TRA na mfumo mpya wa kufanya valuation of Used Vehicles

ManCity

Member
May 19, 2011
40
14
Tarehe 1 July 2011 TRA wanaplan kuintroduce system yao mpya kwa ajili ya valuation ya used motorvehicles...

Mfumo mpya utakuwa kama ifuatavyo...Used vehicles zitakuwa valued on either ex-factory FOB au market value in local market...

Fuatilia link HII

Nianze na ex factory FOB..

Kwenye mfumo hu, TRA wataestablish database itakayo kuwa na bei za magari kipindi yameingizwa sokoni kwa mara ya kwanza...labda nitoe mfano mana kidogo ina mahesabu

Mfano: Mtu akiagiza gari aina ya Toyota Premio 2001 model..hapo ina maana hii gari imezidi miaka kumi tokea itengenezwe...kwa hilo bei pungufu itakayoruhusiwa ni asilimia 70% ya bei ilipoingia sokoni kwa mara ya kwanza..PREMIO bei yake ya awali sokoni ilikuwa USD 40,000 kwa huko Japan...

Kwa maana hiyo FOB ex factory itakuwa USD 40,000 toa 28,000 (70% of USD 40,000) = USD 12,000 na hiyo ndo itakuwa Customs Value ambayo itakuwa subjected kwenye Import Duty, Excise Duty, VAT na uchakavu (kama upo)....

Kwa namna hiyo kodi jumla itakuwa kama ifuatavyo

Import duty (ID)=0.25*12,000
Dumping Fees (DF) =0.2*(12,000+0.25*12,000)
Excise (E) =0.1*(12,000+0.25*12,000)
VAT= 0.18* (12,000+ID+DF+E)

Hii ni tofauti na bei za sasa ambazo weza kuagiza premio ya mwaka 2001 kwa CIF ya USD 3,000 to USD 3,500...na kodi ingekuwa kama ifuatavyo
ukiweka na uchakavu

Import Duty (ID)=0.25*,000
Dumping Fees (DF) =0.2*(3,000+0.25*3,000)
Excise (E) =0.1*(3,000+0.25*3,000)
VAT= 0.18* (3,000+ID+DF+E)

Market Valuation Method

Kwa market value method watachukua bei za sokoni Tanzania na kutoa profit margin ya asilimia 25 na kutoa gharama za kodi zilizolipiwa ili waeze kupata CIF kipindi gari linaingia nchini...Mfumo huu utatumika pale tu ambapo bei halisi wakati gari linaingia sokoni kwa mara ya kwanza itakuwa ni vigumu kujulikana...

Nachotaka kujua JE nchi yetu imejitoa kwenye World Trade Organisation? Na kama ni hivyo mbona ukiingia kwenye mtandao wa WTO bado TZ ni member country? Mana kwenye makubaliano ya WTO mfumo wa Customs valuation ni tofauti na huu unaoanza kutumika nchini..

Wadau naomba mawazo yenu
 
mancity! mimi nigependa kujua zaidi kuhusu huo mfumo mpya. hebu nielimishe kidogo. huo mfumo unalengo la kupunguza gharama au utaongeza?
 
mancity! mimi nigependa kujua zaidi kuhusu huo mfumo mpya. hebu nielimishe kidogo. huo mfumo unalengo la kupunguza gharama au utaongeza?

Huo mfumo mpya unaongeza gharama maradufu.... Kwa haraka haraka gari ambalo ulikuwa unalipa kodi Tsh 3 millioni, sasa ni zaidi ya sh milioni 6. Na utaratibu huu umeanza toka June 1, 2011.
 
Huo mfumo mpya unaongeza gharama maradufu.... Kwa haraka haraka gari ambalo ulikuwa unalipa kodi Tsh 3 millioni, sasa ni zaidi ya sh milioni 6. Na utaratibu huu umeanza toka June 1, 2011.

Guest321. Kaka naomba utoe darasa kwa mapana zaidi kuhusu huu mfumo maana naona kama inatisha vile.
 
Kama inawezekana mkuu Badilisha Heading.
Ni mjadala mzuri, na ni informative kama ni kweli pia.

