DOKEZO TRA mkoa wa Iringa ni kero kwa wafanyabiashara

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Twin Tower

JF-Expert Member
Jan 13, 2023
2,133
2,986
Tunamuomba kamishna wa mamlaka ya mapato akae na hawa vijana na kuwakumbusha maadili ya kazi.

Kabla hatujachukua hatua kali zaidi za kuwavua ngua na adhabu nyingine, meneja na watumishi wake wajitafakari.

Mbinu wanayotumia kufunga akaunti zetu katika mabenki wasidhani italeta tija katika mkoa.

Kwa sasa imekuwa kero kila mfanyabiashara anazuia akaunti yake kwa ajensi notisi.

Tunatoa onyo kwa mabenki pia hata kama yatekeleza sheria, wakae na TRA ama sivyo waache kabisa kutuomba kuweka fedha katika akaunti.

Sisi tutahamisha ofisi zetu na kwenda kutambuliwa katika mikoa inayojali na kuzingatia namna bora ya ukusanyaji wa mapato.

Rais alishakataza kuzuia akaunti, yeye huyu anapata mamlaka kutoka wapi.

Mzee Kidata, itazame timu yako hasa hapa Iringa.
 
Tax~ (a compulsory contribution to state revenue.) kaombe upewe utaratibu mzuri wa kulipa madeni yako mkuu.
 
Tunamuomba kamishna wa mamlaka ya mapato akae na hawa vijana na kuwakumbusha maadili ya kazi.

Kabla hatujachukua hatua kali zaidi za kuwavua ngua na adhabu nyingine, meneja na watumishi wake wajitafakari.

Mbinu wanayotumia kufunga akaunti zetu katika mabenki wasidhani italeta tija katika mkoa.

Kwa sasa imekuwa kero kila mfanyabiashara anazuia akaunti yake kwa ajensi notisi.

Tunatoa onyo kwa mabenki pia hata kama yatekeleza sheria, wakae na TRA ama sivyo waache kabisa kutuomba kuweka fedha katika akaunti.

Sisi tutahamisha ofisi zetu na kwenda kutambuliwa katika mikoa inayojali na kuzingatia namna bora ya ukusanyaji wa mapato.

Rais alishakataza kuzuia akaunti, yeye huyu anapata mamlaka kutoka wapi.

Mzee Kidata, itazame timu yako hasa hapa Iringa.
Asante kwa taarifa.Uongozi wa TRA unafatilia kwa karibu jambo hili.Tutaendelea kusimamia maadili kwa watumishi wetu ili wakusanye kodi kwa ueledi na kwa uaminifu.Pia tunaomba kila Mlipakodi kutekeleza wajibu wake wa kulipa kodi kwa wakati na kutimiza makubaliano ya kulipa kodi kidogo kidogo kwa wale wenye madeni ya kodi ili kuepuka changamoto za hapa na pale
 
Sasa mzee dawa ya deni si kulipa? Unataka kusema ni wafanyabiashara wote Iringa wamefungiwa account? Mbona nimewauliza jamaa zangu hapo Miami Pub, Texas Lodge, wanasema wao hamna kitu kama hicho? Au kodi mnataka tulipe sisi wachache? Pesa unayo kwa nini usilipe ukaendelea na amani yako .
 
Wengine bila enforcement za hivyo hawalipi kodi.

Ingependeza sana iwapo ingelipwa kwa hiyari bila shuruti.

Kama wanajeuri kwa nini wasiende kufunga maduka kuona kweli wanafanya enforcement? Akaunti za watu zinawahusu nini?
 
