TRA imetoa wapi mamlaka ya kugawa Sukari bure?

TRA imetoa wapi mamlaka ya kugawa Sukari bure?

Mfanyabiashara mwenye kiwanda cha juisi lazima atakuwa na stock kubwa ya sukari kama mojawapo ya bidhaa za kiwanda chake.Je ni wakati gani unatambua aliyehifadhi sukari na aliyeficha?
QUOTE="Mdau Mkuu, post: 16142235, member: 20323"]1. Wafanyabishara nao wamepata wapi mamlaka ya kuficha sukari?
2. Je ni kifungu gani cha sheria kinamruhusu mfanya biashara kuficha sukari?

Yaani mie ndo hapa najishangaaga sijielewi au nalazimisha kutokuelewa.

Kable sijajibu swali lako nakwama katika maswali yangu hayo
[/QUOTE]
Hii sukari ya chai sio ya viwandani,kuna sukari maalum.Ficha upumbavu.
 
Nimesikia taarifa ya habari kuwa,Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) imegawa Sukari yote ya Magendo Mifuko 5,319 yenye thamani ya Zaidi ya Shilingi Milioni 373.5 kwa Taasisi mbali mbali Mkoani Lindi

Sakata la hii sukari lilianza Febuary mwaka huu,unaweza ukajiuliza
Tangu Februari hadi leo nini kilikuwa kinasubiriwa?

Je lini TRA imeanza kugawa BURE vitu vinavyodaiwa kodi?kwa hiyo kesho wakikamata gari ambazo hazijalipiwa ushuru watazigawa bure?

Je, wakikamata mafuta yatagaiwa bure?Haya yanayotokea ni madhara ya nchi kutokuwa na DIRA.

Tunakumbuka miezi miwili nyuma wimbo wa viongozi wote wa serikali kuanzia Dc,RCs,na wakuu wa idara zote za umma ulikuwa ni watumishi HEWA!

Suala la watumishi Hewa halijaisha limekuja suala la sukari sasa hadi TRA ambao sheria inawataka wakusanye kodi,ni mamlaka ya kukusanya kodi,wala sio kutoa vitu ambavyo havijalipiwa ushuru!

Kimsingi hii ni ishara na kielelezo cha Ombwe la uongozi,pamoja na ukosefu wa DIRA

Bila MAONO Taifa huangamia
"Kimsingi hii ni ishara na kielelezo cha Ombwe la uongozi,pamoja na ukosefu wa DIRA" Naunga mkono hilo andiko.

Baada tu ya mihemko inayoendelea kwisha tutaona kilio na madhara halisi ya yanatotendwa sasa hivi na Rais Magufuli.
Kila kitu cha Rais kinarembwa na kusifiwa mpaka mawinguni. Kila kosa lake linatungiwa semi na kuvishwa sukari na lawama kutupiwa wengine. Lakini MUDA utatonesha kina cha ugonjwa huu mauti.
 
Nimesikia taarifa ya habari kuwa,Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) imegawa Sukari yote ya Magendo Mifuko 5,319 yenye thamani ya Zaidi ya Shilingi Milioni 373.5 kwa Taasisi mbali mbali Mkoani Lindi

Sakata la hii sukari lilianza Febuary mwaka huu,unaweza ukajiuliza
Tangu Februari hadi leo nini kilikuwa kinasubiriwa?

Je lini TRA imeanza kugawa BURE vitu vinavyodaiwa kodi?kwa hiyo kesho wakikamata gari ambazo hazijalipiwa ushuru watazigawa bure?

Je, wakikamata mafuta yatagaiwa bure?Haya yanayotokea ni madhara ya nchi kutokuwa na DIRA.

Tunakumbuka miezi miwili nyuma wimbo wa viongozi wote wa serikali kuanzia Dc,RCs,na wakuu wa idara zote za umma ulikuwa ni watumishi HEWA!

Suala la watumishi Hewa halijaisha limekuja suala la sukari sasa hadi TRA ambao sheria inawataka wakusanye kodi,ni mamlaka ya kukusanya kodi,wala sio kutoa vitu ambavyo havijalipiwa ushuru!

Kimsingi hii ni ishara na kielelezo cha Ombwe la uongozi,pamoja na ukosefu wa DIRA

Bila MAONO Taifa huangamia
Ungefanya upekuzi kidogo, usingeleta maada hii hapa. Afadhali ungeleta kwa mfumo wa swali ili uelimishwe!
 
Kama hujui Sheria kaa kimya....

Ina maana hujui kuwa TRA ina mamlaka kisheria

1: Kupiga fine bidhaa iliyoingizwa kimagendo AU

2: Kuitaifisha na kuigawa

3: Kuiuza?

