TRA kuja huku kuna tatizo

Nyikanavome

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
484
178
Nilipia Road lisence kwa mpesa tokea jumapili (20/12/2015 saa 12:31 pm) na hela ikakatwa nikaambiwa, imethibitishwa kuwa hela yangu imetumwa TRA Motor Vehicle kwenye account waliyonituma kwa ajili ya malipo.

Badala ya system yao kuniletea message ya kwenda kuchukua road licence yangu ikaniambia,maombi yangu kuhusu malipo ya gari hayakuwasiliswa tafadhali jaribu kutuma tena baadaye.

Kimbembe kilianzia hapo, nitume tena baadaye wakati hela imekatwa na haijarudi? Nikaamua kuwapigia customer care yao na wakaniambia, niandike Rudia niache nafasi halafu nitume ile namba ya account waliyonipa na nikafanya hivyo lakini hela haikuingia.

Nimefuatilia ofisi zao za TRA wakatazama wakaona kweli hela imeingia ila inabidi nikaombe refund kwa mkurugenzi mkuu wa TRA process ambayo wameniambia itachukua kama mwezi mzima kurudishiwa hela yangu.

Wakanishauri nichukue hela zangu nyingine nikalipie tena road licence Max malipo wakati nikisubiri refund. Hivi hili sio jipu kweli? Hivi wataalam wa IT wameona hela yangu wanashindwaje kuingiza kwenye account ya gari langu waliyonipa ili waniprintie road licence yangu?. Ni tatizo la wataalam wa IT au ni mfumo mbovu wa malipo ya mtandao kwani walinimbia hela yangu haikuingia kwasababu wakati nalipa mtandao wao ulikuwa down.

Naombeni msaada wenu kama kunauwezekano wa kuziingiza hizo hela kwenye system yenu bila kuomba refund kwa bosi wa TRA.
 
Last edited by a moderator:
TRA na wadau tra hamjaona uzi wangu?
Nilipia Road lisence kwa mpesa tokea jumapili (20/12/2015 saa 12:31 pm) na hela ikakatwa nikaambiwa, imethibitishwa kuwa hela yangu imetumwa TRA Motor Vehicle kwenye account waliyonituma kwa ajili ya malipo. Badala ya system yao kuniletea message ya kwenda kuchukua road licence yangu ikaniambia,maombi yangu kuhusu malipo ya gari hayakuwasiliswa tafadhali jaribu kutuma tena baadaye.

Kimbembe kilianzia hapo, nitume tena baadaye wakati hela imekatwa na haijarudi? Nikaamua kuwapigia customer care yao na wakaniambia, niandike Rudia niache nafasi halafu nitume ile namba ya account waliyonipa na nikafanya hivyo lakini hela haikuingia.

Nimefuatilia ofisi zao za TRA wakatazama wakaona kweli hela imeingia ila inabidi nikaombe refund kwa mkurugenzi mkuu wa TRA process ambayo wameniambia itachukua kama mwezi mzima kurudishiwa hela yangu. Wakanishauri nichukue hela zangu nyingine nikalipie tena road licence Max malipo wakati nikisubiri refund.Hivi hili sio jipu kweli? hivi wataalam wa IT wameona hela yangu wanashindwaje kuingiza kwenye account ya gari langu waliyonipa ili waniprintie road licence yangu?. Ni tatizo la wataalam wa IT au ni mfumo mbovu wa malipo ya mtandao kwani walinimbia hela yangu haikuingia kwasababu wakati nalipa mtandao wao ulikuwa down. Naombeni msaada wenu kama kunauwezekano wa kuziingiza hizo hela kwenye system yenu bila kuomba refund kwa bosi wa TRA.
 
Yamenikuta na mimi leo nimeambiwa niandike barua kuomba refund. Vipi walikurudishia hela yako?
 
Back
Top Bottom