Asante kwa taarifa.Uongozi wa TRA unafatilia kwa karibu jambo hili.Tutaendelea kusimamia maadili kwa watumishi wetu ili wakusanye kodi kwa ueledi na kwa uaminifu.Pia tunaomba kila Mlipakodi kutekeleza wajibu wake wa kulipa kodi kwa wakati na kutimiza makubaliano ya kulipa kodi kidogo kidogo kwa wale wenye madeni ya kodi ili kuepuka changamoto za hapa na pale
Ni jambo jema
 
Nawapongeza kwa kujitokeza ila msiishie kujibu hapa.
Mnaweza kuwa na utaratibu wa vikao na wafanyabiashara kujua kero ingawa wengi wataogopa lakini inanafuu.
Muanzie hapo Iringa. Kulipa kodi ni wajibu wa kila anayestahili kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria.
 
Sasa mzee dawa ya deni si kulipa? Unataka kusema ni wafanyabiashara wote Iringa wamefungiwa account? Mbona nimewauliza jamaa zangu hapo Miami Pub, Texas Lodge, wanasema wao hamna kitu kama hicho? Au kodi mnataka tulipe sisi wachache? Pesa unayo kwa nini usilipe ukaendelea na amani yako .

Hahaah mzee wa miami. Hao hata kutoa risiti tu ni shida, ingawa wanajitahidi mara moja moja.
 
wahi kulipa kodi mkuu usiwe unasubiri mwishoni ama kupuuzia, wakija unawaonyesha tu malipo ya kodi ya kila robo uliyofanya, kama ni vat hakikisha unafile returns mapema, hawaji kukusumbua kamwe !!

Hakuna kitu nakiheshimu kama kodi kwenye biashara zangu, najua ni za kinyonyaji nami nafanya nachoweza nilipe nikadiriwe kodi ndogo,

sitegemei kusumbuliwa kwa namna yoyote, nahakikisha kila sehemu ya biashara mambo ya kodi nashughulikia haraka sana hao watu wakija hakuna haja ya kukimbia wala kufunga duka wale "njoo tuongee pembeni" wala mambo za kufungiwa makufuli.

Biashara isiyokupa faida ifunge ama ihamishe ama tia juhudi zaidi.
 
Kupiga marufuku jambo ambalo lipo kisheria ?

Sheria imempa mamlaka kamishna mkuu wa TRA, lakin utekelezaji wake unafanywa na wahuni huku mikoani na wilayani.

Ingependeza walau kamishna mwenyewe kwa mamlaka yake bila kukasmisha kwa mtu awe mwenye kutekeleza sheria hiyo.

Hawa maafisa wayapeleka mafile kwake ili aone uhalali wa kufanya hivyo.

Walau itajenga imani kwa mifumo ya fedha na wanaanchi wakaacha kuficha fedha katika masandarusi majumbani mwao badala yake zikahifadhiwa benki.
 
wahi kulipa kodi mkuu usiwe unasubiri mwishoni ama kupuuzia, wakija unawaonyesha tu malipo ya kodi ya kila robo uliyofanya, kama ni vat hakikisha unafile returns mapema, hawaji kukusumbua kamwe !!

Hakuna kitu nakiheshimu kama kodi kwenye biashara zangu, najua ni za kinyonyaji nami nafanya nachoweza nilipe nikadiriwe kodi ndogo,

sitegemei kusumbuliwa kwa namna yoyote, nahakikisha kila sehemu ya biashara mambo ya kodi nashughulikia haraka sana hao watu wakija hakuna haja ya kukimbia wala kufunga duka wale "njoo tuongee pembeni" wala mambo za kufungiwa makufuli.

Biashara isiyokupa faida ifunge ama ihamishe ama tia juhudi zaidi.

Kodi inalipwa, hakuna anayetaka kukwepa kodi. Kodi ya shuruti daima huwa ni unyonyaji tu. Wao kama kweli wanaona hatulipi hizo kodi waje wafunge maduka.

Hii inaleta impact haraka sana, ili mahojiano yawe hadharani hata kwa viongozi wa juu. Kwa mfano tukiacha kutumia akaunti hiyo kodi wataikusanyia wapi?

Kukimbilia kuzuia akaunti wakati tupo ofisini/madukani ni kuonesha maafisa wameshindwa kazi zao na hawana mahusiano mema na walipa kodi.
 
Back
Top Bottom