TRA mnarudia kosa lile lile

TRA mnarudia kosa lile lile

pombe kali

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2014
Posts
312
Reaction score
614
kuna zoezi la kukusanya kodi madukani linaendelea uratibu uonaotumika ni kuvamia maduka ya watu na kuchukua vitu imepelekea baadhi ya maofisa kupigwa maeneo ya kivule, ni utaratibu gani huu jamani elimu ya kodi inatakiwa.

Kwa sasa maduka yote yamefungwa nimemuuliza mfanyabiashara mmoja kwanini umefunga akasema hana leseni nikamuuliza leseni ya biashara au leseni ipi? Akasema hajui kifupi maeneo ya kivule jana ilikuwa ni fujo tupu na ikumbukwe huku wanaishi wakurya tujiandae kusikia lolote
 
Kwa hiyo wakishachukua vitu vya "maintaplinywaa" na kodi inajikata humohumo na wasisumbuliwe tena,sivyo?
Mimi ni mhanga wa hao watu😂
Juzi walichukua vitu dukani wakaondoka navyo, jana nikafatilia wakasema hawanipi mpaka nitoe faini 100k, service levy 30k nikate na leseni 150k

Nilichogundua wanataka rushwa halafu wana lugha chafu sanaa.
Leo nikalipia service levy na leseni nikapewa vitu vyangu.

Vitu vikikaa kwa siku 7 wanavitahifisha.
 
Mimi ni mhanga wa hao watu😂
Juzi walichukua vitu dukani wakaondoka navyo, jana nikafatilia wakasema hawanipi mpaka nitoe faini 100k, service levy 30k nikate na leseni 150k

Nilichogundua wanataka rushwa halafu wana lugha chafu sanaa.
Leo nikalipia service levy na leseni nikapewa vitu vyangu.

Vitu vikikaa kwa siku 7 wanavitahifisha.
Hatari sana.Haukupata hata fotografia zao za mjongeo na majina au "aidintitiiz" zao mkuu?Wallah Wabillah Touwfique!
 
kuna zoezi la kukusanya kodi madukani linaendelea uratibu uonaotumika ni kuvamia maduka ya watu na kuchukua vitu imepelekea baadhi ya maofisa kupigwa maeneo ya kivule, ni utaratibu gani huu jamani elimu ya kodi inatakiwa..... kwa sasa maduka yote yamefungwa nimemuuliza mfanyabiashara mmoja kwanini umefunga akasema hana leseni nikamuuliza leseni ya biashara au leseni ipi? akasema hajui kifupi maeneo ya kivule jana ilikuwa ni fujo tupu na ikumbukwe huku wanaishi wakurya tujiandae kusikia lolote
Tena Uku kivule ndio wamefanywa Shamba la Bibi kuvamiwa Maduka ya WATU nakulazimisha Tufanye Wanavyotaka Wao, Ovyoo Sana Awa WATU wa TRA, Tena wanaweza kuja wa 5 Mwenye kitambulisho Cha TRA ni Mmoja tu
 
Hii nchi mtu akishakua na cheo hata ujumbe wa mtaa anafanya anavyojisikia sababu anajua hakuna kitu wananchi watamfanya.
Jirani ana saloon ya kiume walimchukulia mashine za kunyolea na kiti.
Duuh , kama Mtu anakosa nibora kufunga biashara kwa muda ila wasijipe mamlaka kias hcho.
 
Bahati nzuri wafanyabiashara wengi wanafahamu kabisa hawana leseni na vibari vingine vya kufanya biashara.

Hakuna haja ya kuwatetea, kama Sheria zipo zifuatwe na kama hatuzitaki hizo Sheria basi tuziondoe.

TRA Huwa wanapita na gari wanatangaza kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu biashara, ila wengi wanapuuza wanasubiri kufatwa walipie kwa nguvu.

TRA kamateni hao wajinga kama hawataki kufanya biashara kwa mujibu wa Sheria, ifike mahali tuache kuchekeana kuhusu kufata taratibu.
 
TRA watakua wamekosa ustaarabu hao hao wanatangaza kukusanya kwa kuvunja rekodi baadae unasikia ipo sehemu pana ngumi mpaka wengine wanakufa nadhani inatakiwa mjitafakari kwa kutumia njia sahihi Watanzania wanapenda kulipa kodi ingawaje kodi yenu sio rafiki.
 
Back
Top Bottom