Is this is true than we are in a deep shit! Hilo ungezeko ukiweka na Ukiritimba wa TRA pale Bandarini kama mtu huna gari sasa hivi imekula kwako aisee!
 
Jamani tumekufa!
Ukweli ndiyo huu. All saloon cars ushuru umepanda toka 25% up 50% import duty!

  1. ie ilikuwa C.I.F. * 25% sasa itakuwa ni C.I.F * 50%
  2. Chukua jibu la moja * 1.05 kama if < 1500cc au 1.1 if >1500cc
  3. Jibu la pili * mara 1.2 (dumping charge kama gari la kunzia >10yrs
  4. Ndiyo uje uchukue jibu * 1.18 (VAT)
  5. Bado gharama za kutoa gari bandarini (Agent) amabazo hizo ni mpatano ukitoa port charges
Kifupi magari madogo yatapanda mara mbili ushuru kwa sababu ya kodi iliyoongezeka import duty from 25%-50%. Hichi ni kilio jamani.
 
Huo mfumo mpya unaongeza gharama maradufu.... Kwa haraka haraka gari ambalo ulikuwa unalipa kodi Tsh 3 millioni, sasa ni zaidi ya sh milioni 6. Na utaratibu huu umeanza toka June 1, 2011.
Ni kweli kabisa mkuu, hiyo imetokana na kupandishwa kwa ushuru wa kuagiza vitu kutoka nje (Import Duty) toka 25% - 50% hivyo ina maana ushuru umeongezeka kwa 100% kwenye kodi hiyo kwa saloon cars pekee.
 
nahisi kuchanganyikiwa
hawa jamaa wamenitia kidole big time
kwa kodi sijui kama nitatoboa ina maana nijipange upya
hii nchi hii, hali watu wa migodi wanatanua na tax holiday
hapa itakuwa mwendo wa daladala
 
CCM hoyeeee!! Mamaeeeeeee...kabisa. na bado mbona kama inawezekana kupandisha kodi kwa asilimia 100 au asilimia 150,
mishahara inashindikanaje kupandiswa kwa asilimia hata 20 tu???
kuwa na nchi inayojiendesha bila kuwa na raisi kwa miaka 10 si mchezo.... we will pay big time damn! Najichukia sana mimi Kubwa Jinga...
 
hili mbona balaa, em mwenye tarifa kamili kuwa wanaanza lini wa2ambie mana nimezama kule kwenye webu ya tra naona chenga tu, kama bado haijaanza ni bora niende yard nikalipie mwez huu..
 
DAh! keli wenzangu na mimi wa vijigari second hand sasa kwishnei!!!...Tutatembelea bajaji!
 
ila mbona kama habari hii imekosa ukweli, maana nimetembelea tra web sijaona jipya au ndo mambo ya NIMESKIA...!
 
Tarehe 1 July 2011 TRA wanaplan kuintroduce system yao mpya kwa ajili ya valuation ya used motorvehicles...

Mfumo mpya utakuwa kama ifuatavyo...Used vehicles zitakuwa valued on either ex-factory FOB au market value in local market...

Nianze na ex factory FOB..

Kwenye mfumo hu, TRA wataestablish database itakayo kuwa na bei za magari kipindi yameingizwa sokoni kwa mara ya kwanza...labda nitoe mfano mana kidogo ina mahesabu

Mfano: Mtu akiagiza gari aina ya Toyota Premio 2001 model..hapo ina maana hii gari imezidi miaka kumi tokea itengenezwe...kwa hilo bei pungufu itakayoruhusiwa ni asilimia 70% ya bei ilipoingia sokoni kwa mara ya kwanza..PREMIO bei yake ya awali sokoni ilikuwa USD 40,000 kwa huko Japan...

Kwa maana hiyo FOB ex factory itakuwa USD 40,000 toa 28,000 (70% of USD 40,000) = USD 12,000 na hiyo ndo itakuwa Customs Value ambayo itakuwa subjected kwenye Import Duty, Excise Duty, VAT na uchakavu (kama upo)....

