Justice Kwanza
Member
- Dec 27, 2017
- 36
- 18
Commissioner wa TRA aliagiza kupitia vyombo vya habari kwenda kuchunguza ili kujua kanisa la FULL GOSPEL BIBLE FELLOWSHIP -lina miradi au Askofu Mkuu Zachary Kakobe kama ana miradi binafsi inayomwingizia kipato ili waweze kupata kodi.
Jumamosi ya tarehe 30/12/2017 barua kutoka TRA ilifika makao makuu ya kanisa FGBF -MWENGE DSM. Na jumanne ya tarehe 02/01/2018, kilitumwa kikosi kikiongozwa na afisa mmoja (.....) ambaye pia ndiye alitajwa kwenye barua kama kiongozi wa msafara.
Walipokelewa na kukawa na mahojiano yalichukua zaidi ya masaa sita. Maana waliingia saa sita kasoro mchana. Walitoa karatasi ilikuwa na listi ya maswali (Questionnaire). Upande wa kanisa alikuwepo Askofu mkuu Zachary Kakobe pamoja na viongozi wa kanisa. Zoezi liliendelea ikafikia maamuzi pia ya kutaka Bank Statements kutokea 2014 mpaka 31/12/2017 katika akaunti zote mbili. Moja ni akaunti ya kanisa la hapa DSM (FULL GOSPEL BIBLE FELLOWSHIP) na ya pili ni akaunti ya Kitaifa ya FULL GOSPEL BIBLE FELLOWSHIP. Pia wakataka akaunti binafsi ya askofu na mama mkuu, wakataka pia akaunti za watoto.
Wiki yote hiyo zoezi la kuangalia kupitia Bank Statements na rekodi za fedha katika akaunti za kanisa. Mwisho wa uchunguzi kama commissioner wa TRA alivyoagiza kuchunguza kama kanisa au Askofu Kakobe wana miradi nje ya sadaka.
Kikosi hicho chini ya Afisa wa TRA (......) baada ya uchunguzi kwa siku kadhaaa, walijiridhisha pasipo shaka kwamba kanisa la FGBF nchi nzima na Askofu Kakobe hawana miradi ambayo ndiyo hutozwa kodi.
Hivyo kiongozi wa msafara huo na kikosi chote walirejesha taarifa na kiongozi huyo akashauri mjadala huo ufungwe.
Kinyume chake baada tu ya huyo afisa kushauri kufungwa kwa mjadala, alipewa uhamisho wa ghafla kwenda mkoani. Na kuteuliwa Kiongozi mwingine na badhii ya maafisa kubadilishwa kwenye kikosi.
Mnamo jumanne 09/01/2018 kikosi kazi kipya. Kilifika kanisani. Kwa awamu walikuja kivingine. Mambo waliyokuja nayo ndiyo ambayo yametupa kujua kuna hila ndani yake.
Walifika wakauliza na kutaka zile bank statements za sadaka, wakapewa. Hawakuridhika. Wakaanza kukagua. Wakaingia kila ofisi kanisani hapo FGBF -Mwenge. Mbaya zaidi walienda nyumbani kwa Askofu Mkuu Zachary Kakobe Kijitonyama, wakapekua mabegi na kutoa nguo moja baada ya nyingine za askofu pamoja na za mama askofu Hellen Kakobe.
Wakachukua simu za mama askofu. Pia wamechukua computer za kanisa. Wakaanza kuhoji matumizi ya sadaka jinsi yanavyotumika.
Bodi ya wadhamini ya kanisa la FGBF walikaa kikao cha dharura alhamisi 11/01/2018, walieleza kila kitu kwamba katika sadaka hakuna matumizi yaliyotumika nje na imani yetu ambayo ni kuhubiri Injili pamoja na uendeshaji wa huduma kama taasisi. Lakini muhtasari na maelezo ya bodi ya wadhamini TRA hakuyapokea, sasa sijui wanataka uthibitisho gani na kutoka kwa nani kama wanakataa vielelezo vya bodi ya wadhamini!!?? Pia waliomba idadi ya washirika na rekodi zao za kutoa zaka na sadaka wakapewa maana kila kitu kiko wazi na kiko nuruni.
Jumamosi ya tarehe 13/01/2018 zililetwa barua ikimtaka Askofu Kakobe na mama wafike TRA -MWENGE leo Jumatatu wameitaka wito. Mnamo saa nne kasoro asubuhi leo jumatatu ya tar 15/01/2018 Askofu Mkuu Zachary Kakobe na mama askofu, bodi ya wadhamini na baadhi ya viongozi wa kanisa wamewasili TRA -Mwenge DSM.
Maswali ya kujiuliza, kama walikosa miradi ina maana wanatafuta kodi kwenye sadaka?? Na iweje wahoji juu uhalali wa matumizi ya fedha ya kanisa wakati bodi yenyewe haina tatizo juu ya hilo??
Mwisho nimalizie kwa kauli ya Askofu Kakobe aliyoitoa jana ibadani
"Shetani wa kuninyamazisha bado hajazaliwa, neno lolote Mungu atakalonipa nitasema kama lilivyo bila kupindisha, kwangu kifo ni promotion ya kwenda kukaa na Baba mbinguni, huwezi kunitishia kifo,nina miaka 62 nikifa leo nitakufa sawa na umri wa Petro na Paulo Mtume, ila nikifa ninapoenda wewe utakuja mbinguni ninakoenda?
Pichani, ni nyumba ya Askofu Kakobe na kibao cha mtaa Kijitonyama DSM