July 13 naiuzia bandarini bse sitakua na hela ya kuilipia hela yote hiyo.
 
Wakuu naombeni msaada wenu kuhusu hili, naamini kuna mwenye idea, gari yangu inaingia july mwanzoni bandarini dar na nimejaribu kuitafuta kwenye ile excel sheet ya TRA yenye kuonyesha CRSP (bei za kununulia ikiwa mpya) haijaorodheshwa hiyo modeli, ni Subaru Forester GF-SF5 4wd modeli ambayo ndio nyingi mtaani, wanaonyesha SG5 na nyinginezo pekee, sasa mwenye wazo kwamba case kama hii wanai-treat namna gani pls anijuze. Jamani kwa kifupi TRA wametunyongelea mbali, mtu umejiandaa kwa gharama za kawaida unakuja kuambiwa mara mbili yake..!!!! duuh, si ndio mwanzo wa kuacha gari liozee huko.. msaada tafadhalini jamani..
Kama wakikosa sampuli ya KIMA, watachukua hata ya NGEDERE au TUMBILI waifananishie,wote ndo haohao tu
 
Back
Top Bottom