Kwa namna hiyo kodi jumla itakuwa kama ifuatavyo

Import duty (ID)=0.25*12,000
Dumping Fees (DF) =0.2*(12,000+0.25*12,000)
Excise (E) =0.1*(12,000+0.25*12,000)
VAT= 0.18* (12,000+ID+DF+E)

Hii ni tofauti na bei za sasa ambazo weza kuagiza premio ya mwaka 2001 kwa CIF ya USD 3,000 to USD 3,500...na kodi ingekuwa kama ifuatavyo
ukiweka na uchakavu

Import Duty (ID)=0.25*,000
Dumping Fees (DF) =0.2*(3,000+0.25*3,000)
Excise (E) =0.1*(3,000+0.25*3,000)
VAT= 0.18* (3,000+ID+DF+E)

Market Valuation Method

Kwa market value method watachukua bei za sokoni Tanzania na kutoa profit margin ya asilimia 25 na kutoa gharama za kodi zilizolipiwa ili waeze kupata CIF kipindi gari linaingia nchini...Mfumo huu utatumika pale tu ambapo bei halisi wakati gari linaingia sokoni kwa mara ya kwanza itakuwa ni vigumu kujulikana...

Nachotaka kujua JE nchi yetu imejitoa kwenye World Trade Organisation? Na kama ni hivyo mbona ukiingia kwenye mtandao wa WTO bado TZ ni member country? Mana kwenye makubaliano ya WTO mfumo wa Customs valuation ni tofauti na huu unaoanza kutumika nchini..

Wadau naomba mawazo yenu

Umesahau devaluation kutokana na depreciation ambayo pia itatumika.
 
huu utaratibu wakuu unaanza 1July au umeshaanza toka 1 June,nina kabajaji kangu kanaingia trh 25 so presha inapanda Presha inashuka
 
Teh teh kazi kwako mwana. Wanadai ulianza as trial tarehe 6 June ila rasmi utakuwa announced July 1st
 
Ngojea niwape summary ya applicable rates za EX-FACTORY METHOD kupata Customs value

0 TO < 1 years 90% of initial price wakati gari laingia sokoni
1 TO < 2 years 85% of initial price wakati gari laingia sokoni
2 TO < 3 years 80% of initial price wakati gari laingia sokoni
3 TO < 4 years 75% of initial price wakati gari laingia sokoni
5 TO < 6 years 70% of initial price wakati gari laingia sokoni
6 TO < 7 years 60% of initial price wakati gari laingia sokoni
7 TO < 8 years 50% of initial price wakati gari laingia sokoni
8 TO < 9 years 40% of initial price wakati gari laingia sokoni
9 TO < 10 years 30% of initial price wakati gari laingia sokoni
>10 years 30% of initial price wakati gari laingia sokoni

Mie naona itabidi tuagize ya between 4 to 5 years mana katika computations zao waliruka afu tupelekane mahakaman.

For further references checkin The Guardian la tarehe 25 February 2011 au mweza peruzi link hii http://www.busiweek.com/11/news/tanzania/593-tra-launches-new-valuation-system-
 
Teh teh kazi kwako mwana. Wanadai ulianza as trial tarehe 6 June ila rasmi utakuwa announced July 1st

Hebu nieleweshe kidogo kaka Trial maanake nini? does it mean waliingiza kuanzia tarehe 6 june kodi yao ilikuwa inakokotolewa kwa huu mfumo mpya? au utaanza kutumika rasmi 1July utakapokuwa anounced? na gari zitakazotozwa hiyo kodi ni zitakazo agizwa kuanzia 1July au zitakazofika bandarini muda huo?
 
Hii ndiyo Tanzania. Huyu mlalahoi anatafutwa jinsi ya kummaliza kabisa! Nadhani itafika wakati wananchi watasema imetosha!
 
Sabayi

Mfumo huu mpya ulianza tarehe 6 June 2011 lakini utakuwa announced rasmi tarehe 1 July. Kwa waliokuwa na bahati ni wale waliopata assessments za kodi tarehe 5 June. Si wengine tutauwawa
 
Haya ndio matokeo ya TRA kukosa ubunifu wa vyanzo vingine vya kodi.
Kila mara wanategemea kupata pesa kwa kupandishia kodi zinazohusiana na magari, fegi na ulabu. Hii inanikumbusha yule mama alitupandishia gharama ya Motor vehicle/road licence miaka michache iliyopita...
 
Back
Top Bottom