Mkuu great thinker angeenda mbali zaidi kama kutaja na vifungu vya sheria inayowapa mamlaka hayo ili wengi tunufaike bila shaka na mleta mada.Wengi wetu tunaielewa tu sheria ya kuundwa kwao na makusudio.Kama ujuavyo mara kwa mara sheria inaweza kubadilika aidha kupunguza au kuongeza majukumu kwa idara na wizara za serikali yake na sio wengi tutafahamu.Kama mimi naelewa jukumu lao ni kukadiria na kukusanya mapato ya serikali na kutoza ushuru kwa bidhaa watakazokamata zikiingia nchini ki-magendo.Wameruhusiwa lini kutaifisha na kugawa bure sinayo.Wanaruhusiwa kupiga mnada bidhaa zisizokombolewa kwao kwa muda mrefu na watatangaza mnada.Hili la kugawa pengine ni agizo maalum kwa zoezi hili lililopo.Tena tunavyoelewa wengi na kwa sheria ya uhujumu uchumi ya mwaka 1984.ni mahakama tu inayoweza kutaifisha mali baada ya mtuhumiwa kushindwa mahakamani.Ukisoma michango yangu mingi iliyotangulia nimependekeza kwa serikali na hata kwa raisi kutogawa bure hizo bidhaa badala yake ziuzwe kwa bei halali na hela ihifadhiwe hazina akaunti maalum zikisubiri watakaoipeleka serikali mahakamani/au wao kupelekwa na serikali nao kwa kuwatumia wanasheria waelewa,werevu kama kina Lussu n.k wakashinda kesi.Malipo yao yatoke fungu lililopo hazina.Hata hivyo zipo gharama za kuhamisha bidhaa hizo na kuzigawa.Wengi tunaelewa udhaifu wa wanasheria wetu wa setikali kushinda kesi mahakamani.Katika kesi kumi watashinda moja huku nyingine zote zikitupwa na mahakama kwa mapungufu mbali mbali.
 
Nchi hii ya mazingaombe tu. Ninyi dira ipi mlikuwa nao au Lowassa aliyoitela ndani ya wiki moja ili muuendeshe taifa.

Cha msingi soma sheria na kanuni za TRA hayo yote yapo.
Nimesikia taarifa ya habari kuwa,Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) imegawa Sukari yote ya Magendo Mifuko 5,319 yenye thamani ya Zaidi ya Shilingi Milioni 373.5 kwa Taasisi mbali mbali Mkoani Lindi

Sakata la hii sukari lilianza Febuary mwaka huu,unaweza ukajiuliza
Tangu Februari hadi leo nini kilikuwa kinasubiriwa?

Je lini TRA imeanza kugawa BURE vitu vinavyodaiwa kodi?kwa hiyo kesho wakikamata gari ambazo hazijalipiwa ushuru watazigawa bure?

Je, wakikamata mafuta yatagaiwa bure?Haya yanayotokea ni madhara ya nchi kutokuwa na DIRA.

Tunakumbuka miezi miwili nyuma wimbo wa viongozi wote wa serikali kuanzia Dc,RCs,na wakuu wa idara zote za umma ulikuwa ni watumishi HEWA!

Suala la watumishi Hewa halijaisha limekuja suala la sukari sasa hadi TRA ambao sheria inawataka wakusanye kodi,ni mamlaka ya kukusanya kodi,wala sio kutoa vitu ambavyo havijalipiwa ushuru!

Kimsingi hii ni ishara na kielelezo cha Ombwe la uongozi,pamoja na ukosefu wa DIRA

Bila MAONO Taifa huangamia
 
wasiwasi wangu mimi ni kwamba je ubatizo wa kuita sukari iliyokamatwa ni ya magendo ni sahihi?. nikifika hapa, naishiwa nguvu na tafsiri ya kisheria. ninaunga mkono wazo la mh. Raisi kuwa sukari iliyofichwa itpelekwe sokoni, bali natofautiana pale anaposema sukari igawiwe tena bure. jambo halitofautiana sana na samaki waliokamatwa baharini na kisha kugawiwa kwenye taasisi hizohizo zilizipewa sukari. aidha na mwomba Rais wetu maisha marefu na afya njema katika kulitetea Taifa leo. ombi langu ni kuwa tufanye yooooote lakini utawala wa kisheria iwe ndy nguzo letu.
 
Ndugu yangu nanyaro pole kwa yanayotokea watanzania ni watu wa pekee!
Msrmaji mmja kasema vyema kuwa ni mahakama pekee ndiyo yeye mamlaka hayo. Nafikiri hilo ni jema kwani tumesahau ya samaki wa magufuli?!
 
Ilitakiwa ipigwe mnada ili serikali ichukue kodi yake,lakini sio kuigawa kwenda kwenye taasisi ambazo tayariz zimetengewa pesa ya kununua sukarit
 
Back
Top Bottom