TRA mmeshindwa kuwa wabunifu?

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
13,226
26,048
Nawasalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano Tanzania.

Leo napenda kuwaletea hili swali, Je mmeshindwa kabisa kurekebisha mfumo wa mashine zenu za EFD??? Hili tatizo la mashine zenu kutokufanya kazi kwa mtandao kutokuwepo hamjui kuwa mnaikosesha nchi mapato makubwa sana???

Hivi kwa Jinsi mbavyojifanya mna wataalamu, mmeahindwa hata kuziunganisha hizo mashine zenu na mfumo Kama wa TTCL au mtandao mkubwa hapa nchini ili kuzifanya muda wote ziwe zinapata mtandao na kufanya kazi???

Kwa wiki nzima hii nimekuwa nikienda maeneo mbalimbali kununua bidhaa mbalimbali na kupata huduma Ila ninapodai risiti naambiwa mashine haina mtandao. Naomba mjirekebishe na muweke mfumo mzuri kwenye hizi mashine zenu.

Kama mnataka kumsabotage Mama yetu Samia Suluhu Hassan napenda kuwaambia kuwa mtafeli kama hamjaanza. Kama mmefeli semeni tumshauri Mama alete hata kampuni kubwa za mifumo ya kiteknolojia zije kuweka mfumo mzuri na ku update mashine hizi za EFD ili ziwe zinafanya kazi muda wote.
 
Tatizo sio TRA tatizo ni mtandao wa Internet hapa tz unazingua sana hata kwenye nyanja zingine.
 
Tatizo sio TRA tatizo ni mtandao wa Internet hapa tz unazingua sana hata kwenye nyanja zingine.
Kuna watu wanafanya kazi 24/7 kwa mtandao huu wa internet hapa Tanzania. Hakuna kusingizia internet labda kuna shida mahala
 
Tatizo sio TRA tatizo ni mtandao wa Internet hapa tz unazingua sana hata kwenye nyanja zingine.
Unazingua je? Mbona kuna kampuni nyingi tu hapa Bongo zinapiga kazi kwa kutumia mitandao na hazipati shida? Kwa nini TRA? Kama wanatumia teknolojia ya zamani si waseme wasaidiwe??
 
Kuna watu wanafanya kazi 24/7 kwa mtandao huu wa internet hapa Tanzania. Hakuna kusingizia internet labda kuna shida mahala
Nakubaliana na wewe ndugu! Kuna shida mahala, Kama mfumo wao wa kiteknolojia Uko outdated si waseme hata tender itangazwe ije kampuni itakayoleta mfumo bora?
 
Kuna watu wanafanya kazi 24/7 kwa mtandao huu wa internet hapa Tanzania. Hakuna kusingizia internet labda kuna shida mahala
Yale yale ya mradi wa mabasi ya mwendo kasi Dar es salaam....eti miaka sita bado wanajenga mfumo wa ukusanayaji mapata!
Hii ndiyo namna bora ya koungeza mzunguko wa pesa kwa walala hoi!
 
Yale yale ya mradi wa mabasi ya mwendo kasi Dar es salaam....eti miaka sita bado wanajenga mfumo wa ukusanayaji mapata!
Hii ndiyo namna bora ya koungeza mzunguko wa pesa kwa walala hoi!
Mchawi wa maendeleo ya Tanzania ni watanzania wenyewe! Suala nyeti kama la mapato alafu wanafanyia Mzaha. Mashine zao magumashi matupu sijui zinatumia mfumo gani wa mtandao jambo linalozifanya kutokufanya kazi mda mwingi sana na kupelekea nchi kukosa mapato!
 
hii si sawa kabisa sasa hivi kuna mitandao ya kutumia fibre optic inakuwaje taasisi kubwa kutokuwa na access ya high speed internet,na bado kuna fununu hata bandari wamerudi mfumo wa risiti za mkono
 
Kwa wiki nzima hii nimekuwa nikienda maeneo mbalimbali kununua bidhaa mbalimbali na kupata huduma Ila ninapodai risiti naambiwa mashine haina mtandao.
Mkuu, inawezekana tatizo sio la TRA ila hao wafanyabiashara wanataka kukwepa kutoa receipts.
 
hii si sawa kabisa sasa hivi kuna mitandao ya kutumia fibre optic inakuwaje taasisi kubwa kutokuwa na access ya high speed internet,na bado kuna fununu hata bandari wamerudi mfumo wa risiti za mkono
Hii nchi inabidi sasa tumshauri Mama Samia achukue watu nguli from private sector ndo waendeshe hizi taasisi nyeti ili tupate matokeo mazuri.
 
Suluhisho ni kuwapa sekta binafsi wafanye hio kazi, kwani hata TTCL internet ni kama hakuna unalipa na inasusua kama kinyonga
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom